"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, March 8, 2010

Wanaangalia Mafanikio

Ni kama miongo mitatu sasa wanaharakati wamejitahidi kuwafanya wanaume wajisikie aibu kuvutiwa kimwili na mwanamke anayevutia katika mwonekano wake.

Ingawa ni kweli wanaume walizaliwa kuona (born to see).

Ni kweli huvutiwa na kushtuka pale mwanaume akikutana na mwanamke anayependeza na kuvutia.

Macho mwanaume yanauwezo wa kuona (scanning) mwanamke anayevutia katika kundi la mamia ya Wanawake utadhani macho yana lensi za kivita kwa ajili ya kurusha makombora kwa usahihi.

Au mwanamke anayevutia akipishana na mwanaume (si wote) lazima afanye juhudi ya ziada kuhakikisha mboni ya jicho inakaza kule alikuwa anaangalia vinginevyo anaweza kusababisha ajali.

Tukija suala la Wanawake; ingawa wao hukataa ukiwauliza ila ndani yao ukweli hujieleza kwamba mwanamke huvutiwa na mwanaume kutokana na mafanikio au uwezo alionao katika jamii.

Kuna usemi wa kingereza kwamba:

“Men are evaluated by income and professional status while women are evaluated by their looks”

Hii ina maana mwanamke na mwanaume wapo wired tofauti linapokuja suala la kumpata mwenzi au mtu wa kuishi naye pamoja.

Mwanaume hutafuta mwanamke ambaye anavutia, mwanaume huona uzuri wa mwanamke kuliko akili ya mwanamke kichwani mwake.

Mwanamke hutafuta mwanaume ambaye ana mafanikio, mwanamke huona akili ya mwanaume kuliko uzuri wake wa sura.

Ndiyo maana kuna utani kwamba mwanaume akiwa na pesa hata kama ana sura inayofanana na chimpanzee bado Wanawake watamuona ni handsome wa nguvu.

“A woman who supports a man for a lifetime is called crazy, while a man who supports a woman for a life time is called breadwinner”.

Swali kwa nini mwingine aitwe crazy na mwingine aitwe breadwinner?

Je, ukiwachukua mabinti wanaomaliza chuo na kuwauliza kama wapo tayari kuolewa na mwanaume ambaye atakuwa na kipato cha chini kuliko wao watakubali?

Je, ukimuuliza binti yeyote ambaye ana taaluma yake na anataka kuolewa kama atakubali kuoana na mwanaume asiyevutia ila ana kazi nzuri na kipato cha uhakika?

Si rahisi kwa mwanamke kukubali kwamba anahitaji mwanaume mwenye mafanikio au akili ya maisha ili aoane naye ingawa katika ukweli mwanaume mwenye mafanikio au akili ya maisha humfanya mwanamke kujiona yupo protected, ni mwanaume ambaye anayeonekana anaweza kuwajibika au kwa lugha nyingine si pesa alizonazo bali ule uwezo wa kupata pesa alionao ndiyo humvutia mwanamke.

Ndiyo, wapo wanawake huvutiwa na wanaume walichacha (pigika) au wengine hubeba mwanaume yeyote ili kuwakomoa wazazi wake hata hivyo mwanaume kuwa na pesa ni sexy na mwanamke anajua kuwa na mwanaume asiye na akili ya maisha au uwezo kifedha atatumia muda wake kuishi naye huku akiwa na hofu na mashaka kuhusu pesa.

Kwa wanawake wengi “money is security” najua utabisha ila ndo ukweli!

3 comments:

Anonymous said...

Du hapa naona umetumia too simplified approach kaka. Mimi nadhani kwa wanawake wengi hasa wasomi/wenye uwezo wa kujikimu (si wote) kwao kitu cha kwanza ni mwanaume anayejiheshimu/ hasa kama mwanamke naye anajiheshimu sio kicheche. Huo mtazamo ulchokua ni wa dada/ndugu zetu ambao hawana mtazamo wa kujitegemea sana au wanao ila tamaa kwa kwa kuwa walishajiwekea fikra kuwa ni wanawake. Hasa malezi tuliyolelewa yana-encourage sana kufikiri hivyo ila dunia imebadilika. Nadhani unachodefine hapa kama security kiko too simplistic kwa kuangalia uchumi unaoendeshwa na pesa, ila umeshahau ktk ucumi wa kijadi mwanaume anatafuta mwanamke ambaye anaonekana ana misuli ya kulima, tena wengine ilikuwa ukikaribia umri wa kuolewa anapewa shamba la karibu na barabara kusudi atangaze uwezo wake wa kuzalisha chakula/ food security for the family. Japo wanalima wote mwanamke tangu enzi hizo ni uti wa mgongo wa kilimo na chakula hasa sehemu nyingi. labda kama jamii za wachungaji(pastoralists) labda wanauem walichukua sehemu kubwa ya uzalishaji, ila nako huko nasikia wapo wanachunga sana tu. Ukweli ni kuwa uchumi wa kisasa umewapa nafasi wanawake kwa kushika pesa, kusimama kwenye majukwaa nk ila kwa upande mwingine umewapa double shift kwa kuwa japo wanaleta pesa nymbani, tena wakati mwingine nyingi kuliko mumewe, mila na desturi zimabaki zinawakandamiza, matokeo wanachoka zaidi mwili na akili. Na mwanaume kwa hofu ya KUTAWALIWA anaanza kuwa mbogo na abusive kwa mkewe, Wengine wanaathirika hadi mtarimbo unaweweseka kumbe yote fikra tu, hata kama mke anamoenda na kumheshimu namna gani> Kwa kweli familia nyingi zimevunjika kwa sababu ya HOFU YA MUME KUTAWALIWA na mara nyingi unakuta bado mke anamheshimu sana, maana hata huyu mwanamke naye anajua kuwa jamii itasema nanyanyasa.

kaka kuhusu u-handsome usisemee maana wewe si mwanamke, tumekaa maeneo ya kazi tumeona wanaume ma-handosme wanavyinuliwa na wanawake, sio kama wanunuliwavyo direct kama prostitutes, bali jinsi wanavyopapatkiwa na wanawake. wanapewa kila kitu na wanachukua, saa nyingine wanawaliza ila mara nyingi wanaingia mgodini pia. Ni rahisi mwanamke mzuri kumkataa mwanaume, kuliko mwanamke aking'ang'ania mwanaume mzuri, ni vigumu kuchomoa, wanasema, kajileta mwenywe ..... ooooo ndo ukimwi unavyotumaliza.

Anonymous said...

Kaka u-handsome dili tena usidangwanywe, wale wanawake ambao wamezidiwa na tamaa ya pesa, au concern ya security unakuta ana mwanaume mbaya mwenye pesa ila kwa kuwa kamongo unakuta anazichukua, ila anajifurahisha na vijana wenye seura ka-hausiboy , na ukizingatia kana nguvu pia, ndo kabisaa, kijana ananga'aa usiseme, bread winner akirudi huko na sura yake ya kunusa mavi anakuta mke yuko ndani, kijana anafungua geti kumbe keshakumywa maji yote fresh, mzee akiingia unakuta anauliza humu ndani siku hizi hamchemshi maji ya kunywa ( I mean maji ya kweli hapa) kumbe kijana kapoozea kiu baada ya kunywa yale ya moto. hii ni kwa mwanamke asiyehofu Mungu kama ambayo ilivyo kwa mwanaume asiyemhofu Mungu anavyoweza kufanya kwa mahausigeli au kwa work -mate.

tena nikupe siri, wanaume wazuri wanajua saana kuuza sura zao, kama huamni tembelea face book kwa kuanzia, na kwa kuthibitisha uliza wanawake ambao waa=nathubutu kukiri kuwa waume zai ni wazuri. sikufichi wanawake wanalalamika sana unakuta mume (mwenye kupendeza, si sura tu jamani)anamwambia mkewe "ninasumbuliwa sana na wanawake huko nje" tena unakuta huyo mwanume hana kitu kafulia na mke mke ndo anamlisha yeye na watoto ila jamaa nauza sura, na kumringia mumewe.

take home message
-mwanaume hata awe na sura nzuri au mbaya kiasi gani, akianza ku-missbehave anakuwa mbaya sana sana wala sura haina thamni tena
-vivyo hivyo mwanume akiwa na pesa lakini akaanza kuwa na tabia mbaya na unyanyasaji wa hali ya juu, si pesa yake wala nini kinachikuwa na thamani. mke anaweza asimwache kwa kufofia kuonekana kaachika, au zaidi kwa kuwa hana means za kuishi (na hapa ndipo kipato cha mwanamke kinapokuwa na umuhimu zaidi, lisha ya sababu nyinginezo). Mwanamke atatumia hizo pesa lakini ktk ubongo wake wewe mbaya mbaya tuu, tena una disadvantage ya sura ndo kabisaa anakutukana kimoyo moyo huku anapokea au anakusifia na shati lako alilokuasia ili uendelee kutoa.

Women are very good in manouvering situations for their own advantage,

Lazarus Mbilinyi said...

Naungana na watoa maoni wote!

Ni kweli mwanaume kuwa na pesa na kuwa na zura nzuri huweza kuvutia mwanamke na ukweli unabaki kwamba kuna wa sura nzuri au na pesa nyingi bado si msingi wa kudumisha mahusiano bali tabia njema zinazomfanya kila mmoja kuridhika na mahusiano yaliyopo.

Ila ukweli unabaki palepale kwamba tukija suala la mwanamke kuvutiwa na mwanaume wa kuwa naye kimaisha bado mwanaume mwenye mafanikio ( si pesa tu bali idara zate za maisha) anakuwa na nafasi kubwa zaidi ingawa kuna exceptions ambapo pesa wala sura si sababu au sababu.

Asante sana kwa maoni mazuri ambayo yamefafanua kile ambacho zikukiongea.

Upendo daima