"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, March 24, 2010

NI Sababu Potofu!

Watu huoana kwa sababu au malengo tofauti tofauti. Kama unaoa au kuolewa kwa sababu ambazo si sahihi maana yake unafanya uamuzi au uchaguzi usio sahihi ambao mwisho wa siku utajikuta umetengeneza jehanamu hai duniani.
Hebu leo tujikumbushe sababu ambazo si sahihi kukimbilia kuoa au kuolewa
KUWARIDHISHA NA KUWAFURAHISHA WENGINE:
Usioe au kuolewa ili kuwaridhisha wazazi wako au ndugu zako au rafiki zako.
Unapoona au kuolewa ndoa ni mali yako na si mtu mwingine.
Kama huvutiwa na huyo mtu hulazimishwi kuishi naye maisha yako yote eti kwa kuwa wengine wanamuona mtu maridadi na wazazi wako na rafiki zako watakuona na wewe umeolewa au kuoa.
Ndoa ni mahusiano ya karibu sana kiasi kwamba huwezi kuoa au kuolewa ili kumridhisha mtu mwingine isipokuwa kuwe na upendo wa kweli (compassionate love)
Usijiuze kwa bei rahisi!
ANAFANANA NA BABA AU MAMA YAKO:
Kama kuna vitu baba yako alikufanyia wakati upo mtoto na haviwezi kufanya kwa mtoto yeyote duniani (ubaya) au mama yako alikuwa katili kumzidi Hitler basi inabidi uwe makini na kuvutiwa na mtu wa personality ya huyo mzazi wako kwani watu ambao wana unfinished business na wazazi wao hujikuta wanaoana na mtu ambaye anafanana kutoa mateso kama ya wazazi wake.
Hata hivyo kama mama yako alikuwa na moyo kama wa mama Theresa na baba yako alikuwa mtu mstaarabu na huyo mtu wako anakukumbusha wazazi wako, basi huyo mshike vizuri.
HAFANANI NA BABA AU MAMA YAKO:
Kwa mfano kama binti umechoshwa na tabia za controlling za mama yako au baba yako na unaenda kumtafuta kijana wa kiume ambaye ni weak ili na wewe umkalie.
Usijidanganye eti unataka kuona au kuolewa na mtu mwenye tabia tofauti (opposite) na wazazi wako ukweli ni kwamba mwisho wa siku unaweza kujikuta huyo mtu wako anasumbua the same way na wazazi wako ila opposite direction.
KUJARIBU KUMUOKOA MTU:
Unampenda na kujifanya ume-fall in love na mtu ambaye yupo kwenye matatizo au shida au anapitia katika majaribu na unachukua advantage kutokana na matatizo yake.
Kumbuka watu wenye matatizo na shida wanahitaji rafiki siyo mpenzi na kuoana nao maana yake mwisho wa siku mtajikuta ni wakavu na hakuna upendo wa kweli.
KUONESHA NA WEWE UMO:
Kama muda umeenda sana na unajisikia kuchoka kuwa single na unaamua kumbeba bora mwanaume ili kuonesha na wewe wamo; inawezekuwa disaster.
Hata kama miaka inapita bila hata kuongeleshwa na mwanaume yeyote bado suala la kumbeba mwanaume yeyote atakayepita kwako ni hatari kwake na kwako.
Hata kama imefika Mahali unajiona hajiamini bado kuolewa au kuoa si dawa ya kukufanya uwe unajiamini bali ni kuruka majivu na kukanyaga moto.
Na wala usilazimishe kuolewa kwa hofu kwamba unaweza kukosa mwanaume wa kukuoa.
Ua na wewe unajiingiza kwa mwanaume akuoe kwa kuwa rafiki zako wote wameolewa.
USALAMA KIFEDHA:
Unaoa au kuolewa kwa sababu ya fedha zake.
Dunia ya leo si wanawake tu ambao hufuata mwanaume m wenye fedha bali hata wanaume sasa wanakubali kuoana na mwanamke kwa sababu ya fedha zake na si upendo wa kweli.
Ni kweli umri ni namba tu hata hivyo kwenye masuala ya ndoa wakati mwingine umri ni jambo la msingi mno kwani kijana wa miaka 23 akiona na mwanamke mwenye pesa mwenye miaka 52 inaweza kuleta shida miaka 5 ijayo.
KUTAFUTA MAKARATASI (Immigration)
KWA SABABU UNA MIMBA YAKE.
NK

No comments: