"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, April 26, 2010

Kubemenda!

Karen Lazarus Mbilinyi
(Miezi saba sasa kubemendwa kupo wapi?)

SWALI:
Shalom mtumishi wa MUNGU!
Ni matumaini yangu kuwa wewe na familia mnaendelea vizuri.
Sisi pia BWANA anaendelea kututunza na kutufanikisha ktk yote.
Kama ambavyo nimewahi kusema awali kuwa nimekuwa msomaji sana wa blog yenu na imekuwa shule nzuri kwangu kama ambavyo naamini wengi wamenufaika nayo.
Juzi nilisoma comment ya mtu mmoja ambaye alikuwa ana criticize kunena kwa lugha wakati wa tendo la ndoa; nilifurahia sana jibu lako kwani MUNGU anahusika sana na tendo hilo.
Sasa leo nina concern ambayo najua mtanisaidia kwa sababu ya uzoefu wako kama watu mliotangulia ktk kuwa wazazi.
Kuna hili suala linaloitwa 'kubemenda' mtoto, watu wanadai kuwa sperms huwa zinaleta madhara kwenye maziwa ya mama na kumdhoofisha mtoto kiafya na wengine wanasema ukimshika mtoto baada ya sex pia ina madhara.
Tunaomba uzoefu wenu watumishi ktk hili kwani nimewahi kusoma article ya mtu mmoja kwenye mtandao ambaye alijiita daktari na kusema hakuna kitu kama hicho ni imani tu.
MAY GOD RICHLY
BLESS YOU!
JIBU:
Asante sana kwa swali zuri ambalo naamini si geni sana kwa wanandoa wapya katika jamii za kitanzania.
Kama alivyosoma kwenye article ya huyo Daktari ni kweli suala la Kubemenda ni imani potofu (myth) na hakuna uhusiano wa sperms na maziwa ya mama katika kudhoofisha afya ya mtoto; iwe kwa kushirikiana tendo la ndoa au kumshika mtoto baada ya sex.
Je, nini maana ya kubemenda mtoto?
Kwanza hii imani potofu inaeleza kwamba kubemenda mtoto ni pale wanandoa wanapojihusisha na tendo la ndoa baada ya mtoto Kuzaliwa (pale mke anapokuwa tayari kiafya kwa tendo la ndoa baada ya kujifungua) kwa maana kwamba sperms huharibu maziwa ambayo mtoto ananyonya, si kweli hakuna uhusiano wowote kati ya maziwa ya mama na sperms katika kuathiri afya ya mtoto.
Pili kubemenda mtoto ni kitendo cha wanandoa kujihusisha na tendo la ndoa na mke kushika mimba miezi mwili tu au mitatu tu baada ya kujifungua na kupelekea kuzaa mtoto mwingine baada ya mwaka na matokeo yake mtoto aliyetangulia Kuzaliwa huwa dhaifu kiafya (huchelewa kutembea) na huitwa ni mtoto ambaye amebemendwa, kitu ambacho ni imani potofu kwani kuna wanandoa wengi tu wamezaa watoto waliopishana mwaka na wote wana afya njema kabisa.
Tatu kubemenda ni kitendo cha mwanandoa mmoja kutoka nje ya ndoa (sex) na akirudi ndani huendelea na tendo la ndoa na matokeo yake mtoto wa ndani ya ndoa huwa dhaifu, pia ni imani potofu hakuna kitu kama hicho.
Je, Biblia inasema nini kuhusu tendo la ndoa baada ya kujifungua.
Ndiyo kuna andiko (Mambo ya Walawi 12:1-5) linalotaja lini mwanamke ajihusishe na tendo la ndoa baada ya kujifungua na si hivyo tu bali ni wakati gani mtoto wa kiume atahiriwe.
Hata hivyo sheria hii ni moja ya sheria na maagano 6 ambayo Mungu alitoa kwa watu tofauti kwa wakati maalumu na leo wayahudi hufuata zaidi huo utaratibu kwetu sisi Kristo amemaliza yote msalabani na jambo la msingi ni kufuata ushauri wa kitaalamu ambao ni wiki sita baada ya kujifungua.
Je, kuna ukweli wowote kuhusiana na hii imani potofu
Iwe wanandoa kujihusisha na tendo la ndoa baada ya mtoto Kuzaliwa au kuzaa mwingine baada ya mwaka au hata kutoka nje hakuna uhusiano na mtoto aliyezaliwa kama suala la usafi na lishe bora litazingatiwa kwa mtoto anayehusika.
Je, kulikoni mababu zetu wakaweka imani kama hiyo kwa wanandoa?
Kama zilivyo imani zingine potofu kama vile mwanamke mjamzito kutokula mayai mababu zetu walikuwa na somo ndani yake, inawezekana walitaka kuhakikisha wanandoa wanashiriki vizuri katika kulea mtoto kwa pamoja bila kupendekeza tabia za uchafu na kujirusha nje na ndani ya ndoa bila utaratibu.
Pia labda mababu zetu walihofia kitendo cha mwanamke kutoa maziwa (chuluzika) wakati wa tendo la ndoa hasa anapofika kileleni (tangu akifungue hadi miezi 8 hivi) na wakawa wanahofia kinaweza kuathiri kiwango cha chakula cha mtoto hivyo ili kuzuia ni kutunga imani (potofu) kwamba mtoto ataathirika kwa mke na mume kushiriki tendo la ndoa.
Je, ili mtoto asionekane amebemendwa wanandoa wanahitaji kufanya kitu gani?
Ni vizuri kufahamu kwamba hakuna uhusiano wa sperms kuharibu maziwa ya mama wakati wa kumnyonyesha mtoto hivyo wanandoa kushiriki tendo la ndoa halina uhusiano wowote na mtoto kuwa na afya mbaya kiasi cha kuchelewa kutembea.
Mtoto anahitaji watoto chakula bora chenye viini-lishe vyote vinavyohitajika ili kukua vizuri pia mama anahitaji kujiweka mazingira safi (kuwa msafi) wakati ananyonyesha, ahakikishe anasafisha chuchu zake na mikono yake au kuzingatia usafi kimwili kabla ya kumnyonyesha mtoto iwe baada ya sex au muda wowote.
Ni jukumu la baba na mama wa mtoto kuhakikisha wanatumia muda wao kuhakikisha mtoto anapata lishe bora na mahitaji yote ya msingi ya mtoto ili kukua na kuwa na afya njema na si kujinyima kujihusisha na tendo la ndoa wakihofia mtoto kuonekana amebemendwa.
Pia suala la usafi wa mazingira ya mtoto anapoishi (vyombo vya kutumia kwa chakula cha mtoto, usafi wa mwili wa mtoto na mama na baba pia) ni muhimu sana kwani baada ya tendo la ndoa ni muhimu kwa mume na mke kuhakikisha wanakuwa safi tena bila kujihusisha na kumnyonyesha mtoto huku hawajanawa au kuoga.
NB:
Suala la kubemenda (binafsi naweza kuita ni utapiamlo au kwashakoo kingereza- Kwashiorkor) huzungumzwa sana na jamii za “mtanzania wa kawaida” huwezi kusikia katika nchi zilizoendelea na watu ambao wameenda shule na wanafuata misingi ya afya na uzazi katika kulea watoto wao na pia mke na mume kuwa karibu kimapenzi.
Huwezi kusikia takataka za neno kubemenda katika nchi zilizoendelea kama Canada, Sweden, Australia, Ujerumani nk why? Ni traditions (Myth).

12 comments:

Anonymous said...

Watumishi inawezekana kubemenda kupo. hata kama madaktari wanasema halipo nadhani linahitaji uchunguzi. yapo mambo mengi mwanadamu hajapata kujua chanzo, ht ukimwi, cancer nk unajionea mwenyewe. mimi hili jambo limenisumbua, mwanangu alikuwa anadhohofika na tulifuata ushauri wa dk.Lakini baada ya kumpeleka kwa bibi yake, sasa ndo nimegundua kubemenda inawezekana kupo. Take care!
Rutajama, Dar es Salaam.

Lazarus Mbilinyi said...

Kama nilivyosema kubemenda ni imani potofu, ndivyo ilivyo.
Mwenyewe nina watoto wawili wote wana afya njema na wote wameteanza kutembea kablya ya umri wa kawaida na wana afya njema kabisa hadi wengine huuliza unawatunzaje watoto wako.
Ukweli ni kuhakikisha wanapata lishe bora, usafi na mahitaji yote mtoto anahitaji wakati huohuo sisi kama wanandoa tunaendelea na intimacy kama kawaida.
Hivyo mimi nina ushahidi kwamba kubemenda ni imani potofu, ndivyo naamini na ndivyo ilivyo.
Hili ni suala la imani na binadamu akishajiingiza kwenye imani basi hatoki hata kama hiyo imani imepitwa na wakati.
Naamini hekima ni kwa wale wanaoamini kuendelea kuamini na kuendelea kujinyima kuwa karibu (sex) katika ndoa zao huku wakiogopa kitu ambacho hakipo na wale ambao hatuamini tuendelee kutoamini huku tukiendelea kufurahia ukaribu wa kimapenzi huku watoto wakiwa na afya njema.
Swali je, mnaoamini kubemenda kupo ni lini mnarudiana (resume) tendo la ndoa au ni hadi mtoto awe na umri miaka mingapi?
Kazi kwelikweli!

Upendo na Heshima daima.

Yasinta Ngonyani said...

kwa kweli hizo lazima zitakuwa mila na sijui za kibena kaka Lazarus mimi sijawahi kusekia hilo neno. Pia nina watoto na walikuwa na afya njema kabisa walipokuwa wadogo na walitem,bea mapema ajabu.

Anonymous said...

Habari za kazi kaka Mbilinyi, mimi ninavyoona kubemenda kupo kama mmoja kati ya wenye huyo mtoto atatoka nje ya ndoa na akirudi kumshikashika mtoto au kufanya mapenzi na mwenza wake hapo ni kweli mtoto anaharibika, ila kwa wanandoa wenyewe kama ni waaminifu, na pia wanamjali mtoto siyo sex tuu bila kuwa na kiasi hapo hakuna kubemenda mtoto. Mimi nimeowaona kabisa watoto waliobemendwa tena huwa tunawaita mafundi wa viatu maana akikaa chini hukunja miguu tuu mpaka miaka miwili inakatika hatambai wala hasimami

Anonymous said...

Hapa ni kazi kweli mimi binafsi sikubaliani na kitu kama hicho, mimi na mume wangu tunao watoto watatu hakuna mtoto ambaye ametembea zaidi ya miezi kumi, mdogo kabisa ana miezi miezi nane na anasisima. Halafu kwa kweli baada ya mimi kupona baada ya kujifungua huwa tunaendelea na sex kama kawaida ila suala la kuhakikisha mtoto anakula vizuri na usafi hayo tunayapa kipau mbele

Anonymous said...

Mimi nimekuwa nikisikia sana kuhusu hilo, ila nina mtoto wa miezi sita ambaye kwa sasa anatambaa na kweli nilikuwa ninahofu sana baada ya kujifungua kwamba nitafanyaje ili nisimbemende first born wangu ingawa mume wangu alikuwa akiniambia hakuna kitu kama hicho, ukweli ninacheza game (sex) kama kawaida na mtoto wangu yupo vizuri kabisa ana afya na nguvu.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,
Naungana na wewe kwamba hiyo ni imani potofu tu. Hata kama wengine mnasema kupo ni mtazamo wenu na traditions tu scientifically hakuna kitu kama hicho hakuna cha wabena wala wangoni ni imani potofu.

Pia kuna hatari kubwa kuamini vitu kama hivyo kwani mtoto anaweza kuchelewa kutembea na wanandoa wakaanza kutoa macho nani kasababisha (katoka nje ya ndoa) kumbe hakuna aliyetoka na kuchelewa kwa mtoto kutembea (mafundi viatu) ni sababu za kukosa lishe bora au suala la afya tu.
Na pia hatari kubwa nyingine ni kwamba mtoto anaweza kuwa na afya njema na mwanandoa mwingine akawa anatoka nje na kukaonekana hakuna tatizo kwa kuwa mtoto ana afya njema kumbe mwingine anatoka.
Imani ni imani na binadamu ni wagumu sana kuwatoa kwenye imani ndiyo maana nakubali kwamba wapo wanaoamini na tupo tusioamini hata chembe.
Pia nilikuwa sijajua kama kuna watu wanaamini hii kitu kwa msimamo mkali hivi.

Kazi kwelikweli!

Upendo na heshima daima

Lazarus Mbilinyi said...

Mimi na mke wangu tunaungana na wote wanaoamini kwamba kubemenda ni imani potofu na hakuna ukweli wowote, ukiacha scientific research zinazoafiki kwamba hakuna kitu kama hicho pia na sisi ni mashahidi kwani tuna watoto wawili na wa kwanza alitembea akiwa na miezi mapema kabla ya wakati na wa pili sasa ana miezi 7 anasimama na yupo fit kiafya na tunaamini si muda mrefu atakuwa anatembea.
Jambo la msingi ni lishe bora na usafi kwa wanandoa period.
Kuamini vinginevyo ni kujipa hofu mwenyewe na hizo imani.

Upendo na heshima daima!

Anonymous said...

great content!

Anonymous said...

Inasemekana wazee wa zamani walikuwa wanasema hivyo ili kuogopesha watu wasifanye tendo la ndoa kipindi hiko kwasababu walishindwa kutoa maelezi kamili ya kisayansi lakini ikumbukwe kipindi hicho kulikuwa hakuna contraceptives na vilevile wanasayansi wameprove mwanamke anaeweza pata mimba akiwa ananyonyesha na mwanamke akipata mimba tena mtoto atakosa maziwa ya mama sababu milk production itakuwa stopped na akaishia kupata malnutrition

Anonymous said...

Nafkiri hakuna ubishi kwamba hili neno is a mere myth na sababu ya kuwepo hiyo imeelezwa vizuri na mdau aliyecomment kabla yangu.

Kazi nzuri Wapendwa.

Anonymous said...

Mm naomba mnisaidie wapendwa wenzangu mke wangu nilisex nae lakuni alimnyonyrsha mtoto ksbls hajaoga je inaweza kumuathiri mtoto kiafya yaani kumbemenda......kwan mpaka sasa mroto ana mwaka hajasnza kutembea.......