"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, February 17, 2010

Nimechoshwa!

Je, unajisikia frustrated linapokuja suala la sex katika ndoa yako?

Ukweli lazima uongelewe na kuna ulazima wewe unayesoma sasa hivi kujibu na kuwa mkweli.

Kama jibu lako ni NDIYO basi swali la pili ni kwa nini upo frustrated?

Hebu tuangalia sababu kubwa tatu za msingi

Kwanza inawezekana umekuwa na matarajio yasiyo halisi,

Pili inawezekana kuna uchoyo na ubinafsi au umimi,

Na tatu inawezekana humuelewi mwenzi wako.

Hapo ndipo kwenye source ya matatizo ya mume na mke chumbani kama kungekuwa hakuna unrealistic expectation usingekuwa unakuwa disappointed na hali ya mapenzi na mume wako au mke wako

MATARAJIO YASIYO HALISI

Baadhi ya njia za kukuwezesha kuondoa matarajio yasiyo halisi na kuondoa frustration ni pamoja na kuondokana na matumizi ya mikanda ya ngono ambayo wanandoa wengi hutumia eti kujifunza.

Hii ni pamoja na kuangalia pornography.

Video za ngono hazielezei maisha halisi ya mapenzi katika ndoa na kuangalia kunakufanya ujiweke katika kundi la failures kwani hakuna mwanamke ambaye yupo na afya njema kihisia anaweza kufanya kama wanavyofanya Wanawake wa kwenye mikanda (porno) kwani wao wanafanya business na wanaigiza.

Porn stars wao wanatengeneza pesa kwa kuigiza na kuwakamatisha wanaume wenye tama na ni laana ya mapenzi (intimacy).

Biblia inafundisha kutoa ndiyo msingi kwa ajili ya kufurahia mahusiano ya ndoa. Ili kufurahia tendo la ndoa kwanza huanza kwa upendo wa kweli na upendo wa kweli ni kwanza kumpa au kufanikisha mahitaji ya mwenzi wako kwanza na wewe baadae.

UCHOYO NA UBINAFSI

Kama wewe ni mchoyo, mbinafsi (selfish), maisha yako yatakiwa balaa, huwezi kukwepa kuwa na frustrations linapokuja suala la sex na mwenzi wako.

Kwani mzunguko wa maisha yako ni kujipa raha wewe tu na kila kitu kuvutia kwako na si mwenzi wako.

Mtazamo wa aina hii ni adui na huweza kuharibu ukaribu wa mapenzi baina ya wanandoa.

Kuwa karibu kimapenzi (intimacy) kwa wanandoa huweza kusababisha kuwa na sex inayoridhisha na pia maisha bora kwa kila mwanandoa.

Jambo la msingi unahitaji kubadilika kabla huharibu ndoa yako kwanza jikubali kwamba wewe ni selfish na anza kumpa priority mke wako au mume wako kwanza.

Pili lazima uwajibike kwa yule unampenda yaani mke wako au mume wako na kubali kubadilika inawezekana.

Na mwisho confess kwamba umekosa na sasa unaanza plan mpya maisha mapya.

KUTOMWELEWA MWENZI WAKO

Sababu kubwa ya wengi kuwa frustrated na ndoa kimapenzi ni suala la kutomfahamu vizuri mke au mume.

Ukiwa na mtazamo kwamba mke wako au mume wako ana mahitaji sawa ya kimapenzi kama wewe basi hilo tayari ji tatizo kubwa.

Mungu alituumba tofauti kati ya mwanamke na mwanaume na lazima mahusiano yetu yakubaliane na hiyo design ambayo Mungu aliiweka.

Kumbuka mahitaji ya mwanamke na mwanaume ni tofauti na ni muhimu kila mmoja kutimiziwa mahitaji yake.

Mwanamke huhitaji LOVE na mwanaume huhitaji RESPECT

2 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Bwana Mbilinyi. Ni mara yangu ya kwanza kupita hapa kibarani kwako. Ni moja kati ya vibaraza vizuri vyenye ujumbe wa kuelimisha sana. Hongera.

Kila mtu yuko tofauti na bila kufahamu mahitaji halisi ya mwenzi wako katika tendo hili, ni vigumu kuwa na fumano la kweli. Ni vizuri kupeana viashiria (tips) kuhusu mambo ambayo huuchochea moto wa mwenzako mpaka volkeno ikaripuka...Ngoja niishie hapa

Anonymous said...

Kaka Masangu,

Nashukuru sana kwa kupita hapa na ninakukaribisha sana.

Nimepita kwako pia na nimeweka blog yako kwenye list yangu ili niwe nakupata kirahisi.

Asante sana kwa comments na Ubarikiwe.

Upendo daima