"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, April 8, 2010

Kama Ananipenda.....

Looking is one thing but grabbing is another!

KAMA ANANIPENDA KWA NINI AVUTIWE NA WANAWAKE WENGINE?

Fikiria wewe ni mwanamke upo na mume wako na mume wako anakwambia amekutana na mwanamke mrembo huko barabarani na anavutia sana.

Kama mwanamke utajisikiaje?

Au wewe ni mwanamke na upo na mume wako mnatembea mtaani na mnakutana na mwanamke kisura na mume wako anakunong’oneza na kukwambia huyo mwanamke (kisura) anavutia sana, au hasemi ila unamuona mumeo anamtazama dada wa watu hadi anajisahau.

Utajisikiaje?

Kwa wanawake wengine unaweza kuta mwanaume unazabwa kibao palepale!

Inakuwaje mwanaume akiongea struggles zake za kumuona mwanamke anayevutia husababisha mwanamke kukasirika badala ya kumsaidia au kuona ni kitu cha kawaida?

Ukweli ni kwamba wanaume pia hupenda kuwa wazi kwa wake zao hata hivyo topic ambayo wanapenda kuwashirikisha wake zao husababisha hatari, kutoelewana badala ya kujisikia wanaheshimiwa na wake zao.

Wanawake wengi hujisikii uncomfortable pale mume akiongelea habari za kuvutiwa na mwanamke mwingine (siyo kumtamani bali kuvutia)

Kama kanuni mwanamke huhitaji ukaribu wa kimapenzi (intimacy) kutoka kwa mume wake ili ajisikia anapendwa, ukaribu huo ni pamoja na sharing ya habari kuhusu struggles za maisha, lakini mwanaume akiongelea struggles za mwanamke mwingine kwamba alimvutia basi moja kwa moja mwanamke anakuwa uncomfortable.

Kwa maneno mengine mke anamwambia mume wake

“ Unatakiwa kuwa kama sisi wanawake, hatuvutiwi kwa kuona mwanaume, hivyo usivutiwe kwa kuona mwanamke”

Kama ni mwanaume ukiongea na mke kuhusu hofu za maisha, mwanamke kujiamini, namna ya kupunguza uzito, ndugu zake, uimbaji na marafiki zake basi mke hujisikii vizuri, tatizo ni kwamba mwanaume hana tatizo na hofu za maisha, mwanaume kujiamini, au kupunguza uzito au marafiki, ndugu nk.

Mke hawezi kukuelewa kama unaweza kumpenda na ukavutiwa na mwanamke mwenye shingo ndefu kazini au unayemuona njiani.

Mke anaamini unamdanganya, anaamini unavutiwa kwa sababu umekuwa na muda (spend) mwingi na yeye ndiyo maana anakuvutia au unataka kutumia muda na yeye.

Anaamini unaongea naye sana na mnajuana sana na mpo close ndiyo maana anakuvutia.

Haamini kama wewe mwanaume unaweza kuvutiwa na mwanamke ambaye hata humjui au humfahamu.

Anataka ujue kwamba kama mwanaume huruhusiwi kuvutiwa na mwanamke yeyote no matter what!

Na hapendi kusikia hizo habari tena.

Mwanaume huathiriwa sana na kile anaona na linapokuja suala la mwanamke anayependeza mwanaume hukutana na struggle kwani ndivyo alivyoumbwa kwamba kwa kuona anakuwa stimulated.

Hakuomba iwe hivyo, bali amezaliwa yupo hivyo na hawezi kukimbia wala kujificha.

Yesu mwenyewe alijua kwamba wanaume wanaweza kuleta maafa kwa namna wanavyomwangalia mwanamke (anayependeza) ndiyo maana akawaambia “Amtazamae mwanamke kwa kutamani ameshazini naye (Mathayo5:28)

Mwanamke anayetamani kuwa karibu na mume wake, mume kuwa wazi kwake, mume kumuelewa anaweza kufanikiwa pale tu akizingatia haya mambo mawili

KWANZA

Kumtimizia mume wake hitaji la tendo la ndoa (sexual release) hata kama mke hayupo kwenye mood.

PILI

Jitahidi kuhakikisha mume wako anaelewa kwamba unaolewa kwamba na yeye anajaribiwa kwa kuvutiwa na mwanamke mwingine anapomuona si lazima kwamba anamtamani au anamjua au anatumia muda na yeye bali anavutiwa kwa sababu ni mwanaume ambaye anaathirika kwa kile anaona.

Ukimsikiliza namna ana struggle kutakuwa na opportunity ya kuwa marafiki na wapenzi wazuri.

SUMMARY

Mume wako ataona unamheshimu pale utakapo;

Itikia kimapenzi (sexually kwake na wakati mwingine wewe mwanamke kumtaka (initiate) yeye.

Unapotambua kwamba anahitaji tendo la ndoa (sexual release) kama wewe unavyohitaji upendo (emotional release)

Kumpa uhuru wa kujieleza kwamba na yeye ana struggle na jaribu la kuvutiwa na mwanamke yeyote bila wewe Kuamini kwamba anaweza asiwe mwaminifu kwako.

Usimfanye aongee au akupende au akusaidie kazi kwa wewe kumnyima tendo la ndoa.

2 comments:

Anonymous said...

Bwana asifiwe kaka Mbilinyi, je mme wangu akiniambia kwamba anavutiwa na dada mmoja wanafanya nae kazi je mimi napaswa kumjibu nini ama kumshauri nini? ili asiendeelee kuniambia kuwa anavutiwa na akina dada wengine?

Ubarikiwe!

Lazarus Mbilinyi said...

Dada asante sana kwa swali zuri.
kwanza inabidi umshukuru kwa yeye kuwa wazi kukupa taarifa kama hizo hii ina maana sasa si tatizo lake bali tatizo lenu wote, ikiwa tu hana maana ya kutaka kukufahamisha kwamba anavutiwa na huyo dada kwa sababu wewe umeonesha aina fulani ya kusababisha yeye ajione havutii kwa wanawake wengine.
Jambo la msingi ni kukaa wewe na yeye na kujadili namna mnaweza kusaidiana ili kushinda hili jaribu la yeye kuvutiwa na huyo dada kazini. Inabidi muwekane sawa kwa kujadili mikakati mbalimbali ambayo mnaweza kuiweka.
ubarikiwe na Bwana.