"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, March 25, 2010

Hapo zamani za kale!


Mipango ya kuchagua mwenzi wa maisha (mke au mume) hapo mwanzo ilihusisha familia, jamii, tamaduni na asilimia 80 ya tamaduni zote duniani zilifuata huo mfumo ambao ulijulikana sana kama arranged au forced marriages.
Njia hii iliwezesha kujenga uwiano na uhusiano wa kuwaleta pamoja wawili wanaotaka kuoana kwa kufuata;
Utamaduni unaofanana, dini inayofanana, sehemu wanayotoka inayofanana, kufanana kwa uwezo kijamii, kufanana kwa jadi na faida ambazo familia mbili zitapata kutokana kwa uhusiano wa hao wawili.
Kwa ufupi walitumia kichwa kufikiria nani aoane na nani badala ya moyo.
Katika jamii nyingi za kiafrika huu utamaduni umedumu hadi miaka ya hivi karibuni ingawa Baadhi ya nchi za Asia bado arranged/forced marriage zipo hata leo na wanajivunia aina hii ya ndoa na katika huu utaratibu jamii au wazazi wanakuwa na sauti kuliko waoanaji.
Mwaka 1926 mwanasosholojia Ernest W. Burges alipingana sana na utaratibu mpya ambao watu ambao tumezaliwa karne ya 21 tunautumia ambao kumpata mke au mume jambo la msingi ni kuangalia mapenzi, mahaba, kuvutia na ukaribu wa kimapenzi, sex, chemistry, kutimiziwa mahitaji na kufanana au kwa ufupi kutumia moyo (feelings) badala ya kichwa (akili).
Huyu mtaalamu alisisitiza kwamba ni vizuri kutumia kichwa kwanza na baadae moyo ili kumpata mtu wa kuishi naye kwani upendo wa kweli hujengwa katika muda ambao wawili wanaishi na si mapenzi peke yake kwani ni vigumu sana kutambua upo kwenye mapenzi au la (love Vs infatuation).
Jambo la msingi unatakiwa kutambua kwamba hapa kuna mambo matatu yaani wewe (nafsi), moyo na akili (kichwa) na utaratibu ni kwamba wewe (ambaye ni nafsi) unatakiwa kuongeza akili na moyo na tatizo kubwa la kutumia moyo (feelings) huweza kukuhadaa hadi feelings zinaanza kukuongoza wewe na matokeo yake ni akili kushindwa kutambua information sahihi za kupata mtu wa kuoana naye
Love is blind kwa maana kwamba ukitanguliza love akili hutiwa giza na kushindwa kufanya maamuzi sahihi kuhusu mwenzi wako.
Sasa kuchagua mke au mume katika Karne ya 21 ni romantic attraction na feelings ingawa data zinaonesha kwamba pamoja na kutumia moyo bado watu wanaachana kuliko wakati wowote katika historia ya dunia.
Sasa ukitafutiwa mke na jamii au familia unaonekana mshamba wa kutupwa na huna maana au ni mwanaume weak au mwanamke uliyeshindikana.
Pia information society tuliyonayo sasa inashangalia na kukumbatia (embrace) romantic love kupitia muziki, movies, TV, magazeti, vitabu, mahubiri nk.
Tatizo kubwa la approach ya kutumia moyo (feelings na love kwanza) ni kwamba mtu aki- fall in love (moyo) hawezi kutumia vizuri akili zake (kichwa) kwani moyo hutia giza akili na wahusika hushindwa kupata information halisi zinawawezesha kumpa mke au mume anayefaa ambaye anaweza kumpenda na kudumu hadi kutengeneza upendo wa kweli (true love) ambao unatakiwa katika ndoa.
Hii haina maana kwamba turudi enzi za mababu zetu bali tunaweza kutumia njia sahihi ambazo akili na moyo huweza kufanya kazi pamoja na kukupa chaguo sahihi wewe (nafsi)
Tutaendelea........................................

No comments: