"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, April 16, 2010

Akioa Anakuwa Kimya

Kwa nini mwanaume anakuwa si mwongeaji kama alivyokuwa wakati wa uchumba?

Wote tunafahamu kwamba wakati wa kuchumbiana wahusika (dada na kaka) wote huwa wawazi, wanapeana habari muhimu, wanajadili ndoto za maisha pamoja, wanakuwa na hamu ya kuwa pamoja na inafika Mahali kila mmoja huwa na hofu ya kumkosa mwenzake anapoona siku imepita bila kufahamu yupo wapi ana Anafanya kitu gani.

Huongea heart to heart (lugha ya moyo), na kila mmoja ndani ya moyo wake hujisikia ukaribu na uwazi uliopo na kujiona ni kweli huu ni uzoefu mpya kabisa katika maisha ya binadamu (Na wale wanaotumia moyo hupelekana mbali zaidi ya wale wanaotumia akili)

Kutokana na kuwa wazi na karibu hujikuta wapo attracted kila mmoja kwa mwenzake kiroho na kimwili na kujiona maisha bila mwingine hayana maana.

Mara wanajikuta wapo mbele ya mchungaji na ndoa inafungwa na wanaanza maisha.

Sasa ni kitu gani hutokea kwa kule kuwa wazi kwa mwanaume akishaoa?

Kawaida mwanaume ni mtu wa malengo (goal oriented) hii ina maana kwamba katika uchumba mwanaume huwa na mission ya kumvumbua mwanamke (mke) ambaye atatimiza ndoto zake na njia sahihi ni kuwa wazi na karibu ili wafahamiane.

Kwake ni shughuli nzito ambayo hummaliza pumzi na akiifanikisha hujiona ametimiza malengo.

Baada ya kufanikiwa kumuweka ndani ya nyumba mke aliyekuwa anamuota usiku na mchana kinachofuata ni KURIDHIKA NA KUTOSHEKA katika kuendelea kumvumbua.

Kwake kazi amemaliza na mission accomplished.

Sasa haoni umuhimu wa kuwa wazi na kuwa karibu na mke kwani ni historia.

Wakati huohuo jambo la msingi ni kwamba mwanamke alikubali kuolewa na huyu mwanaume kwa sababu alikuwa muwazi na karibu (intimate) alivutiwa na huyu mwanaume kwa hizo sifa zake na aliamini kwamba hata wakiingia kwenye ndoa mwanaume ataendelea kuwa muwazi na mwongeaji kama alivyokuwa wakati wa uchumba.

Je, ni kweli kwamba wanawake wanapenda sana mwanaume ambaye ni mkimya (asiyeongea) wakiamini kwamba ni msikilizaji mzuri?

1 comment:

Lazarus Mbilinyi said...

Mwanaume anayo attitude ya kuwa "winner".
Alipokuwa katika uchumba lengo lake lilikuwa ni kukupata wewe (mwanamke), ilikuwa ni mission: anafanya lolote analoweza ili kukupata (kuwa wazi, kukusikiliza, kukujali nk).
Baada ya kuoa mwanaume huwa na malengo (goals) mpya kama vile kuwa na familia, kujenga nyumba, kuwa na kazi nzuri zaidi, kusoma zaidi, kuingiza kipato zaidi na kwa kuwa hata huko anataka kuwa winner basi anaelekeza nguvu zote huko na kujikuta amezamishwa na hayo na kusahau kuwa wazi na karibu na mke wake kama wakati wa uchumba.

Upendo na Heshima daima