"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, February 18, 2010

Nenda Mbali!

Kubadilisha mazingira au eneo au mahali ni jambo la msingi sana kwa ajili ya wanandoa kufurahia ukaribu kimapenzi (intimacy).
Inajulikana kwamba kwa wanandoa kwenda mbali na nje ya nyumbani kwao let say Motel huweza kuwafanya kupata msisimko mkubwa na tofauti wa kimapenzi.

Sababu za msingi ni kwamba:
Kunakuwa na privacy kwa wahusika yaani mke na mume wanaweza kuvaa wanavyotaka.
Pia kunakuwa na uhuru (freedom) kwani mkiwa sita kwa sita unaweza kupiga kelele, unaweza kuugulia kimapenzi, mnaweza kucheza, kucheka bila majirani wala watoto kuwasikia.

Hakuna kuingiliwa na kitu chochote kama ndugu kuwatembelea au watoto kuwaita kwa ajili ya kitu chochote. Pia kama simu zimezimwa ndo mnakuwa dunia yenu wenyewe.

Zaidi na kubwa kuliko yote ni kwamba wanandoa huwa mbali na masumbufu ya maisha kama vile kupika, kuangalia watoto, kutembelewa na ndugu au majirani nk.

Ukiona suala la tendo la ndoa linakupa maumivu kwa maana kwamba hakuna anayeridhika au wewe mwenyewe huridhiki ufahamu kwamba na ndoa yako itakuwa na maumivu.
Hata hivyo hujachelewa kurekebisha mambo, anza sasa.
Wanandoa wengi hujikuta katika wakati mgumu wa kuwa karibu kimapenzi, inawezekana mmoja au wote hujisikia wamechoka muda wote, au wanajisikia msongo wa mawazo au basi tu hakuna mwenye hamu na mwenzake, no feelings.
Haitakiwi kuwa hivyo, naamini ingekuwa hivyo wala msingekubaliana kuoana.
Je, ule moto wa mapenzi mmeuzima vipi?

3 comments:

Anonymous said...

Kaka,
Hii nuimeikubali kweli picha hii huwa inajijia kwenye kichwa changu kwamba mara nyingine mtu unatakiwa kuhama mazingira ua kubadilisha mazigira ili kujitafutia utulivu wakipekee na kweli hii husaidia kuenjoy kwa nama ya ajabu kukumbushiana mambo mengi na kuongea vitu vingu sana.
pia kupeana habari mawazo hata kuonyana pia.
Kweli hii inafaa kuelimisha.

AM

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Am,

Upo sahihi kabisa nab kamam wanandoa tunahitaji kuwa na wakati kama huo angalau mara kadhaa au mara moja kwa mwaka inaweza kusaidia kuimarisha ndoa zetu.

Jiulize tangu umeolewa acha ile wakati wa honeymoon je, ni wakati gani mwingine wewe na mume wako au mke wako mmewahi kwenda mbali kwa ajili ya kuenjoy?

Upendo daima

Anonymous said...

Hii hata mimi naikubali, mara nyingi mazingira ya nyumbani yatufanya wanandoa tuwe busy kiasi kwamba wakati wa faragha tunakuwa tumechoka sana.

Mungu akubariki kwa kutuelimisha wanandoa.