"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, February 19, 2010

Nitajuaje tunafanana kitandani?

Mimi ni kijana wa kiume naishi Arusha kwanza nashukuru sana kwa masomo ambayo tunajifunza kupitia blog yako swali langu la msingi ni kuuliza hivi “Kama huruhusiwi sex kabla ya ndoa, je nitajuaje ninayeoana naye tunafanana katika kiwango cha kuhitaji sex?”

Kaka nashukuru sana kwa swali lako zuri ambalo linaonekana ni kama mtego, na kibinadamu linaonekana kama lina hekima fulani hivi hata hivyo mbele za Mungu ni swali rahisi mno.

Jambo la msingi kwenye swali lako ni kukuuliza wewe mwenyewe ni kipi kigumu hapo? Unataka kujua kiwango kwa kufanya sex au kwa sharing ya mawazo na ukaribu kufahamu anajisikia vipi au unajisikia vipi kuhusiana na suala zima na ninyi kuwa pamoja.

Kuna mambo makuu mawili kwenye swali lako yaani tamaa ya mwili na upendo wa kweli ambao hubebwa na uvumilivu, subira na imani katika Mungu na kumpenda mtu kwa ndani na si mwili tu.

Je ukitembea naye (sex) ndipo utajua mnafanana uhitaji wa sex? Au kukaa naye na kuongea naye na kushare ndoto mawazo na feelings kutakusaidia kufahamu ni mtu wa aina gani.

Unaweza kufahamu kufanana kwa kiwango cha sex kwa sharing ya kimawazo na hisia katika kuwasiliana kwenu na si kwa kupeana mwili.

Kupeana sex kabla ya ndoa hakuwezi kutatua tatizo lolote au kuwa jawabu la kuwasaidia kujuana kama mpo mnafanana kwenye suala sex baada ya ndoa.

Kupeana sex kabla ya ndoa huweza na husaidia kufunika matatizo kati yenu na hayo matatizo huweza kuwa juu ya meza baada ya ule upendo wa kwanza (illusions, fall in love) kwisha.

Na kinachotokea ni kwamba baada ya kupeana mwili na fall in love kwisha unachobakiwa ni mtu ambaye humjui kabisa.

Jambo la ajabu lingine ni kwamba vijana wengi wa leo hawana lolote, akiona mpenzi wake anasuasua basi wanahongana kwa sex ili warudiane (eti kuleta connection upya) ukweli ni kwamba hiyo connection ni ya mwili tu na ni kwa muda mfupi.

Hata hivyo kuweka msingi wa mahusiano ya ndoa kwa kipengele cha kufanana kwa uhitaji wa sex ni hatari kubwa kwani ndoa ni zaidi ya kupendana na mapenzi.

Kama ukisubiri sex hadi ukiolewa au kuoa suala la kufanana kwa kiwango cha kuhitaji sex itakuwa si tatizo kwani utakuwa hukuwa na uzoefu wowote ambao unaweza kuulinganisha, kwani uzoefu wote huwa baada ya ndoa na baada ya ndoa tayari ni mke na mume, wote mpo wapya.

Kwa ufupi ukiona umefanya sex kabla ya ndoa yafuatayo huweza kutokea

Kwanza uchumba unaweza kuvunjika muda wowote,

Pili uliyenaye anaweza kukwambia anataka kumuoa au kuolewa na bikira

Tatu unaweza usiwe mtu wa furaha katika ndoa yako,

Nne unaweza kuachwa baada ya ndoa.

Tano unaweza kuanza kutoka nje ya ndoa (adultery)

Sita unaweza kudanganywa kwa kuolewa au kuoa kwa sababu potofu.

Saba unaweza usifurahie mapenzi katika ndoa yako.

Nane unaweza kujisikia hatia (guilt) katika ndoa yako.

Mwisho ni wazo zuri sana kusubiri sex hadi ukioa au kuolewa na yule unataka kuoana naye na kuishi naye maisha yako yote. Kwa njia hii wote mtafurahia uzoefu mpya kabisa pamoja na ni kweli hicho kitendo kitakuwa so special hasa ukizingatia kwamba kila mmoja alivumilia na kusubiri kwa muda mrefu hadi mmeoana.

Ni kweli sex lilikuwa wazo la Mungu na Mungu aliumba sex na sex ni kitu kizuri, tatizo linakuja pale binadamu anapo distort na kukataa standards halisi ambazo Mungu ameweka na matokeo yake ni uharibifu na matatizo.

Hivyo tunaweza kuchagua kufanya mambo katika njia ya Mungu na tukabarikiwa au tukachagua kufanya kwa njia zetu zilizopotoka na tukaangamia

Mithali 16:25

2 comments:

Anonymous said...

Asante sn Mbilinyi kwa ushauri wako mzuri!Mimi ni binti nina mchumba tunatarajia kufunga ndoa,ila nina huzuni sn moyoni maana mchumba wangu amekuwa akisisitiza sn juu ya suala la sex,sijui nifanye nini!
Pili mchumba wangu hataka kunipeleka nyumbani kwake nikapafahamu bali yy huwa anakuja kwakngu nikimuuliza juu ya hilo ananiambia atanipeleka tu niwe na subira!kweli hapo kuna ndoa kaka yangu?

Lazarus Mbilinyi said...

Dada!

Pole sana kwa huzuni unayokumbana nayo, kupenda kitu cha ajabu sana na ni kitu kizuri hata hivyo kuna wakati inabidi uwe makini na kama kungekuwa na kufunga break na kujichunguza basi wewe unatakiwa kupunguza speed na kuchunguza mambo ya msingi kwanza.

Ingawa nimeeleza sana kwenye bandiko langu lenye kichwa "ANANITAKA" kwa nyongeza na kutokana na swali lako kwanza unasema anakutaka sex kabla ya ndoa, na umesema mnataka kufunga ndoa swali la msingi kama mnataka kufunga ndoa je, kwa nini hawezi kuvumilia? ukimuuliza anasemaje?

Pia kama anakuona kwa sababu anataka sex basi ni sababu potofu kwani hatuoi kwa sababu tunataka sex bali tunaoa ili kuondoa upweke na katika kumpata mwenzi wa kukuondoa upweke kuna package ya sex, kama sex peke yake ndiyo sababu ya kukuoa basi hapo kuna tatizo kwani ndoa si sex tu bali sex ni kipengele kimoja kati ya mia.

Umesema kwako anakujua na huwa anakuja lakini kwake hataki uende na mnataka kuoana.

Dada inabidi uwe makini, wewe si rahisi kiasi hicho yaani akutake sex na hata kwake hataki uende je, ina maana anataka hata sex iwe hukohuko kwake? kwa mbali inaonekana kuna tatizo.

Tafuta rafiki zako au rafiki yako unayemwamini then peleleza anakaa wapi, mtaa gani na nyumba gani na tafuta siku ambayo una uhakika yupo kwake then mmshukie kama mwewe hapo kwake uone nini kitatokea, isije kuwa anataka kukuoa kumbe anatunzwa na rafiki yake au ana mke.

Hata hivyo wewe ndiye unamjua zaidi kuliko sisi wengine, na ukijiuliza ndani ya moyo wako unaona kila kitu kipo shwari kabisa yaani unajiona una amani naye mia kwa mia?

Pole sana