"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, February 11, 2010

Mwili wa mwanamke kwa mwezi!

Mzunguko wa mwezi (menstrual cycle) ni moja ya maajabu katika mwili wa mwanamke.
Kwa kuchunguza ushahidi ulijificha katika mzunguko unaweza kujua kwa nini mwanamke hufurahia au kutofurahia tendo la ndoa siku kadha ndani ya mwezi mmoja.

Jambo la msingi ni kukumbuka kwamba kuna hormones 4 muhimu ambazo hufanya kazi kama timu kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa katika mzunguko wa mwanamke (yaani siku 28)
Hormones hizo ni Estrogen, Testosterone, Progesterone na Oxytocin.

ESTROGEN
Mwanamke anapoanza mzunguko wake wa siku 28 (yaani siku ya kwanza baada ya kumaliza MP) mwili wake huanza kuzalisha hormone ya estrogen.
Hii hormone ambayo huhusika moja kwa moja na kutengenza mazingira mazuri ya tendo la ndoa (sex) na pia kuimarisha na kuweka sawa reproduction system iwe na afya.
Pia hii hormone huandaa ubongo na mwili kwa ajili ya kushika mimba.

Estrogen humfikisha mwanamke hadi siku akiwa tayari kwa ovulation na hii hormone huweka mazingira ya uke katika hali ya juicy and smells beautiful na kumpa mwanamke uhitaji wa sex kwa kiwango cha juu.

TESTOSTERONE
Hii ni hormone ambayo huchochea hamu ya mapenzi (desire for sex), kukua kwa nywele sehemu zote za mwili, na nguvu (energy) ingawa mwanamke ana kiwango kidogo cha testosterone kuliko mwanaume.
Hormone hii huwa katika kiwango cha juu sana inapofika siku ya 7 hadi 14 ya mzunguko wa mwanamke na hii hufanya estrogen na testosterone kuunganika siku ya ovulation.
Hii ina maana mwanamke akitumia vidonge vya uzazi wa mpango huweza kupunguza kiwango cha testosterone na matokeo yake kupungukiwa na libido yaani hamu ya tendo la ndoa.

PROGESTERONE
Hii ni hormone ambayo huzalishwa kwenye ovaries na huja kwa full force siku za 14 hadi 28 ya mzunguko wa mwanamke.
Hii hormone husaidia kuimarisha (thickening) ya uterus kwa ajili ya kupokea kiumbe kama mwanamke ameshika mimba.
Kama mwanamke amepata mimba siku ya ovulation basi hii hormone husaidia fertilization ya yai, kama hakupata mimba basi hii hormone kuhakikisha uke unarudishwa katika yali tofauti na kile estrogen/testosterone vimefanya na kupunguza hamu ya sex na uke huwa more sensitive kiasi kwamba msuguano (thrusting) wakati wa sex huweza kusababisha mwanamke ajisikie uncomfortable.

OXYTOCIN
Hii ni hormone ya connection na bonding.
Mwanamke huzalisha kwa wingi akiwa kwenye labour wakati wa kujifungua mtoto/watoto.
Husaidia mwanamke kufanya bonding na mtoto aliyezaliwa pia uzalishaji (stimulation) wa maziwa ya kumnyonyesha mtoto.

Ukimbukwe kwamba ukaribu wa kimapenzi (intimacy) kwa mwanamke na mwanaume huzalisha hormone ya Oxytocin.
Pia wote mwanaume na mwanamke wanapofika kileleni (orgasm) huzalisha hii hormone ili wajisikia closer baada ya tendo la ndoa.

+++++++++++++++++++++++

1 comment:

Anonymous said...

Hello Kaka Mbilinyi,
Hii imenibariki sana.

Ubarikiwe,