"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, March 26, 2010

Vive la différence!


Kuna sentensi moja ambayo wanandoa wengi hupenda kuitumia ambayo ina makosa makubwa kupindukia nayo husema;
“Kama mume/mke wangu angebadilika na kuwa kama ninavyotaka mimi basi ndoa yetu ingekuwa nzuri sana na ya kuridhisha”
Ukweli ni kwamba kitu kama hicho hakipo na haiwezekani na ikiwezekana itakuwa kituko.
WHY?
Kwa sababu wewe ni mwanamke na mume wako kuwa kama wewe unavyotaka maana yake unataka awe mwanamke, afanye mambo kama mwanamke hapo nyumbani. Swali kwa nini uliolewa na mwanaume?
Kama wewe ni mwanaume ukitaka mke wako awe kama wewe unavyotaka, maana yake unataka awe mwanaume na afanye mambo kama mwanaume kitu ambacho kitafanya nyumba yako iwe na wanaume wawili, guess what? Vita ya tatu ya dunia itatokea.
Mungu alituumba mwanaume na mwanamke kuwa tofauti na hizi tofauti ndizo zinatufanya tuwe mwanaume na mwanamke hivyo badala ya kulazimisha kila kitu kiwe kama wewe unavyotaka badala yake zikubali na kuzisherehekea, vive la différence!
Kuna tofauti ambazo zipo kati ya mke na mume na haziwezi kubadilika na haitawezekana na kujaribu kumbadilisha mke wako au mume wako ni kupoteza muda wako bure.
Punguza matarajio ya mfurahie na kumpenda kama alivyo!
Mwaka 1981, Dr Roger Sperry alipokea Tuzo (Prize) katika masuala ya Medicine/Physiology kutokana na ugunduzi wa namna ubongo unavyofanya kazi kwa watoto tumboni.
Daktari aligundua kwamba katika mimba ya watoto wa kiume kuna kuwa na chemical reaction katika umri wa wiki ya 16 hadi 26 tofauti na watoto wa kike.
Hiki kitendo hudhoofisha utendaji wa ubongo wa mtoto wa kiume sehemu ya kulia ambayo huhusika na utunzaji, uleaji, uuguzi au uuguzaji (caring) na matokeo yake upande wa kushoto kunakohusika na mantiki (logic) hutumika zaidi ya mtoto wa kiume hadi akiwa mtu mzima.
JE, HII INA MAANA GANI?
Hii ina maana ubongo wa mwanaume na mwanamke ni tofauti kwa maana kwamba mwanamke hutumia sehemu ya kulia ya ubongo unayohusika na uleaji, uuguzi, kumbukumbu nk wakati mwanaume hutumia ubongo sehemu ya kushoto ambayo huhusika na mantiki (logic).
Hii ina maana pia mwanaume huzaliwa na udhaifu wa ubongo upande wa kulia
JE, HII INA MAANA GANI KATIKA NDOA
Suala la mwanamke kutumia right brain na mwanaume kutumia left brain huathiri kila eneo la ndoa na husababisha tofauti kubwa mno kati ya mke na mume.
Bila kufahamu hizo tofauti na kuzikubali ndoa inaweza kujikuta inaishi kwenye vita kuu ya tatu ya dunia.
Mr, inawezekana Mrs. akikwambia hupo sensitive au rejecting inawezekana tatizo ni ubongo wako namna upo wired ndiyo maana wakati mwingine hakuna kuelewana ndani ya ndoa.
MIFANO
Mke anaweza kuongea na simu kwa dakika 20 na bado anaweza kuanza kumsimulia mume details zote za ile simu kile alikuwa anaongea hata kama mume hahitaji kujua.
Pia mwanaume anaweza kuongea na simu kwa dakika 20 na mke akiuliza nini alikuwa anaongea, mume atajibu neno moja tu na imetoka!
Mke akienda kwenye sherehe na anaporudi atamsimulia mume kila kitu kimetoke na kila mtu aliyekuwepo kwa mume wake hata bila kuulizwa, na mwanaume akienda kwenye sherehe anaporudi mke akimuuliza sherehe Ilikuwaje atamjibu neno moja tu ‘ilikuwa safi” imetoka hiyo na mke anabaki kushangaza tu.
Kama huamini kwamba mwanamke ana memory tofauti na mwanaume basi muulize mume mke wako honeymoon ilikuwa wapi na mlifanya kitu gani na kama kuna watu anawakumbuka aliowaona kwenye honeymoon, hata kama ni miaka 5 iliyopita bado anakumbuka hata nguo mlizovaa rangi zake nk.
Mwanamke anatakiwa kufahamu kwamba, mwanaume kusahau au kutokuwa sensitive katika issue mbalimbali zinazowahusu (kama vile kusahau kukwambia kuhusu msiba unaowahusu) si kuonesha hajali bali wakati mwingine ni ubongo wake unafanya kazi tofauti na mwanamke.
(this has a scientific facts)
Si mwanaume kuwa logic au mwanamke kuwa emotional ndiko hujengwa ndoa bali ni kuishi kwa kutii neno la Mungu ambalo linasema mke na mume kuishi kwa hekima ya kimungu.

5 comments:

Anonymous said...

Habari ya kazi kwanza nashukuru kwa kutuelimisha kupitia blog yako. Mimi naitwa Ishita nimeolewa, siku chache baada ya ndoa yetu baada ya kutoka honeymoon niligundua kuwa mume wangu ana mtoto nilisoma kwenye simu yake na ndio kwanza mtoto alikuwa na wiki moja. Kabla ya sisi kuoana tulikuwa tunaishi pamoja kwa zaidi ya mwaka mmoja. Nilipomuuliza mara ya kwanza alikataa, lakini baadae alikuja kukubali na akaniomba msamaha, kwa vile nampenda sana mume wangu na yule mtoto hana hatia nilimsamehe na nikamwambia mtoto akiwa mkubwa akamchukue ili tuishi nae akakubali. Lakini cha kushangaza na kinachoniuma mimi ni kwamba kila akitaka kumpeleka mtoto kliniki yule dada aliyezaa nae anataka aende na mume wangu kliniki na huwa namruhusu mume wangu ampeleke mtoto wake cliniki lakini roho yangu huwa inaniuma sana na isitoshe nahisi bado wanaendelea na uhusiano wa kimapenzi naomba ushauri nifanyeje na hapa nilipo ni mjamzito? Je? niombe talaka niachane nae? Au niendelee kuvumilia maumivu

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Ishita,
Pole sana kwa yale unapitia na asante sana kwa swali zuri, upo sahihi vile unajisikia na ni kweli inaumiza sana na inachanganya sana.

Nitalijibu swali lako baada ya muda kidogo.

Mungu akutia nguvu!

Anonymous said...

Bwana asifiwe kaka nashukuru kwa moyo wa upendo uliokuwa nao.Ila nilishangaa sana kwa nini umetoa ile picha ya wawili lakini sasa umerudisha ubarikiwe na Bwana ek

Anonymous said...

Habari za kazi kaka, ni kweli unayoongea ni sahihi kabisa na kweili inabidi tuzikubali hizo tofauti na kuzifurahia. Ila kwa kweli wakati mwingine hawa wanaume wanakuwa wabishi sasa na huo ubishi nao ni tofauti?

Lazarus Mbilinyi said...

Kazi ni njema kabisa,

Kama mwanaume ni mbishi inabidi uchunguze mnabishana kuhusu nini isije kuwa ubishi unatokea kwa sababu ya tofauti zilizopo. Kutozikubali tofauti zilizopo kati ya mwanamke na mwanaume husababisha kubishana na mara nyingi mwanaume huonekana mbishi kwa kuwa yupo logic na mwanamke yupo emotional, pia kuna wanawake wabishi sana. Muhimu chunguza chanzo cha ubishi ni nini.

Pia ukiona mwanandoa mwenzako ni mbishi chunguza ni wa ngapi kuzaliwa kwao kama ni first born na wewe ni last born uwezekano wa kubishana ni mkubwa kwani personality zenu zinakuwa tofauti sana na ukichanganya na tofauti za mwanamke na mwanaume basi hapo kiwanja kitawaka moto.
Muhimu ni kuzikubali tofauti zilizopo na kuzisherehekea au kumpenda mwenzako kama alivyo pamoja na tofauti zake.