"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, March 20, 2010

Tunabeba zaidi ya mabegi!


Baadhi ya wanawake huamini kwamba wanaume wote ni waongo (cheaters) kwa kuwa ndicho ameona wanaume wanafanya au familia aliyokulia na kulelewa wanaume/mwanaume aliyekuwepo alikuwa hivyo.
Pia wapo wanaume wanaoamini kwamba wanawake wote ni viumbe dhaifu (weak) kwa kuwa alilelewa na mwanamke mmoja ambaye alikuwa dhaifu.
Mtazamo wa kijana yeyote kuhusu jinsia nyingine ni muhimu sana katika suala la uchumba na hatimaye kuwa mke au mume katika maisha yako.
Kama hujaoa au kuolewa ni muhimu sana kufahamu vizuri kijana wa kiume unayetaka kuoana naye au binti unataka kumuoa amelelewa katika mazingira gani (background).
“A woman can not be just jealous by accident, she is responding to her dad who was not trusted”
Hulazimishwi kumuoa fulani kwa lazima.
Kama unataka ndoa yenye furaha afadhari uwe mtu ambaye anachagua sana (picky) na wala usiwe na aibu kuachana na mwanaume au mwanamke ambaye hawaoneshi kukua kihisia kitu ambacho ni muhimu sana kwa maisha yako marefu ya ndoa hapa duniani.
Pia kumbuka mwanaume na mwanamke wanapooana na kukubaliana kwenda kuishi pamoja huwa hawabebi mabegi tu ya nguo na vyombo bali hubeba na vitu vingine vingi kutoka huko walitoka na kuvileta kwenye ndoa mpya kama vile tabia za mama yake, baba yake, kaka yake, dada yake, kabila lake, dini yake, ndugu zake, malezi yake, na kila aina ya mzigo na namna unavyochagua kwa makini ni bora kwako maana utafahamu nini anakuja nacho kuanza maisha na wewe kwenye ndoa na nyumba yenu mpya.

No comments: