"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, March 31, 2010

Kufahamiana!

Kuna umuhimu wa kuonana uso kwa uso kwanza hata kama yupo North pole....

Kile UNAKIFAHAMU (know) kuhusu partner wako huelezea kiasi gani unaweza KUMUAMINI (trust) katika KUMTEGEMEA (rely) akutimizie mahitaji yako ili uweze KUJITOA (committed) kwake na hata wewe kuwa tayari KIMWILI (sexual)

Hii ina maana kujiingiza kwenye mapenzi kabla hujamjua vizuri, hujamuamini vizuri, au hujajitoa kwake vizuri ni dhambi na hatari kubwa katika mahusiano hasa ya uchumba.

Pia kujitoa kwake bila kumfahamu vizuri, au hujamuamini vizuri na kuweza kumtegemea ni hatari.

Kabla ya kuoana wawili wanatakiwa kufahamiana au kujuana, kuaminiana, kutegemeana na kila mmoja kujitoa kwa mwenzake na wakiingia kwenye ndoa ndipo wanaweza kuendelea na masuala ya mwili yaani mapenzi.

Ili kumfahamu mtu na kuwa karibu naye (intimacy) lazima kuwa na mambo makubwa matatu;

Kuongea ili kufahamiana,

Kuwa pamoja,

Na Muda.

Kama unapenda Hesabu kwa kifupi:

F= K + U + M

Ambapo

F= Kufahamiana, K = Kuwa pamoja, U = Upamoja (uso kwa uso) na M = Muda

Hayo mambo matatu ni nyuzi ambazo hushona vizuri vazi liitwalo KUFAHAMIANA.

Hii ina maana kuongea peke yake bila kuonana ana kwa ana ni hatari kwani unahitaji kumuona mwenzako uso kwa uso in action.

Hii ni kudhihirisha kwamba kumpata mke au mume kwa kutumia internet ni RISK kubwa mno.

Kutafuta mchumba kwa njia ya Internet is just talking without togetherness.

=================

Jane alikutana na James online na kwa kuwa wote walikuwa na uhitaji wa mwenzi wa maisha wakaanza kuwasiliana kwa email na instant messaging na hatimaye simu.

Jane alijisikia raha sana kuwasiliana na James kwa njia ya email na instant message (chat) kwa kuwa kwake ilikuwa rahisi sana kuandika mawazo yake bila kuogopa kwamba unayeongea naye anakuangalia (hakuna mambo ya self esteem au nimevaaje nk)

Baada ya miezi 3 penzi likakua na kukolea kwelikweli.

Wakaamua kupanga wakutane kwa mara ya kwanza na wakapanga weekend moja wote waende Bagamoyo kwenye hotel zilizopo kando kando ya Bahari ya Hindi, ila kila mmoja chumba chake.

Weekend ilipofika wakaenda na katika maongezi yao wakajikuta wanatumia muda wote chumbani kwa Jane mchana wote na usiku mzima.

Kisia nini kilitokea.....................

Jane alirudi nyumbani mwenye furaha kwani ameonana na soul mate ambaye alikuwa anatimiza ndoto zake.

Akiwa na furaha kubwa akaamua kumpigia simu James, hakuna majibu, akienda kumwaga email ndefu na yenye sifa na kukumbushia raha aliyopata na namna James anatimiza ndoto yake, hakujibiwa vilevile.

Haijulikani James kwa nini alimsusa dada wa watu baada ya kukutana na kulala naye (sex)

Jane hakuamini ila ni kweli alikuwa amepoteza muda wake, alidanganywa, alisalitiwa na mwanaume aliyemuamini, akajitoa hata kumpa mwili wake.

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@

Jane alikosa kitu kimoja katika mahusiano yake na James (kabla ya falling in love), waliongea kwa email na simu, wakawa na muda miezi 3 lakini walikosa kuwa pamoja ili kufahamiana.

Kosa kubwa la Jane alimpenda James kabla hajamfahamu kwa kuwa naye pamoja (togetherness) ili kumjua James uso kwa uso kabla hata ya kwenda Bagamoyo.

Walihitaji kuongea pamoja, kuwa pamoja na muda wa kutosha ili kufahamiana tofauti walizo nazo, vitu ambavyo wanafanana, historia zao na hata life style zao.

Never trust your feelings

Tuesday, March 30, 2010

Imekuwaje?

Kila mwili wa mwanamke ambaye hajafikia hatua ya menopause anao mzunguko wa wastani wa siku 28 (ovulation).

Hii ina maana katika siku 14 katika 28 anakuwa na chemical balance nzuri, hizo ni siku za kunywa na kuburudika na vicheko.

Na siku 14 zingine huwa na chemical imbalance ambazo ni siku za radi na ngurumo, be extra careful hasa kama ni mara yako ya kwanza kuishin na mwanamke.

Kuna Baadhi ya wanawake ni afadhari ukutane na terrorist kama ni nyumbani hapakaliki, kama ni ofisini unaweza kuacha kazi!

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@

Siku moja James anarudi nyumbani kutoka kazini; ile anafika mlangoni anakutana na tabasamu la kuvuti kutoka kwa mke wake Jane ambaye alikuwa anamsubiri mlangoni, Jane amevaa amependeza, ananukia vizuri na kumfanya James kuhisi bomu lililomo kwenye mwili wake linataka kulipuka ghafla, wanakaribiana na kupeana mabusu ya nguvu na wanabebana juu kwa juu hadi chumbani kwa raha zao, sikwambii nini kiliendelea!

Siku ya pili yake James anaamua kutoroka kazini dakika 30 kabla ya muda ili kumuwahi mke wake Jane nyumbani kwani huduma aliyopewa jana yake logically imemfanya aamini na leo raha ya kula na kunywa katika mke wa ujana wake.

Anafanikiwa kupiga chenga msongamano wa magari mjini na hatimaye anawahi zaidi ya muda wa kawaida kufika nyumbani huku akijisemea moyoni “leo ni leo naamini itakuwa mara mbili ya jana”.

Ile anafika nyumbani, mlangoni mke hayupo, anamtafuta kila chumba utadhani ni detective agent wa FBI bila mafanikio, anajaribu kuita kwa sauti hakuna majibu.

Anaenda upya kumtafuta mke wake kitchen, bedroom, store, bafuni, living room, chini ya sofa na kitandani; hakuna.

Ile kupita kwenye uchochoro katika moja ya vyumba anamkuta mke wake Jane amejikunyata, machozi yanamtiririka kwenye mashavu kama mvua za masika za Iringa na mbeya, macho yamemtoka utadhani ameambiwa ammeze chura kwa lazima.

James kwa upendo anamsogelea mke wake ili kumfariji kwa kumkumbatia,

Ghafla Jane anamzuia na kumbwatukia kwa sauti;

Don’t touch me, leave me alone! Unachotaka kwangu kila siku ni mwili wangu tu, kila siku unawaza na kutaka sex, sex, sex, sex......................”

Maskini James ni mwezi wa pili tu tangu amemuoa binti mrembo Jane na anajiuliza ni kitu gani kimetokea?

au kitu gani nimefanya?

HAPATI MAJIBU!

Hujajua kwa mwanamke kuna siku za radi na chemical imbalance

Kuna siku mwanamke anakuwa mbongo, anakuwa na mood na hatabiriki no matter what!

Mwanamke anabadilika na unatakiwa kukaa mbali!

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@

Baadhi ya wanawake huwa affected na tatizo la hormones - chemical imbalances (estrogens & progesterone) ni sababu kubwa ya kibaolojia ambayo huweza kuathiri uhusiano wa mwanamke na mume wake au wale wanaomzunguka na hii hutokea mara nyingi anapokaribia kupata siku zake (Premenstrual Syndrome – PMS).

Mwanamke anakuwa depressed.

Anajisikia kuchoka hata baada ya kulala masaa ya ziada, kukosa usingizi anaweza kuamka saa kumi usiku na asipate tena usingizi.

Kukosa hamu ya kula na kupenda kula vitu vitamu vitamu tu.

Kukosa hamu ya tendo la ndoa na pia kukosa hamu ya kufanya kitu chochote ambacho huwa anapenda kufanya.

msongo wa mawazo, mood kupenda na kushuka, kilio cha machozi bila sababu, kuvunja vitu, hasira.

Atapenda kuwa antisocial, anaweza asijibu simu, na kutopenda kujumuika na wengine.

Kukosa kujiamini (self esteem/confidence).

Maumivu ya tumbo, kichwa na kubadilika joto mwilini.

Anakuwa negative kwa kila kitu na mtu akiongea anajisikia usumbufu na mwingine asipoongea anajisikia hasira na kwamba yupo ignored.

Anaongea kidogo, ana smile kwa binde ana anaweza kukaa Mahali kwa masaa bila kuwaona wengine.

Anapenda kukaa kwenye giza au chumba chenye giza lonely.

Monday, March 29, 2010

Je, Niachane naye?

SWALI

Habari ya kazi kwanza nashukuru kwa kutuelimisha kupitia blog yako.

Mimi naitwa Ishita nimeolewa,

Siku chache baada ya ndoa yetu baada ya kutoka honeymoon niligundua kuwa mume wangu ana mtoto nilisoma kwenye simu yake na ndio kwanza mtoto alikuwa na wiki moja.

Kabla ya sisi kuoana tulikuwa tunaishi pamoja kwa zaidi ya mwaka mmoja. Nilipomuuliza mara ya kwanza alikataa,

Lakini baadae alikuja kukubali na akaniomba msamaha, kwa vile nampenda sana mume wangu na yule mtoto hana hatia nilimsamehe na nikamwambia mtoto akiwa mkubwa akamchukue ili tuishi nae akakubali.

Lakini cha kushangaza na kinachoniuma mimi ni kwamba kila akitaka kumpeleka mtoto kliniki yule dada aliyezaa nae anataka aende na mume wangu kliniki na huwa namruhusu mume wangu ampeleke mtoto wake cliniki lakini roho yangu huwa inaniuma sana na isitoshe nahisi bado wanaendelea na uhusiano wa kimapenzi naomba ushauri nifanyeje na hapa nilipo ni mjamzito.

Je, niombe talaka niachane nae?

Au niendelee kuvumilia maumivu?

MAJIBU:

Dada Ishita,

Pole sana kwa shida, tatizo na machungu unayopitia.

Ni kweli Inaumiza sana, kitendo cha kuingia kwenye ndoa mpya na kukutana na shughuli nzito kama hii, kweli inaumiza sana na inaaibisha mbele za wanaokuzunguka.

Upo sahihi kabisa kujisikia vile unajisikia, kwani jambo hili huumiza, hutisha, hukatakata moyo na kukufanya ujione kama hufai kwa wazazi, ndugu, marafiki na watu wote wanaowazunguka.

Ni kitendo kinachoumiza sana kwani mwanaume uliyemwamini na kuchukua risk ya kuishi pamoja mwaka mzima bila ndoa na baada ya kukuingiza kwenye ndoa unajikuta kumbe hukuwa mwenyewe bali kuna mwingine ambaye tayari amesha mpa first born; inatisha na inaumiza sana.

Dada Ishita, kumbuka mume wako kuwa kuzaa na mwanamke mwingine ni matokeo ya ubovu wa mahusiano yenu tangu siku zile mmekubaliana kuishi pamoja bila ndoa.

Kuvutana na kuishi pamoja maana yake hakuna commitment, hakuna agano, hakuna kifungo ni kuishi kwa kubahatisha na matokeo yake mtu anakuwa huru kufanya kile anataka kwa kuwa anajua hakuna commitment.

Sasa maji yamemwagika na kilichopo ni kutafuta njia na namna ya kupata maji upya.

Kumbuka vile unajisikia hutajisikia milele ingawa ni kweli trust uliyonayo kwake huiwezi kuwa kama siku ya kwanza ulipokubaliana naye kuishi pamoja na mwenye kukuthibitishia kwamba amebadilika ni yeye mwenyewe.

Kuachana ni kama kuruka majivu na kukanyaga moto, ni kutafuta matatizo mapya magumu zaidi hasa kama hujui mzizi wa hili tatizo.

Hapo kwanza una mimba na una safari ndefu na ndoa bado mpya kabisa achana na wazo la talaka kwanza hadi utatue tatizo lililopo kwa kushirikiana na mume wako.

Na inawezekana ukiachana naye unaweza kwenda kuolewa na mwanaume mwenye sifa kama hizo tena na hali ikawa mbaya zaidi kwako.

Angekuwa mume wako alikuwa na uhusiano na huyo mwanamke na hakuna mtoto, issue ingekuwa asiwasiliane na huyo mwanamke milele, ila suala la mwanaume kuwa na mtoto na mwanamke nje ya ndoa ni suala gumu sana si katika ndoa yako tu bali ndoa zote ambazo hukutana na tatizo hili chini ya uso wa dunia.

Kwanza hawezi kukwepa responsibilities za kuwa baba kwa huyo mtoto na si haki kabisa mtoto kukosa haki zake kwa baba yake halisi.

Kuna wanawake wengi sana duniani na Tanzania wamejaa sana ambao wanahangaika na watoto kwa kuwa wanaume waliowazalisha na baadae wamewatelekeza watoto wasio na hatia, huyo mtoto hakuomba kuletwa duniani imetokea tu na hana kosa, pia anastahili kuwa na baba ambaye anahusika katika maisha yake mia kwa mia.

Hii ina maana kwamba ukitaka (pia unastahili) kuendelea kuishi na mume wako inabidi ukubali kwamba hili tatizo ni lenu wote na si yeye peke yake na huyo mwanamke na huyo mtoto hivyo shirikiana naye bega kwa bega tena kwa upendo (hata kama unaumia kiasi gani) ili kupata majibu sahihi ya kwanza namna ya kumtunza au kumlea huyo mtoto na pili ili wewe mwenyewe upone maumivu.


Bila kushirikiana wewe na mume wako itakuwa ngumu sana kwa mume wako kuwa na upendo wa kweli kwa mtoto wake na pia kwako.

Pia bila mume wako kuongea na wewe kwa uwazi, kwa akili na busara ili wewe ujue chanzo cha affair yake hadi kupelekea kupata mtoto (pia achunguzwe vizuri isije akawa ana mtoto mwingine sehemu zingine tena) na pia ashirikiane na wewe kutoa misimamo na namna atakavyolea mtoto na namna atashirikiana na huyo mwanamke na wewe kuhakikisha mtoto anapata haki zake na ndoa yako na yeye inaendelea.

Pia huyo mwanamke unatakiwa umfahamu na anatakiwa kutambua kwamba ninyi ni mume na mke na atambue mipaka yake na ashirikiane na ninyi namna ya kumlea huyo mtoto kiumbe kisicho na hatia.

Pia mume wako anatakiwa asimame mbele ya mshauri wa ndoa, au wazazi au watu wenye ndoa imara ambao wanaweza kuwasaidia kuwashauri.

Kutokana na tatizo lililopo; mume wako amekusababishia kidonda kikubwa sana moyoni, hivyo jiandae kukabiliana na hasira, ukali, kukosa hamu ya tendo la ndoa, kuwa na msongo wa mawazo, na inaweza kuchukua muda mrefu zaidi ya unavyotegemea kurudi kwenye hali yako ya kawaida.

Kama una maswali zaidi naomba tuwasiliane kupitia email ifuatayo:

lazarusmbilinyi@gmail.com

Sunday, March 28, 2010

Uwe Jasiri!

Usione vinaelea; vimeundwa kwa ujasiri!

Wakati mwingine unabidi uwe jasiri kuachana na mahusiano ovyo (uchumba) ambayo unaona kuna deep seated issues ambazo haziwezi kupata muafaka kabla ya kuoana na kuwa mke na mume.

Kama mwanaume ni kiruka njia (muasherati) na huoni dalili za kubadilika ingawa anakuahidi amebadilika na unaona bado ana pepesa macho, ukweli ni kwamba kipande cha karatasi (mkataba wa ndoa) hakitaweza kubadilisha tabia yake.

Kama mwanamke ni manipulator mzuri na mwongo mwenye usumbufu kila siku kwa style mpya hadi mwanaume unatoa jasho kama si kuingia matatizoni au madeni ili kumtimizia mahitaji yake, ukweli ni kwamba atakuwa mzuri sana kuendelea na manipulation hata akiwa mke.

Do you want to feel this way for the rest of your life?

Jibu ni NO,

Kama ni No sasa unasubiri ni kwenye mahusiano ya aina hiyo ambayo ukijidanganya kwamba eti mkioana atabadilika itakufikisha uwe na maumivu maisha yako yote ya ndoa.

Nini kinamzuia asibadilike kabla hamjaoana na nini kinakufanya uamini atabadilika akikuoa?

Uwe jasiri na kuwa na msimamo na kuwa na maamuzi, afadhari upate maumivu ya mwezi mmoja au miezi miwili kuliko kuwa na maumivu ya maisha yote ya ndoa kwa kufanya uchaguzi ovyo wa mtu wa kuingia naye kwenye ndoa.

KUMBUKA

Huwezi huwa na health relationship kama utaendelea kushikamana na mtu ambaye ni ovyo (anakupa homa kila siku) sababu ya msingi ni kwamba watu wazuri na wenye afya nzuri kimahusiano huwa hawaandamani na wale wenye mahusiano yasiyo na afya hivyo kuachana na mchumba mwenye sifa mbaya ndiyo jibu la kumpata mwenye sifa nzuri na huwezi kushika yote kwa wakati mmoja.

“Your only hope for a rewarding, satisfying, inspiring relationship is to get out of a frustrating, defeating, discouraging and manipulating one:”

Pia watu wazuri huwa na risk kubwa sana kuangukia kwa mtu ovyo (rude) kwa sababu mtu mzuri ni mwepesi kusamahe, ni mtoaji, huyaangalia matatizo na kuona ni kitu kidogo, huweza kusamahe na kutoa nafasi kwa mkosaji zaidi ya mara mbili, tatu, nne nk.

Watu wenye moyo safi huamini kwamba watu hubadilika kirahisi.

Linapokuja suala la ndoa lazima uwe makini maana unaweza kuendelea kuumizwa maisha yako yote ya ndoa.


Saturday, March 27, 2010

Mr. & Mrs P. Sanga

God, the best maker of all marriages,
Combine your hearts into one.

By

Lazarus & Gloria Mbilinyi

Friday, March 26, 2010

Vive la différence!


Kuna sentensi moja ambayo wanandoa wengi hupenda kuitumia ambayo ina makosa makubwa kupindukia nayo husema;
“Kama mume/mke wangu angebadilika na kuwa kama ninavyotaka mimi basi ndoa yetu ingekuwa nzuri sana na ya kuridhisha”
Ukweli ni kwamba kitu kama hicho hakipo na haiwezekani na ikiwezekana itakuwa kituko.
WHY?
Kwa sababu wewe ni mwanamke na mume wako kuwa kama wewe unavyotaka maana yake unataka awe mwanamke, afanye mambo kama mwanamke hapo nyumbani. Swali kwa nini uliolewa na mwanaume?
Kama wewe ni mwanaume ukitaka mke wako awe kama wewe unavyotaka, maana yake unataka awe mwanaume na afanye mambo kama mwanaume kitu ambacho kitafanya nyumba yako iwe na wanaume wawili, guess what? Vita ya tatu ya dunia itatokea.
Mungu alituumba mwanaume na mwanamke kuwa tofauti na hizi tofauti ndizo zinatufanya tuwe mwanaume na mwanamke hivyo badala ya kulazimisha kila kitu kiwe kama wewe unavyotaka badala yake zikubali na kuzisherehekea, vive la différence!
Kuna tofauti ambazo zipo kati ya mke na mume na haziwezi kubadilika na haitawezekana na kujaribu kumbadilisha mke wako au mume wako ni kupoteza muda wako bure.
Punguza matarajio ya mfurahie na kumpenda kama alivyo!
Mwaka 1981, Dr Roger Sperry alipokea Tuzo (Prize) katika masuala ya Medicine/Physiology kutokana na ugunduzi wa namna ubongo unavyofanya kazi kwa watoto tumboni.
Daktari aligundua kwamba katika mimba ya watoto wa kiume kuna kuwa na chemical reaction katika umri wa wiki ya 16 hadi 26 tofauti na watoto wa kike.
Hiki kitendo hudhoofisha utendaji wa ubongo wa mtoto wa kiume sehemu ya kulia ambayo huhusika na utunzaji, uleaji, uuguzi au uuguzaji (caring) na matokeo yake upande wa kushoto kunakohusika na mantiki (logic) hutumika zaidi ya mtoto wa kiume hadi akiwa mtu mzima.
JE, HII INA MAANA GANI?
Hii ina maana ubongo wa mwanaume na mwanamke ni tofauti kwa maana kwamba mwanamke hutumia sehemu ya kulia ya ubongo unayohusika na uleaji, uuguzi, kumbukumbu nk wakati mwanaume hutumia ubongo sehemu ya kushoto ambayo huhusika na mantiki (logic).
Hii ina maana pia mwanaume huzaliwa na udhaifu wa ubongo upande wa kulia
JE, HII INA MAANA GANI KATIKA NDOA
Suala la mwanamke kutumia right brain na mwanaume kutumia left brain huathiri kila eneo la ndoa na husababisha tofauti kubwa mno kati ya mke na mume.
Bila kufahamu hizo tofauti na kuzikubali ndoa inaweza kujikuta inaishi kwenye vita kuu ya tatu ya dunia.
Mr, inawezekana Mrs. akikwambia hupo sensitive au rejecting inawezekana tatizo ni ubongo wako namna upo wired ndiyo maana wakati mwingine hakuna kuelewana ndani ya ndoa.
MIFANO
Mke anaweza kuongea na simu kwa dakika 20 na bado anaweza kuanza kumsimulia mume details zote za ile simu kile alikuwa anaongea hata kama mume hahitaji kujua.
Pia mwanaume anaweza kuongea na simu kwa dakika 20 na mke akiuliza nini alikuwa anaongea, mume atajibu neno moja tu na imetoka!
Mke akienda kwenye sherehe na anaporudi atamsimulia mume kila kitu kimetoke na kila mtu aliyekuwepo kwa mume wake hata bila kuulizwa, na mwanaume akienda kwenye sherehe anaporudi mke akimuuliza sherehe Ilikuwaje atamjibu neno moja tu ‘ilikuwa safi” imetoka hiyo na mke anabaki kushangaza tu.
Kama huamini kwamba mwanamke ana memory tofauti na mwanaume basi muulize mume mke wako honeymoon ilikuwa wapi na mlifanya kitu gani na kama kuna watu anawakumbuka aliowaona kwenye honeymoon, hata kama ni miaka 5 iliyopita bado anakumbuka hata nguo mlizovaa rangi zake nk.
Mwanamke anatakiwa kufahamu kwamba, mwanaume kusahau au kutokuwa sensitive katika issue mbalimbali zinazowahusu (kama vile kusahau kukwambia kuhusu msiba unaowahusu) si kuonesha hajali bali wakati mwingine ni ubongo wake unafanya kazi tofauti na mwanamke.
(this has a scientific facts)
Si mwanaume kuwa logic au mwanamke kuwa emotional ndiko hujengwa ndoa bali ni kuishi kwa kutii neno la Mungu ambalo linasema mke na mume kuishi kwa hekima ya kimungu.

Thursday, March 25, 2010

Hapo zamani za kale!


Mipango ya kuchagua mwenzi wa maisha (mke au mume) hapo mwanzo ilihusisha familia, jamii, tamaduni na asilimia 80 ya tamaduni zote duniani zilifuata huo mfumo ambao ulijulikana sana kama arranged au forced marriages.
Njia hii iliwezesha kujenga uwiano na uhusiano wa kuwaleta pamoja wawili wanaotaka kuoana kwa kufuata;
Utamaduni unaofanana, dini inayofanana, sehemu wanayotoka inayofanana, kufanana kwa uwezo kijamii, kufanana kwa jadi na faida ambazo familia mbili zitapata kutokana kwa uhusiano wa hao wawili.
Kwa ufupi walitumia kichwa kufikiria nani aoane na nani badala ya moyo.
Katika jamii nyingi za kiafrika huu utamaduni umedumu hadi miaka ya hivi karibuni ingawa Baadhi ya nchi za Asia bado arranged/forced marriage zipo hata leo na wanajivunia aina hii ya ndoa na katika huu utaratibu jamii au wazazi wanakuwa na sauti kuliko waoanaji.
Mwaka 1926 mwanasosholojia Ernest W. Burges alipingana sana na utaratibu mpya ambao watu ambao tumezaliwa karne ya 21 tunautumia ambao kumpata mke au mume jambo la msingi ni kuangalia mapenzi, mahaba, kuvutia na ukaribu wa kimapenzi, sex, chemistry, kutimiziwa mahitaji na kufanana au kwa ufupi kutumia moyo (feelings) badala ya kichwa (akili).
Huyu mtaalamu alisisitiza kwamba ni vizuri kutumia kichwa kwanza na baadae moyo ili kumpata mtu wa kuishi naye kwani upendo wa kweli hujengwa katika muda ambao wawili wanaishi na si mapenzi peke yake kwani ni vigumu sana kutambua upo kwenye mapenzi au la (love Vs infatuation).
Jambo la msingi unatakiwa kutambua kwamba hapa kuna mambo matatu yaani wewe (nafsi), moyo na akili (kichwa) na utaratibu ni kwamba wewe (ambaye ni nafsi) unatakiwa kuongeza akili na moyo na tatizo kubwa la kutumia moyo (feelings) huweza kukuhadaa hadi feelings zinaanza kukuongoza wewe na matokeo yake ni akili kushindwa kutambua information sahihi za kupata mtu wa kuoana naye
Love is blind kwa maana kwamba ukitanguliza love akili hutiwa giza na kushindwa kufanya maamuzi sahihi kuhusu mwenzi wako.
Sasa kuchagua mke au mume katika Karne ya 21 ni romantic attraction na feelings ingawa data zinaonesha kwamba pamoja na kutumia moyo bado watu wanaachana kuliko wakati wowote katika historia ya dunia.
Sasa ukitafutiwa mke na jamii au familia unaonekana mshamba wa kutupwa na huna maana au ni mwanaume weak au mwanamke uliyeshindikana.
Pia information society tuliyonayo sasa inashangalia na kukumbatia (embrace) romantic love kupitia muziki, movies, TV, magazeti, vitabu, mahubiri nk.
Tatizo kubwa la approach ya kutumia moyo (feelings na love kwanza) ni kwamba mtu aki- fall in love (moyo) hawezi kutumia vizuri akili zake (kichwa) kwani moyo hutia giza akili na wahusika hushindwa kupata information halisi zinawawezesha kumpa mke au mume anayefaa ambaye anaweza kumpenda na kudumu hadi kutengeneza upendo wa kweli (true love) ambao unatakiwa katika ndoa.
Hii haina maana kwamba turudi enzi za mababu zetu bali tunaweza kutumia njia sahihi ambazo akili na moyo huweza kufanya kazi pamoja na kukupa chaguo sahihi wewe (nafsi)
Tutaendelea........................................

Wednesday, March 24, 2010

NI Sababu Potofu!

Watu huoana kwa sababu au malengo tofauti tofauti. Kama unaoa au kuolewa kwa sababu ambazo si sahihi maana yake unafanya uamuzi au uchaguzi usio sahihi ambao mwisho wa siku utajikuta umetengeneza jehanamu hai duniani.
Hebu leo tujikumbushe sababu ambazo si sahihi kukimbilia kuoa au kuolewa
KUWARIDHISHA NA KUWAFURAHISHA WENGINE:
Usioe au kuolewa ili kuwaridhisha wazazi wako au ndugu zako au rafiki zako.
Unapoona au kuolewa ndoa ni mali yako na si mtu mwingine.
Kama huvutiwa na huyo mtu hulazimishwi kuishi naye maisha yako yote eti kwa kuwa wengine wanamuona mtu maridadi na wazazi wako na rafiki zako watakuona na wewe umeolewa au kuoa.
Ndoa ni mahusiano ya karibu sana kiasi kwamba huwezi kuoa au kuolewa ili kumridhisha mtu mwingine isipokuwa kuwe na upendo wa kweli (compassionate love)
Usijiuze kwa bei rahisi!
ANAFANANA NA BABA AU MAMA YAKO:
Kama kuna vitu baba yako alikufanyia wakati upo mtoto na haviwezi kufanya kwa mtoto yeyote duniani (ubaya) au mama yako alikuwa katili kumzidi Hitler basi inabidi uwe makini na kuvutiwa na mtu wa personality ya huyo mzazi wako kwani watu ambao wana unfinished business na wazazi wao hujikuta wanaoana na mtu ambaye anafanana kutoa mateso kama ya wazazi wake.
Hata hivyo kama mama yako alikuwa na moyo kama wa mama Theresa na baba yako alikuwa mtu mstaarabu na huyo mtu wako anakukumbusha wazazi wako, basi huyo mshike vizuri.
HAFANANI NA BABA AU MAMA YAKO:
Kwa mfano kama binti umechoshwa na tabia za controlling za mama yako au baba yako na unaenda kumtafuta kijana wa kiume ambaye ni weak ili na wewe umkalie.
Usijidanganye eti unataka kuona au kuolewa na mtu mwenye tabia tofauti (opposite) na wazazi wako ukweli ni kwamba mwisho wa siku unaweza kujikuta huyo mtu wako anasumbua the same way na wazazi wako ila opposite direction.
KUJARIBU KUMUOKOA MTU:
Unampenda na kujifanya ume-fall in love na mtu ambaye yupo kwenye matatizo au shida au anapitia katika majaribu na unachukua advantage kutokana na matatizo yake.
Kumbuka watu wenye matatizo na shida wanahitaji rafiki siyo mpenzi na kuoana nao maana yake mwisho wa siku mtajikuta ni wakavu na hakuna upendo wa kweli.
KUONESHA NA WEWE UMO:
Kama muda umeenda sana na unajisikia kuchoka kuwa single na unaamua kumbeba bora mwanaume ili kuonesha na wewe wamo; inawezekuwa disaster.
Hata kama miaka inapita bila hata kuongeleshwa na mwanaume yeyote bado suala la kumbeba mwanaume yeyote atakayepita kwako ni hatari kwake na kwako.
Hata kama imefika Mahali unajiona hajiamini bado kuolewa au kuoa si dawa ya kukufanya uwe unajiamini bali ni kuruka majivu na kukanyaga moto.
Na wala usilazimishe kuolewa kwa hofu kwamba unaweza kukosa mwanaume wa kukuoa.
Ua na wewe unajiingiza kwa mwanaume akuoe kwa kuwa rafiki zako wote wameolewa.
USALAMA KIFEDHA:
Unaoa au kuolewa kwa sababu ya fedha zake.
Dunia ya leo si wanawake tu ambao hufuata mwanaume m wenye fedha bali hata wanaume sasa wanakubali kuoana na mwanamke kwa sababu ya fedha zake na si upendo wa kweli.
Ni kweli umri ni namba tu hata hivyo kwenye masuala ya ndoa wakati mwingine umri ni jambo la msingi mno kwani kijana wa miaka 23 akiona na mwanamke mwenye pesa mwenye miaka 52 inaweza kuleta shida miaka 5 ijayo.
KUTAFUTA MAKARATASI (Immigration)
KWA SABABU UNA MIMBA YAKE.
NK

Tuesday, March 23, 2010

Ana Bomu Mwilini

Kila siku mwanaume hujiona yupo Zanzibar kwa holiday!

Kwa binti ambaye unataka kuolewa!

Sex itakuja kuwa issue muhimu sana katika yenu.

Inawezekana wewe binti hujafahamu mume wako mtarajiwa anawaza mara ngapi kuhusu sex kwa saa moja tu acha siku nzima.

Kuwaza kuhusu sex kwa wanaume wengi ni suala ambalo lipo constant kwenye akili na anataka kukuoa kwa kuwa anajua utakuwa tayari kwa hitaji lake la sex.

Kama unajiona hupo tayari kwa sex angalau mara 2 au 3 kwa wiki katika maisha yako ya ndoa, basi fikiria upya uamuzi wako wa kuolewa.

Au kama hujisikii kuwa karibu naye kimapenzi au Unaona hakuvutii kimahaba na bado unataka kuolewa naye basi wewe unataka kusababisha vita ya tatu ya dunia katika ndoa yenu.

++++++++++++++++++++++++++

Katika chumba cha ushauri wanawake na wanaume ambao wameoa waliulizwa swali

Je, utajisikiaje kama kuanzia sasa haitawezekana tena kuwa na sex na mume au mke wako?

Wanawake wengi walijibu

“Haitakuwa tatizo sana kama kutakuwa hakuna sex, ila itakuwa tatizo kama kutakuwa hakuna kubusiana, kushikana au kukumbatiana na mahaba (romance)”

Kwa upande wa wanaume, hata kabla hawajajibu swali ile kuangalia sura zao namna macho yanavyowatoka na jasho linavyotiririka mwilini wakionekana kushangazwa na kutoamini kama wanaweza kuulizwa swali hilo na badala ya kujibu na wenyewe wanauliza swali

“Yaani kutopata sex tena?”

Kumwambia mwanaume kuachana na sex katika ndoa ni kama kumwambia aachane na suala la kupumua au kula chakula.

Swali la kujiuliza ni kwa nini kuna tofauti kubwa kiasi hiki kati ya mke na mume linapokuja suala la sex?

Ukweli ni kwamba aliyetuumba (Mungu) aliachofanya ni kuweka atomic bomb lijulikanalo kwa jina la testosterone katika mwili wa mwanaume.

Hili bomu humfanya kushika moto wa kimapenzi (kulipuka) kwa sekunde chache tu na kuwa tayari kwa sex.

Hata mke wake akiwa anavua nguo ili alale mwanamke bomu lake hulipuka ghafla na mitambo inakuwa tayari kufanya kile ambacho hata yeye mwenyewe haamini.

James aliulizwa swali wakati anajiandaa kuona ni namna gani atajihusisha na suala la sex na mke wake, alijibu bila woga kwamba kwa kweli kwake atapenda sana sex iwe mara tatu kwa siku kwa maana kwamba asubuhi, mchana na usiku kila siku, unaweza kuona ana matatizo ila ni kutokana na kiwango cha atomic bomb alilonalo mwilini mwake.

Firikia wewe ni mwanamke unatumiwa mail inayokwambia kwamba kutokana na matumizi yako ya simu (cell phone) ya kampuni ya Vodacom umeshinda zawadi ya kwenda holiday na mume wako visiwa vya Zanzibar kwenye Hotel ambayo ni five stars kila kitu mtalipiwa kwa wiki nzima.

Wewe na mume wako mtachukuliwa na private jet kutoka huko Arusha mnakoishi na mume wako hadi Zanzibar na mtapewa milioni 25 kwa ajili ya shopping (fedha za matumizi).

Ukifikiria namna utakavyotumia muda na mume wako mkicheza na wakati mwingine mmeshikana mikono katika beaches za bahari ya Hindi na kurudi hotelini kuwa na wakati mzuri (privacy) basi unakuwa very excited kiasi kwamba unamsubiri mume wako mlangoni kwa hamu ili akiingia tu kutoka kazini umpe hizo habari njema za kusisimua.

Ile anaingia tu unamwambia kwamba

“Nina habari njema, tumeshinda grand prize kwenda Zanzibar kwa siku tano, five star hotel kila kitu bure na zaidi tunapewa milioni 25 kwa ajili ya matumizi yetu na tutaenda kwa private jet kwenda na kurudi”.

Kwa mshangao mume wako anakujibu,

“Achana na mimi nimechoka , kichwa kinaniuma, tutaongea baadae au kesho”

Utajisikiaje?

Kama wewe ni mwanamke umeolewa basi kwa taarifa yako atomic bomb (testosterone) ndani ya mwili wako humfanya ajisikia ameshinda grand prize kila siku.

Na huwa anakuwa na hamu kubwa sana kukwambia kuhusu hiyo grand prize, unapoonesha kutopenda au kutojisikia kuwa na tendo la ndoa na yeye hukumbwa na frustrations kubwa sana, hata akienda kulala hapo pembeni kitandani kwenu huwa anakuwa amehuzunika, amejikunyata anaugulia na kuumia moyoni mwake.

Please do not underestimate his sexual needs!