"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, March 11, 2010

Ukuni wangu!

Isije kuwa ukubwa tu na ndani hakuna Risasi!

Samahani mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 42 tatizo langu ni kwamba ukuni wangu hauwezi kusimama kwa muda hata dakika 3.

Ukweli nampenda sana mke wangu na anajitahidi sana kuhakikisha ninasisimka na ukuni unasimama hata hivyo nikiingia tu hata dakika haifiki ukuni unadondoka na kuwa laini kabisa na nimechoka kutumia ukuni uliolala.

Naomba msaada kwani naogopa mke asijeanza kutoka nje kutafuta mtu wa kumtosheleza.

HMMM

Kaka HMMM,

Pole sana kwa tatizo ulilonalo na ukweli si wewe peke yako unayekumbana na tatizo la ukuni kuamua kufanya kile unataka wenyewe as if unatumia akili zake tofauti na akili zako.

Kumbuka ile hofu na wasiwasi kwamba nikiingia tu ukuni utalegea na kuwa ovyo inatosha kabisa kuupa ukuni ushindi na unakuwa defeated vibaya sana tena hands down.

Inaonekana huwa unawaza sana kwamba nikiiingia tu ukuni nao utakuwa umemaliza safari kwani “You are by what you think” unachokiwaza ndicho hutokea na jambo la msingi unatakiwa kuwaza namna gani unajisikia raha wakati upo ndani ya mke wako kuliko kufikiria ukuni wako umesimama namna gani au kwa muda gani.

Waza kwamba leo nataka kumfurahisha mke wangu kwa saa nzima, hata ukimfikisha nusu saa utakuwa umefika mbali zaidi.

Waza kwamba leo nataka apate raha kwa style zaidi ya moja, ukiishia style tatu badala ya tano bado utakuwa mbali zaidi.

Jiamini, weka malengo kwamba leo nataka kufika mbali zaidi.

Pia fanya mazoezi ya Kegel ambayo husaidia sana kukaza misuli na hivyo kukuwezesha ukuni wako kusimama kwa muda mrefu.

Mwisho nenda ukamuone daktari ambaye anaweza kukushauri aina ya tiba ambayo inaweza kukusaidia hasa baada ya kukufanyia vipimo kujua chanzo cha tatizo lako ni nini zaidi ya kisaikolojia kwani suala la ukuni kufanya yale hujautuma wakati mwingine ni hadi vipimo vya daktari.

Kumbuka:

Kutumia medication (Viagra, herbal) lazima iwe ndiyo option ya mwisho kabisa.

No comments: