"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, April 21, 2010

Aina za Cheating!

AINA ZA KUCHEPUKA (cheating)

Kama wanandoa wapo katika kufanya matengenezo ya damage iliyofanywa na mwanandoa mmoja kuchepuka basi ni muhimu kufahamu kitu ambacho wanashughulika nacho kwani bila kufahamu ni sawa na kumpa mgonjwa wa Malaria dawa za kutuliza maumivu ya meno.

Watu wanaotoka nje ya ndoa wamegawanyika katika makundi makubwa matatu ambayo ni:

1. KUCHEPUKA KWA USIKU MMOJA (one night stand)

2. KUCHEPUKA KWA KUNASWA NA KUFUNGAMANA

3. KUCHEPUKA KWA URAIBU (addiction)

UFAFANUZI ZAIDI:

1. KUCHEPUKA KWA USIKU MMOJA

Mfano mzuri kati Biblia ni namna mfalme Daudi alivyomtamani mwanamke aliyekuwa anaoga (2Samuel 11-12)

Daudi alipomuona yule mwanamke akioga akawaka tamaa, hakuwa na hisia na huyo mwanamke huko nyuma na hata baada ya uzinzi wake.

Hutokea katika jamii ambayo masuala la sex yameilemea, kukosa uadilifu, kukosa nidhamu na kuheshimiana.

Katika modern world ambapo watu wanasafiri (business trips) sana basi cheating za usiku mmoja kwa anandoa zimekuwa nyingi kuliko watu wanavyofikiria hasa baada ya wanawake kuingia kwa wingi katika ajira zinazowafanya wasafiri mara kwa mara.

Hii hutokea kwa kufanya sex kwa usiku mmoja (au mara moja) bila hata kuwa na uhusiano na baada ya sex wahusika hawajuani tena.

Wakishamaliza haja zao kinachofuata ni kumpiga chini huyo mhusika kama vile hawajuani.

Hutokea ghafla kutokana na kushindwa kuhimili tamaa za kimwili au kuwaka kwa tamaa.

Ni rahisi mhusika kurudi kwenye mstari kama vile Daudi alipokuwa confronted na Nabii Nathani aliutubu dhambi yake (2 Samuel 12)

Wanaume au wanawake wa hili kundi akibanwa na kukomaliwa anaacha na kugeuka.

Hii haina maana kwamba cheating kama hii haina damage kwani isiposhughulikiwa vizuri huweza kuzaa affair nyingine.

Kama umefanya affair kama hii na umeficha fahamu kwamba hilo ni bomu ambalo muda wowote linaweza kufumka na kuleta madhala katika ndoa iwe kukosekana kwa ukaribu na partner wako au kujiingiza zaidi kwa mwingine nje ya ndoa.

2. KUCHEPUKA KWA KUNASWA NA KUFUNGAMANA:

Mfano mzuri katika Biblia ni namna Samson alivyonaswa na Delilah (Waamuzi 16).

Hapa cheating huanza kwa mahusiano na urafiki na hatimaye kuwa na uhusiano wa kimapenzi wa kudumu kwa muda mrefu na kuvunja hii bond huhitaji kazi ya ziada.

Hutokea polepole na baadae baada ya urafiki kukomaa kutokana na mazingira ya kufanya kazi pamoja au kuhusiana katika shughuli mbalimbali na kujenga urafiki na mahusiano.

Wanakuwa wame-fall in love kama mahusiano ya ndoa yanavyoanza.

Wanapokuwa pamoja hujikuta wanatimiza lile hitaji ambalo mmoja au wote wanakosa kwenye ndoa zao.

Hapa ndipo tunakuta na neno “nyumba ndogo”.

Huwa kazi sana kuvunja mahusiano kama hayo kwani watu hawa huwa na uhusiano unaohusisha mioyo na hisia zao.

Pia ili kuvunja uhusiano wao lazima mwanandoa ajue “hitaji” ambalo lilikuwa linakosekana nyumbani au katika ndoa hadi mwenzake akanasa kwa huyo mwanamke au mwanaume.

Msemo maarufu wa kingereza ni:

“The hooks in deep and it takes real soul surgery to get it out”

3. KUCHEPUKA KWA URAIBU:

Mfano mzuri katika Biblia ni vitendo vilivyokuwa vinafanywa na watoto wa kuhani Eli (1Samuel 2:22)

Hutokea kwa kusukumwa hisia zake kwa kuwa hana uwezo wa kuhimili emotions ni kama mvuta sigara au mlevi wa pombe.

Haya ni mahusiano tofauti kabisa na kundi la kwanza na la pili hapo juu.

Kwa kuwa ana hisia zinazomsukuma anaweza kuathiri hata maisha yake kwani huwa Huyu huwa na msululu wa partners kila port meli yake inatua au mji.

ladha kutoroka kazi na kujiingiza katika sex haramu kama vile ukahaba, ubakaji, pornography na anaweza kukamatwa na polisi mara kwa mara kutokana na addiction aliyonayo kuhusiana na ngono.

Pia anakuwa na risk kubwa kupata magonjwa ya zinaa (bila kusahau UKIMWI) kutokana na tabia zake, wakati mwingine huuawa kutokana na kuwa violent.

Wakati mwingine anakuwa mwizi, mwongo ili kukamilisha kiu yake (craving)

Pia huendana na tabia chafu na za ajabu zinazohusiana na masuala ya sex kama kubaka, sex kinyume na maumbile, kupigana nk.

Ili kuvunja tabia kama hii huhitaji ushauri (therapy) kutoka kwa mtaalamu wa masuala ya addictions ambaye anaweza kutumia approach tofauti na aina zingine.

NB

Tabia zote zimeelezwa hapo juu ni tabia za mwilini na dawa pekee ambayo inaweza kutoa suluhisho la kudumu KUOKOKA, kujikabidhi kwa BWANA YESU kuwa BWANA NA MWOKOZI wa maisha ya Mhusika.

YESU ANABADILISHA HATA KILE KISICHOWEZEKANA KWA BINADAMU

(Mathayo 19:26, Luka 18:27, Luka 1:37, Marko 10:27, Zakaria 8:6, Yeremia 32:17, Ayubu 42:2 na Mwanzo 18:14)

2 comments:

Anonymous said...

Hello Kaka,
Hii ni funga kazi yaani hapo mwishoni ndo umenibariki zaidi.
Ni kweli kumkimbilia bwana Yesu ndiyo jibu la matatizo yote.

Ubarikiwe
AM

Anonymous said...

nataka niwashauri na kuwabariki wote ambao wenzi wao wanachepuka nje ya ndoa, dawa ni kuamini damu ya Yesu kristo, kama wewe mwanamke mumeo anatoka nje wewe usibishane nae msamehe, ingia chumbani kwako piga magoti karibu na kitanda chako, mwambie Yesu kristo ulinipa huyu mume naomba damu yako inene uzima kwa ndoa yangu ,omba kwa imani mpendwa, sema Mungu namkamata mume wangu kwa damu ya Yesu kristo namfunga asikamate network kwa mwanamke awaye yeyote yule isipokuwa mume wangu akamate network kwangu tu mkewe na ufanye tusikie utamu sana kwa jina la Yesu kristo amen. mpendwa utashuhudia hapa ninachosema, nakwambia hatafanikiwa kwa vimada na atarudi kwako, wanawake wengi imewasaidia sana waume zao waliokuwa wanachepuka damu ya Yesu imewafedhehesha kwa vimada ila kwa wake zao network inakamata vizuri utadhani kuna minara ya yote vodacom, zantel,zain, tigo kwa wakati mmoja tehetehehehe, amini damu ya Yesu kristo haijalishi wewe dini gani ebu omba na amini tu utaona mkono wa Mungu.

mbarikiwe sana

MS GBENNETT