"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, February 9, 2010

Siri zingine!

Unaficha siri kwa mchumba wako "Eti huna mtoto wakati yupo kijijini na afya tele" Ndoa ni institution ambayo ni takatifu na hujengwa kwa msingi wa kuaminiana (trust/respect).
Huu msingi wakati mwingine hujikuta una hofu ya kubomoka na kusambaratika kwa vitu vidogo vidogo kama suala la siri katika ndoa.

Siri katika ndoa huweza kuharibu msingi wa ndoa ambayo imejengwa vizuri na kuonekana mbele za watu ipo imara.
Ni kweli inawezekana mke wako au mume wako hatakiwi kujua kila kitu kuhusu wewe vile umefanya ana unajua kila siku inayopita duniani hata hivyo ukiangalia kwa undani zaidi siri unazoficha kwa mume wako au mke wako zinaweza kukupeleka pabaya.
Iwe siri nzuri au siri mbaya kumbuka kwamba inaweza kuweka madoa mabaya sana kwenye ndoa yako.

Jambo la kujiuliza ni je, kwa nini unaficha hizo siri?
Kumbuka kiapo (vow) namna ulivyoahidiana wakati mnaoana kwamba ninyi ni kitu kimoja na kama unajikuta unajitahidi kuficha siri basi unaelekea kwenye big trouble.

Je, unaficha matumizi ya pesa?
Kumbuka siri katika ndoa mara nyingi ni hatari kwani itafika siku utaangukia pua, kwa mfano kama unaficha namna unatumia pesa na madeni yanazidi kuingiliana ipo siku wanaokudai watakuja kuuza nyumba ndipo mke au mume atajua kulikuwa na tatizo na utakuwa umeshachelewa!
Inawezekana unamficha mchumba wako kwamba huna mtoto wakati mtoto unaye, siku akigundua hata kama mmeoana miaka 5 au 10 gharama ya kurudisha trust itakuwa kazi ya ziada, Utajuta!

Inawezekana unaficha siri kwamba mtoto uliyenaye si wa huyo mume wako na umeamua kula jiwe, hata hivyo siku akigundua hapata tosha!
Kumbuka
“The earlier the better!”

Je, ni siri kiasi gani unamficha mke wako au mume wako au mpenzi wako?
Kumbuka mahusiano ya kweli hujengwa kwa trust, kuficha siri ni moja ya bleach ya trust na zaidi kuliko yote hakuna siri duniani.

"A secret is like a dove: when it leaves my hand it takes wing".
Arabian Proverb

2 comments:

Anonymous said...

Kaka kweli hii nimeshuhudia watu wakiachana kisa mume alikuwa na mtoto akamficha mke wakati wa uchumba mpka wakaoana.
Kali ya mwaka ilikuwa mWakwa 2006 rafiki yangu mmoja aliolewa kumbe alimficha jamaa kama ana mtoto wa kiume nje ya ndoa mpaka kamuoa na mtoto alikuwa kijijini kwa bibi yake yeye mwanamke. Basi wakafunga ndoa na wakiwa ndani ya ndoa ukapita mwaka wa kwanza hawana mtoto then ukapita mwaka wa pili hawana mtoto,mwaka wa tatu hakuna mwishowe siku moja mume akamuita mkewe akamwambia leo ujiaandae nakupeleka dinner mpenzi, mkea kafurahi kweli wakaenda wakala wakapata na wine.
Mume akawa anawaza jinsi ya kumwambia mke kuhusu mtoto mkubwa tu wa kiume ambaye yupo kwa babu na bibi kijijini, waliporudi nyumbani huku wote wakiwa wamejawa na furaha tele; Mume akamwambia mke ni miaka mingi sasa hatujabarikiwa kupata mtioto,ila nina kitu kimoja kinanisumbua sana moyoni mke wangu.
Mke akajibu nini tena mume wangu! Mume akasema unajua nimewa sana nimekaa sana naona naumia sana bora leo nikuelee wazi.
Mimi naitwa baba James , mke akasema kivipi akasema ni miaka ya nyuma nilizaa na dada mmoja na huyo dada kaolewa ila nilimchukua mtoto na kumpeleka kwa wazazi wangu.
Mke akamuuliza ndo yule mtoto uliyesema ni wa marehemu dada yako unamlea wewe kakuzoea kama baba KAJIBU NDIYO.
Mke akafurahi sana na kuanza karukaruka kwa vigelegele na kelele kubwa. Mume akashituka na kumwambia umefurahishwa na nini? Akajibu kwamba nimefurahi kwa kuwa James amepata dada yake Stella wa kucheza naye kwani na mimi nina mtoto yupo kwa mama yangu kijijini.
Mume akasema ndo Yule ulisemaga ni yatima na mama yako anamtunza? Akajibu ndiyo na mume akazimia na siri zikawa siri kwelikweli

Lazarus Mbilinyi said...

Hao walikutana wote kiboko!