"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, April 11, 2010

Je, Bikira Mpya?

The Artificial Virgin Hymen Kit Box is Sold by a Chinese Company.

Je, naweza kuwa bikira tena?

Mimi ni dada mwenye miaka 29 huku nyuma nikiwa na miaka 19 nilijihusiha na kufanya sex na nikapoteza bikira yangu.

Natarajia kuolewa si muda mrefu kwa ndoa na nahitaji msaada kufahamu namna ya kuirudisha bikira yangu upya.

Neema H.

Dada Neema H

Asante sana kwa swali zuri, nami nitajibu swali lako kama ifuatavyo.

Kabla sijafika mbali na swali lako tuone maana ya bikira ambayo ni kuwa na maana kwamba hujaguswa, hajawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi (sex).

Neno bikira hutumiwa pia na vitu vingine kama vile ardhi (ardhi bikira - maana haijaguswa) nk.

Hii ina maana ikishaguswa (ukishafanya sex) si bikira tena NO MATTER WHAT!

Soma hapa kwa maelezo zaidi

Sijajua kwa nini unataka kuwa na bikira tena, inawezekana ulimfunga kamba mchumba wako kwamba wewe ni bikira na uliogopa kusema ukweli kwamba si bikira eti anaweza akuache au kutokuoa, sasa harusi inakaribia na wewe si bikira na unaogopa asije kukushtukia.

Hakuna dawa (pills au medicines) zinazoweza kukufanya uwe bikira upya.

Mtu asikudanganye; anayekwambia unaweza kuwa bikira tena ni mwongo.

Kama unazungumzia bikira kwa maana ya kuwa na kizinda (hymen) tena na ukaonekana chini kumeziba (kanyaboya) unaweza kwenda kwa daktari (plastic surgeon) akakufanyia ukarabati (repair) ya kukijenga kizinda upya na ukaonekana kama vile hajawahi ingiliwa. Pia inategemea upatikanaji wa huyo daktari.

Hata hivyo hiyo haiwezi kukufanya uwe bikira sana sana unaweza kumfunga kamba jamaa yako akadhani hajawahi ingiliwa, kitu ambacho sikushauri na wala Sidhani kama ni business itakayo kuongezea point yoyote kama si kujidanganya mwenyewe.

Kumbuka bado moyoni mwako unajijua si bikira tena.

Kama kengele ilishapigwa ikalia; basi ni historia tuu, ni record kwamba ulikuwa bikira na sasa si bikira na pia hakuna tatizo (tragedy) kwa wewe kutokuwa bikira sasa, kama umeamua kuwa mwaminifu kwa huyo mtarajiwa wako sasa na hata kwenye ndoa yenu.

Unajijua wewe si bikira na kumwambia mtu (mume wako) mtarajiwa kwamba si bikira una kuwa mwongo wa kuogopwa, kimsingi kuanza ndoa kwa misingi ya kudanganya kama unavyofanya si busara na si njia nzuri ya kuanza safari ndoa.

Sidhani kama ni wazo zuri kwako kuwa concerned sana na kuwa bikira tena.

Na siamini kama mume wako mtarajiwa anachokitaka kwako ni wewe kuwa bikira na pia Sijajua kama na yeye (mume wako mtarajiwa ni bikira).

Huna haja ya kuwa na aibu kwa kuwa si bikira tena, kilicho muhimu kwako ni kujisikia vizuri kama ulivyo na kuendelea na maandalizi ya ndoa yako na uwe mwangalifu kwa future ya ndoa yako na kuwekeza upendo na heshima kwa mume wako.

Kwa maelezo zaidi kuhusu bikira soma hapa

2 comments:

Anonymous said...

bwana asifiwe kaka.Hata mimi nachangia hapa,huku ni kujidanganya mwenyewe kama hukuwa mwaminifu katka ubinti wako na sasa unataka kuingia kwenye ndoa na uongo hautafika mbali ushauri,jaribu kuwa mkweli kwa mwenzio mweleze ilikuwaje mpaka ukafanya hivyo na sasa uko vipi kimabadiliko kitabia.Na sijui kama ameokoka au la lakini ukimdanganya siku akigundua kuwa ni mwongo ohooo utakuwa umejipalia mkaa ya moto samahani,ni moja ya ushauri.ek

Lazarus Mbilinyi said...

Dada EK,
Upo sahihi kabisa.

Upendo na heshima daima!