"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, February 12, 2010

Umri Nao......

Siku hizi wakifikisha miaka 50 wanabugia ili kuongeza libido! Kama mwili wa mwanaume unavyozalisha kiwango kidogo sana cha estrogens pia mwili wa mwanamke huzalisha kiwango kidogo cha Testosterones.
Hormone
ya testosterone huupa mwili libido na energy, huimarisha misuli na bones na kuhakikisha chuchu na kisimi cha mwanamke vyote vinakuwa sensitive kwa ajili ya
sexual pleasure.
Tunapoongeza umri miili yetu hupunguza uzalishaji wa androgens (testosterone, estrogens and progesterone).

Miaka 10 hadi 19
Kwa mara ya kwanza mwanamke (binti) hupata MP.
Kunakuwa na fluctuations za balance za hormones na hujikuta yupo emotional.
Uso hujikuta upo na chunusi.
Pia huwa na mood swings.

Miaka 20 hadi 29
Huu ni umri ambao hormones huwa katika kiwango cha juu (best).
Hakuna kitu rahisi kama kupata mimba.
Hormones za estrogens na testosterones huwa makini kama saa.

Miaka 30 hadi 39
Kutokana na mabadiliko ya uchumi wa dunia sasa wanawake wengi wanaanza kuzaa wakiwa na umri wa miaka 30.
Umri huu ndio umri ambao wanawake wengi huwa wameshaolewa na wanao uzoefu wa kutisha kuhusu tendo la ndoa.
Bado mwili unakuwa na kiwango cha juu sana cha estrogens na testosterones kiasi kwamba wanakuwa na libido ya juu na matokeo yake ni moja ya kundi linalo enjoy sex kwa full speed.

Miaka 40 hadi 49
Ukiwa na umri wa miaka 40 sasa unakuwa umepoteza nusu ya kiwango cha testosterones zile ulikuwa nazo ukiwa na miaka 20.
Mwanamke anapofikia miaka 45 maandalizi ya menopause huanza (perimenopause).
Hiki ni kipindi ambacho mwili unaanza kujiweka sawa ili kufanya shutdown ya reproductive system.
Hormones za estrogens na testosterones
huanza kupungua kwa kasi ya ajabu.
Mwanamke huanza kuwa na irregular MP, hot flashes na kutoa jasho usiku mara kwa mara.
Mwanamke huwaza kujisikia leo ana juicy vagina na kesho ana total dried vagina pia anaweza kujikuta ana enjoy sex na mume wake dakika 5 na dakika 5 zinazofuata anajisikia kuumia (hurt).
Mume huanza kuchanganyikiwa kwa vile mke anabadilika kuhusu mambo ya kitandani hata hivyo jambo la msingi ni kuwa na communications za uhakika kuhusiana na mabadiliko yale mwili unapitia.

Kipindi hiki mwanamke pia huzalisha kiwango kidogo sana na hormone ya oxytocin na hii ina maana kwamba hutahitaji sana bonding na matokeo yake unakuwa na maisha yako na you don’t care.

Miaka 50 na zaidi
Mwanamke akiona ameshapitisha mwaka bila MP maana yake tayari yupo kwenye menopause.
Huu ni umri ambao unakuwa huna energy, hamu ya kufanya mapenzi hushuka.
Jambo la msingi ni kwa mwanamke kujua namna ya kupambana na mabadiliko ya mwili hasa suala la sex kwani mwili hauna hormones za kutosha kukupa libido na mazingira mazuri ya tendo la ndoa.


Kukumbusha mambo ya msingi kuhusiana na Hormones ni vizuri mwanamke kuwa na ufahamu (MP literate) kuhusu mwili wake hasa kuhusiana na suala la mzunguko wa mwezi.

Je, unafahamu mzunguko wako ni wa siku ngapi? 28 au tofauti?
Je, unaweza kufahamu (pinpoint) tarehe ambayo ulimaliza MP iliyopita?
Je, unaweza kutambua aina ya ute (discharge) inayotoka kwenye uke ili kujua upo wapi katika mzunguko wako wa mwezi?
Je, unafahamu ni siku ngapi na ipi kabla ya kuanza MP matiti yako huwa tender?
Je, unafahamu ni siku zipi huwa unajisikia vizuri mume wako akuguse softer au harder wakati wa faragha?

Kama unayajua haya umebarikiwa!

No comments: