"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, March 1, 2010

Mjomba Hana Lolote

Nina sehemu ya kuishi kwenye mwili, wakati mwingine naishi kwenye hotel inayoitwa damu; kila mmoja ananijua mimi ndiyo naitwa Kirusi mtoto wa UKIMWI, na nilizaliwa kwenye mwili wa binadamu kutokana na vitendo ZINAA.

Mama nisikilize, baba nisikilize, kaka nisikilize, dada nisikilize, wewe uliye mwerevu nisikilize, hata wewe mwehu nisikilize, uliye mtii nisikilize, mwenye kiburi pia nisikilize, msomi nisikilize, usiye na elimu nisikilize, sina urafiki na mtu yeyote.

Tunazaliana kama mchwa unaweza ukawauliza matajiri, maskini, weupe, weusi, wanawake, wanaume, madaktari na waganga wa kienyeji wote wananijua vizuri sana, hata kaka yangu STD ananifahamu nashambulia maelfu ya watu kila siku inayoenda duniani.

Sikiliza!

Na wewe nitakubeba na hasa kama unachukia kuwa mwaminifu kwa mke wako au mume wako.

Nawabeba wote wanaokataa kusubiri na kuwa waaminifu ili wakapambe makaburi.

Utakufa bado kijana!

Afrika wananijua, Ulaya wananijua, Amerika wananijua, dunia nzima wananijua kwamba mimi ni KIRUSI, mtoto wa kiume wa Mzee Ukimwi.

Kawaida natembelea baa, vilabu vya pombe, kumbi za disko na siogopi umri wa mtu, najificha kwenye maumbile ya miguu inavyovutia, makalio makubwa, mapaja yanayovutia.

Wengine huniita mimi NGOMA, UMEME, wengine wananiita JULIANA, na wengine wananiita MDUDU wengine huniita MIWAYA, na wengine TRANSFORMER, wengine wananiita mimi Nambari ONE, na wengine MANYONYOBA na majina mengine mabaya mabaya kwani jina langu ni KIRUSI mtoto wa Ukimwi wala sina urafiki na mtu yeyote wala simuogopi mtu yeyote.

Nawauwa Madaktari, Wauguzi, Wanasheria, Walimu, Maprofesa, Mawaziri, Wachungaji na wafagiaji barabara wala sina aibu.

Nitakunywa damu yako na nyama nyama zote hadi ubaki mifupa na baadaye nakupiga teke kwenda kaburini.

Nakushauri wewe mwanaume ukaze vizuri mkanda wa suruali yako na wewe mwanamke tunza nguo yako ya ndani kwa sababu ninakuangalia.

Njia kamili ya kunishinda ni wewe kuwa mwaminifu kwa mpenzi wako mmoja ambaye naye ni salama.

Ukikubali kuwa rafiki na mjomba wangu (Condom) hutakuwa na nafasi ya kunikimbia kwani kazi ya mjomba ni kwa ajili ya uzazi wa mpango, huwezi kumtumia mjomba na ukanishinda mimi.

Baada ya kusoma fahamu kwamba nipo nimekaa pembeni yako kosa moja tuu nakumaliza mzima mzima.

Nani anajua! inawezekana tayari nipo kwenye mfumo wako wa damu nenda kapime, ila kama wewe ni mwaminifu haina haja ya kuwa na hofu. Naitwa KIRUSI mtoto wa Ukimwi sina urafiki na mtu.

No comments: