"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, March 18, 2010

Kichwa kwanza, Moyo Baadae!

Unapotafuta mchumba "tumia kichwa chako kwanza" na tumia moyo wako ukisharidhika naye.

Katika ndoa kuna namna tofauti ya kupambana na matatizo au kutoelewana au kubishana au kutokubaliana na jambo au shida yoyote na kila wanandoa wana namna yao, hii ina maana kwamba tatizo lilelile ambalo wengine wanavurugana na kuachana kwa wengine ni opportunity ya kujenga ndoa yao.

Inaweza kutokea kwamba mke anapenda kuwa karibu na mume wake kimapenzi (intimacy) na mume akawa anapenda kuwa mwenyewe (privacy), inaweza kuwa mke hupenda kuchelewa kulala (night owl) na mume ni mtu wa kuwahi kulala na kuamka mapema, inaweza kuwa mume anapenda kuhakikisha anapata milo 3 ya uhakika kwa siku, wakati mke anapenda milo miwili tu na imetoka. Inawezakena mke anapenda sana kuongea na mume ni mtu wa kuwa silent.

Hata hivyo bila wanandoa kuwa na aina ya kuchukuliana (flexibility/adaptivity) itakuwa ngumu sana kwa wanandoa kuridhika na ndoa yao.

Kwa kijana mgeni na masuala ya mapenzi anashauriwa kutumia kichwa na si moyo ili kuweza kumfahamu binti au kaka anayempenda awe mke wake kwa maisha ya baadae.

Kwani ukishampenda (fall in love) unaweza kupoteza mwelekeo kwa kupelekeshwa na emotions hadi kupoteza lengo la mke au mume uliyekuwa unategemea uoane naye.

Kwa wastani inachukua hadi miaka 2 tangu umemuweka kichwani (mke/au mume mtarajiwa) hadi kuoana.

Kwani bila kuchunguza kwa makini unaweza kujikuta unaingia kwenye jehanamu ndogo.

Kumbuka mwanaume ambaye anakupelekesha na kukukalia wakati wa uchumba akikuoa hiyo tabia yake itakuwa maradufu.

Kama binti hajiamini wakati wa uchumba, akiolewa ndo hatajiamini zaidi.

Utakuwa unajidanganya sana ukiamini kwamba kuoa au kuolewa kunaweza kuondoa au kutatua matatizo kama wivu, hasira, uchoyo, ukali, kukosa uaminifu, ubabe, kutojiamini nk

Ukweli ni kwamba kama Unaona tabia mbaya kwa mchumba wako basi tegemea hali mbaya zaidi baada ya kuona.

Pia, wapo watu ambao huamua kuoana baada ya kujuana au kufahamiana kwa muda mdogo sana kama vile mwezi mmoja au miezi miwili.

Kama unaamini ndoa ni hadi kifo kitakapowatenganisha, kwa nini uchukue uamuzi ambao utalazimika kuishi naye maisha yote huku unateseka kwa kuwa ulifanya mambo haraka haraka.

“The same thing that moves you to get married too quickly is the same thing that will lead you to choose the wrong person”.

Pia siri kubwa ambayo wengi hawaijui ni kwamba kati ya asilimia 80 hadi 90 ya wanaume au wanawake unaowaona si wazuri kiasi cha kutosha kuoana na wewe.

Hii ina maana kwamba ni asilimia 80 hadi 90 ya watu hao wanakupenda lakini wanatamani sana wakubadilishe kwanza ndipo wakupende na mapenzi ya kweli ni kumpenda mtu na kumchukua kama alivyo.

“You marry as is”

Kumtafuta mke au mume wa kudumu katika maisha siyo “kids play” ukienda kizembe kama mtoto utaoana na mtu mwenye akili za kitoto.

Ukweli ni kwamba unamtafuta mtu asiye wa kawaida, ambaye ana sifa maalumu unazohitaji na hakuna mchezo wa kukisi bali lazima uwe na uhakika.

Pia lazima ufahamu maeneo ambayo unaweza kumpata mwanamke mwenye sifa au mwanaume mwenye sifa.


6 comments:

Anonymous said...

Habari za siku tele kaka Mbilinyi!

Umenena vema kabisa ni vema kumchunguza mtu unaetegemea kuishi nae mpaka kifo maana nanukuu kutoka kwako "ndoa ni shimo ambalo ukishaingia umeingia" sasa iweje upate mke au mume ambae atakuwa kero kwako hasa kitabia jamani.

Ila kaka kwa wanaume wengi ukae na mchumba miaka miwili hajaku....
mh nani atakubali nyie wanaume huwa wagumu katika hili mpaka aonje halafu ajue nini cha kufanya,halafu wengi wanaume wanaangalia hicho tuu hata kama una tabia njema lakini ikulu yako hovyo ataachana na wewe tu yaani wanaume mh!
Salamu kwa baby gal jamani tuonyeshe amekua kiasi gani jamani tumuone.
Siku njema.

Mama P!

Lazarus Mbilinyi said...

Mama P,
asante sana kwa comments zako.
Ila ukweli ni ukweli mwanaume makini na anayejua kupenda hata iweje atakulinda na kuhakikisha anajiepusha na sex na wewe hata kaman ni miaka 3 hadi siku muoane vinginevyo ukimpa mwili wako unajirahisisha na kujiweka katika bei ya chini kama si bure na kuwa candidate wa kuiachwa muda wowote.
Kumbuka kuingia kwenye ndoa huku mmeshamalizana mambo ya sex ni kuwekeana mkataba wa kutoaminiana katika ndoa yenu na kwamwe hamtaaminiana kama ni wakristo wa kweli ila kama ni wakristo jina hizo ndo zenu.
Historia hujirudia siku zote na kumbuka tabia mbaya ndogo unayoiona kichuguu kabla hamjaoana, mkioana ni mlima kilimanjaro.

Upendo daima!

Anonymous said...

Habari kaka Lazarus, ni kweli hapa umeongea ndugu yangu ila tstizo ni kwamba utamjuaje mtu wa kweli? kwani wakati wa urafiki hadi uchumba kila mtu hujitahidi kuficha uhalisi wa tabia zake.

Upendo M

Anonymous said...

Yes, this is true brother.

Ila ni ngumu maana wakati wa urafiki hadi uchumba kila mtu huficha tabia yake halisi.

Lazarus Mbilinyi said...

Asante kwa maoni mazuri,

Hata hivyo si kweli kwamba mtu anaweza kuficha tabia yake halisi eti kwa sababu yupo kwenye uchumba.
Kama upo makini na ukawa makini kuhakikisha zile fall in love hazikupumbazi na ukawa na akili timamu ambazo hazijawa addicited na mapenzi ya uchumba ukweli ni kwamba tabia halisi ya mchumba wako utaijua, huwa inakuwa ngumu kwa sababu mapenzi yanakuwa yameshakufanya kuwa blind na hadi yaanze kupungua ndipo unajua tabia yake vizuri.
Ukweli unaweza ku-act vitu vingi lakini tabia ni kitu halisi ambacho huwezi kuficha hata kama utaficha ipo siku aanajisahau na kuonesha hata bila yeye mwenye kujua maana ni tabia yake.

Pia wakati wa uchumba ukiona mwenzako ana tabia fulani ambayo huipendi unaona simple na kwamba atabadilika hata hivyo ukweli ni kwamba ukiingia kwenye ndoa hali huwa mbaya zaidi kwani maisha ya ndoa ni kitu halisi si kufurahisha tu bali ni kuwajibika na makujumu ya maisha na ndipo macho huanza kuona vile yalikuwa hayaona na masikio yanaanza kusikia vile yalikuwa hayasikii.
Ndiyo maana nakazia kwamba wakati wa uchumba tumia Kichwa (akili) na moyo (love)baadae. Usiongozwe kwa feeling bali uwe logic kama huyu mtu anafaa maana ukiingia kwenye ndoa basi imetoka.

Upendo daima

Anonymous said...

Mh! nimesoma nimepata darasa la hali ya juu, hongera sana kuna baadhi ya mambo sikuyajua leo nimeyapata na kama ni kweli yanatumika kwenye dunia ya leo na yakaleta matokeo mazuri, basi mimi nina hakika nilichelewa na ndio maana ndoa yangu ndoano sometimes!
UBARIKIWE