"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, February 15, 2010

Tunachonga mdomo ... Hatufanyi!

Mke na mume huishia kuishi kama traffic police barabarani bila kuwa na muda wa kuongea pamoja.

Kama unavyosikia kwamba siku za leo ndoa nyingi huishia katika talaka huku zikiacha uchungu kwa wanandoa wenyewe na watoto ambao wanakuwa confused na jambo lililotokea kwa wazazi wao. Usikubali hili litokee kwako haijalishi ndoa yako ipo katika wakati mgumu kiasi gani au ipo katika afya njema kiasi gani au kwanza ndo unafikiria suala la kuoa au kuolewa.


Huwezi kuwa Engineer au Doctor au successful business man/woman over night, lazima uwekeze muda na juhudi ya kutosha ili ifike hapo hata ndoa ni hivyo hivyo kwamba ni kazi huweza ukakaa na kuishi kizembezembe ukawa na ndoa nzuri.

Jambo la msingi ni kufuata tips ambazo kila siku tunakumbushana ili kufanyaia kazi katika ndoa yako hebu leo tuangalia suala la mawasiliano.


Tafiti nyingi zinaonesha kwamba wanandoa wengi katika nchi zilizoendelea kama Marekani na Canada huweza kuwa na mawasiliano (kuongea pamoja) ya wastani wa dakika 17 kila week.

Kama kwa wiki mke na mume wanaongea kwa dakika 17 tu je ni zinatosha kuweza kuelezea au wasilisha matatizo unayokutana nayo? Hamu, hofu au vitu vinavyofukuta ndani ya moyo wako kuhusu mume wako au mke wako kama vile masuala ya sex? Bila kuwasiliana kinachofuata ni frustration kujaa ndani yako na huweza kuathiri ndoa.

Je, kuongea kwa dakika 17 tu unaweza kuwasiliana topic ngumu ambayo inatakiwa kuongelewa openly na kwa muda wa kutosha?

Kutokana na kuhangaika na maisha mke na mume huishia kuwa kama polisi wa barabarani anayeongoza magari (Traffic police) ndani ya nyumba zao.

Wengi hukiri na kuongea kwamba wanataka kuwa na muda na wake zao au waume zao hata hivyo hujikuta muda wao mwingi wanatumia kufanya mambo mengine na si kuongea na waume zao au wake zao.


“Hii ni kumaanisha kwamba kufahamu jambo siyo kulitenda”


Kufahamu kwamba unahitaji muda wa kuongea na mke wako au mume wako ni vitu tofauti na kutenda jambo la msingi ni kutenda siyo kuongea na kuahidi tu.

Kama kuongea na mume wako au mke wako ni number one priority basi inabidi uweke kwenye kitabu chako au ratiba yako suala la kuongea na mume wako au mke wako liwe namba moja na utekekeze.


“The reason most goals are not achieved is that we spend our time doing second things first,’


Huo ni ukweli na unauma kama kupigwa msumari kichwani.

Tunasema mdomoni linapokuja suala la ndoa na vitu vingine, ndoa ni namba moja na tunaishia kutumia muda wetu kufanya mambo mengine.

Kuipa ndoa kipau mbele au kuyapa mahusiano yako na yule umpendae first priority ndiyo siri kubwa ya kurudisha maongezi mazuri na muhimu yanayokosekana mkiwa pamoja.

No comments: