"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, March 4, 2010

Miezi Miwili Mara Moja!

SWALI

Ndoa yetu ina miaka 4 na tunafanya tendo la ndoa mara moja kwa miezi mwili. Kila siku usiku mume wangu husema kwamba amechoka na hawezi tendo la ndoa kwa kuwa alikuwa na siku ngumu hata hivyo nafahamu aina ya kazi alikuwa nazo mchana kwa kuwa tunafanya kazi pamoja.

Kinachokishangaza ni kwamba anakusisimka sana akimuona mwanamke mtaani hasa kama anavutia.

Ninachojiuliza kwa nini mara zote anasema amechoka kwangu na je nifanyeje ili awe na hamu na avutiwe na mimi?

Mama E

JIBU

Swali lako ni la msingi sana.

Tuanze kwanza na suala la “nifanyeje ili awe na hamu au nimvutie” ingawa unapenda sana mume wako awe na hamu na wewe jambo la msingi ni wewe kukaa chini kwanza na kujichunguza vile unajiona na kujisikia wewe mwenyewe.

Wewe mwenyewe unajionaje, unajiamini vipi na unavyovutia, unavyopendeza? kwani kama wewe mwenyewe hujioni unavutia basi inakuwa ngumu sana mume wako kuona unavutia.

Mahusiano mazuri kimapenzi na mume wako hayaji tu kwa kuwa mnafanya business pamoja bali kwanza wewe mwenyewe unajisikiaje au unajiamini vipi kuhusiana na mwonekano wako.

Hatua inayofuata ni wewe na yeye kuanza kuongea pamoja kuhusiana na suala la mahusiano ya kimapenzi katika ndoa yenu.

Ni kawaida kwa wanandoa kuwa na up na downs zinazohusiana na tendo la ndoa hata hivyo kunapokuwa na ukame wa kimapenzi au ukaribu wa kimapenzi ni muhimu kwa wandnoa wenyewe kukaa chini na kuanza kujadili wapi pamepungua au kitu gani kinakosekana na si kuanza kulaumiana bali kila mmoja kuwa wazi kuelezea na kusema kile anahitaji katika mahusiano ili moto wa mapenzi urudi tena.

Je, kama mwanamke unahitaji mume kuwa karibu na wewe kwa kukubusu mara kwa mara ua kukukumbatia mara kwa mara?

Je, unahitaji kushikwa mikono au mwili wako na mume wako mara kwa mara?

Je, kuna migogoro nje ya chumbani au kutokuelewana au una hasira kutokana mambo fulani fulani kitu kinachofanya mume wako kuwa mbali na wewe kihisia?

Nk

Ukijiuliza hayo maswali na mengine na kukaa na mume wako kujadili mnaweza kufika Mahali kila mmoja akafahamu nini wajibu wake ili kurudisha moto wa mapenzi chumbani kwenu.

Mawasiliano yaliyo wazi na yanayomruhusu kila mmoja kusema kile anahitaji ndiyo njia sahihi ya kurudisha ukaribu wa kimapenzi upya katika ndoa.

Baada ya kufahamu hatua tatizo lipo wapi weka plan na kuanza kufanyia kazi na hakikisha kila mmoja anakuwa positive kwa mwenzake bila kulaumiana.

No comments: