"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, April 20, 2010

Fanya Mara Tatu

Haina haja kuogopa eti mume wangu anaweza kujiingiza kwenye tatizo la kukosa uaminifu (kuchepuka, kutoa nje ya ndoa, kuanguka, kurudi nyuma, affair, cheating, astray).

Jambo la msingi ni kujiangalia ni namna gani au ni kitu gani unafanya katika ndoa yako kuzuia kitu kama hicho kisitokee.

Kuna wanaume ambao hawa hawafahamu kama wanaweza ku-cheat na hujikuta wame-cheat na hii ina maana kwamba hawakuwahi kupanga kufanya hivyo ila imetokea.

Je, ni vitu gani wanavikosa hapo nyumbani?

Je ni sex, hisia au mawasiliano au heshima?

“Appreciation and respect is the key”

Hata hivyo wapo wanawake ambao wanaamini waume zao hawastahili kupewa respect au appreciation kwa kuwa vyote wanavyofanya ni wajibu wao.

Usijidanganye! Wavunja ndoa ni wanandoa wenyewe!

Ukitaka kujua ni kweli mume ugonjwa wake ni respect na appreciation unachotakiwa kufanya kuanzia leo ni:

Tafuta vitu vitatu ambavyo unaweza kumpa appreciation mume wako inaweza kuwa anavyofanya kazi (kipato katika familia), anavyokusaidia kazi ndogondogo, au anavyokufanya uwe happy au vyovyote vile (please usiseme mume wangu hana cha kupewa respect au appreciation)

Ukikutana naye jioni unaweza kumpa hizo sifa zake na fanya 3 times a week kama mambo hayatabadilika.

Kwa taarifa yako ni kwamba anampenda sana “Yule mwanamke” kwa sababu Anampa respect na appreciation ana ajiona ni winner na anajisikia vizuri.

No comments: