"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, April 9, 2010

Hawajali, Wanatazama Lengo tu!

Wanaume na wanawake ni tofauti na kujitahidi kuondoa tofauti zilizopo wakati mwingine ni kupoteza muda badala yake tunahitaji kuzikubali na kupunguza matarajio .

Wanawake hufurahia harakati au mfumo au mchecheto (process) kufikia lengo wakati wanaume kufurahia kufikia lengo.

Wanaume hufurahia kufikia lengo haraka iwezekanavyo hawana mpango na njia au mfumo au harakati zitakazo tumika kufikia lengo.

MFANO:

Kama mwanamke ataenda ofini au jengo fulani atajitahidi kuzunguka sidewalks zote hadi kufikia mlango wa jingo au ofisi na kuingia. Kwa upande wa mwanaume yeye atakatiza hata kwenye hedges au kukanyaga maua na kwenda straight kwenye mlango na kuingia bila kujali watu watamuaonaje kwani lengo lake ni kufikia mlango wa jengo na kuingia kwenye ofisi au jengo.

Mwanamke akienda kununua kitu dukani (shopping) akifika atachukua gauni au nguo anayoipenda kutoka kwenye racks, ajajiangalia na hiyo nguo kwenye kioo kwa muda wa kutosha then atairudisha kwenye rack na kuendelea na kutafuta nyingine na anaweza kutumia saa nzima kuchagua tu bila kununua na anaweza kwenda duka lingine hadi aridhike ndipo anunue.

Mwanaume akifika dukani kununua nguo anaangalia size kama ni ile anavaa basi anachukua na kulipa na kuondoka zake within 10 minutes.

Linapokuja suala la tendo la ndoa basi mwanaume hulinganishwa hupewa mfano wa gari la mashindano (race car) na mwanamke hulinganishwa na treni la mizigo (freight train).

Hii ina maana kwamba mwanaume siku zote yupo tayari kwa sex, anamaliza haraka, wakati mwanamke husisimka polepole na polepole hufikia mwisho.

Maana yake ni kwamba mume na mke wanahitaji kufahamu mahitaji ya kimapenzi ya kila mmoja.

Kila mmoja anatakiwa kujitoa kwa mwenzake bila kuwa mbinafsi na mchoyo (selfish) pia kuwasiliana na kuzungumza kwa mwenzako (mume na mke) kile unahitaji katika tendo la ndoa ni muhimu sana.

Tendo la ndoa kwa mwanamke huanza kwa kushikana mikono, kukumbatiana, kubusiana, kupeana maneno ya kimapenzi, kusifiana na siyo pale taa zinapozimwa chumbani na mlango kufungwa.

No comments: