"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, February 20, 2010

Unaweza Kudumu!

Swali:

Je, ni kweli mapenzi ya kweli (true love) huweza kudumu maisha yote kati ya mke na mume?

Jibu:

Ni kweli kabisa huweza kudumu muda wote au maisha yote ya mke na mume.

Hata hivyo huhitaji kazi, juhudi, jitihada na kujitoa.

Timu ya wanasayansi hivi karibuni walifanya utafiti wao na kugundua kwamba watu wawili mwanaume na mwanamke wanapopendana (fall in love) huhusisha mabadiliko ya kikemia kwenye ubongo ambayo hudumu kwa miezi 12 hadi 18 tu na baada ya hapo wanaanza kwenda wenyewe.

Mahusiano huhitaji matengenezo mapya (maintenance/repair).

Hivi karibuni nilikutana na mwanamke mwenye miaka 60 na alikuwa anaumwa Hospitalini na pembeni alikuwepo mume wake wa miaka 75 akimuuguza huku wameshikana mikono na wanatiana moyo kwa furaha.

Ile kuongea nao wakasema “tangu tulipokuwa high school tulikubaliana kuwa tutakuwa marafiki na kuishi pamoja ni ahadi yetu na tunafurahia hilo”.

Unaona hiyo ni love story.

No comments: