"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, April 27, 2010

Ni Sensitive Mno!

Kuna uwezekano mkubwa kwamba kukiwa na tatizo linalohusiana na suala la mahusiano katika ndoa au uchumba kati ya 10 ni mara 9 mwanamke ndiye atakuwa wa kwanza kujua au kugundua hilo tatizo.

Pamoja na huo uwezo wa kugundua tatizo kinachosumbua wanaume wengi ni ile hali ya kutaka kurekebisha au kukefyakefya kutaka tatizo lijadiliwe hapo hapo ingawa kwa upande wa mwanaume wakati mwingine huonekana si tatizo kubwa au hatari kwa mahusiano (kwa mtazamo wa mwanaume) ingawa wakati mwingine ni kweli huwa ni tatizo.

Huyu mwanaume na mwanamke wakiingia kwenye ndoa hali huwa mbaya zaidi kwani mwanaume hugundua kwamba huyu mwanamke ni sensitive mno na itakuwaje kuishi naye kwa namna alivyo.

Ni kweli mwanaume huwa sahihi kwamba mwanamke ni kiumbe sensitive na ni muhimu sana mwanaume kufurahia mke kuwa sensitive kwani kwa mke kuwa sensitive ndiko husaidia;

Mke wako kukaa macho usiku mzima kuhakikisha mtoto anayeumwa anakuwa katika uangalizi wa karibu hata kama wewe mwanaume utakuwa unakoroma kwa usingizi mzito.

Awe concerned na wewe unapoumwa kuhakikisha anakusukuma kwa nguvu zote hadi unaenda kwa daktari au una meza dawa hata kama ulikuwa umesahau na matokeo yake umepona.

Kuwa sensitive kwake kumsaidia kukurudisha kwenye mstari baada ya wewe kuanza kujiweka mbali.

Kuwa sensitive kwake ndiko kumefanya ujulikane kwamba wewe ni mwanaume mzuri sana linapokuja suala la misiba kwani yeye ndiye hukusukuma kuhakikisha mnaenda kwenye msiba pamoja na sababu zako za kutaka kushinda unaangalia TV (sports).

Kuwa sensitive kwake ndiko kumsaidia wewe kuwajali ndugu zako kwani kila wakikutafuta Unasema upo busy na kumbe ni mzito linapokuja suala la kusaidia ndugu zako na mke wako ndiye amekuwa mstari wa mbele.

Kuwa sensitive kwake ndiko kumesababisha uonekana ni mwanaume unayetoa michango mbalimbali kwenye jamii mnayoishi kwani huwa hujali umetoa au hujatoa “who cares! Bila mke wako kukuvalia njuga usingetoa.

Kuwa sensitive kwake ndo kumefanya ndoa yako ionekane imara kwani pamoja na vurugu unazofanya amekuwa akikusamehe na kuendelea kukuheshimu na kukupenda.

Kuwa sensitive kwake ndiyo kumefanya uonekana ni mwanaume smart kwa kuwa huhakikisha anafahamu ni nguo gani unatakiwa kuvaa na zinakuwa safi hata kama hajawahi kusema asante mke wangu!

Kuwa sensitive kwake ndo kumefanya nyumba yako ionekane ni safi muda wote kwa kuwa mke wako huhakikisha nyumba inakuwa safi ili ukija na wageni wako uonekane ni kweli una nyumba nzuri hata kama hajawahi msaidia kazi ndogondogo hapo nyumbani.

Kuna mambo mengi tu mke wako amefanya kwa kuwa yupo sensitive na wewe hujui!

Unaweza kujisemea moyoni ni afadhari kuwa na mke ambaye si sensitive kama alivyo mke wako hata hivyo ni muhimu ufahamu kwamba hiyo ni strength moja muhimu sana kwa wanandoa.

Jambo la msingi ni wewe kuwa wazi na sharing kwa mke wako kwani kwa uamuzi wako unaweza kusababisha siku kuwa nzuri au mbaya.

&&&&&&&&&&&&&&&&&&

No comments: