"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, April 28, 2010

Mchecheto kweli!

Hapo tunaalikwa kwa kadi la nguvu!

Iwe ni kanisani, au chini ya mti, au shambani, au kwenye park, au kwenye meli au angani kawaida kuna kitu kimoja ambacho hufanana ukiacha utofauti wa kimazingira nacho ni kwamba wahusika wote hujawa na furaha na matarajio mapya kwa ajili ya future.

Bibi Harusi:

Humeremeta mithili ya malaika, uso wake hufunikwa na furaha na namna anaonekana hutoa picha kamili namna alivyo na uhakika na matarajio yake ya ndoa yatakavyotimizwa.

Anakuwa na mchecheto wa kuharakisha kutoa ahadi na kuweka agano mbele ya mume mtarajiwa na mbele ya Mungu.

Anamshika mkono mwanaume ambaye amemchagua kuishi naye maisha yako yote yaliyobaki duniani.

Baada ya miezi sita tu, jehanamu inaanza na machozi yanaanza kutiririka kwenye mashavu yake na anasema

“Ni kitu gani nilikiona kwake hata nikajidanganya kuoana naye?”

Bwana harusi:

Anamshika mkono laini wa binti ambaye amemchagua katika maisha yake na sasa anaenda mbele za Mungu kutoa kiapo na ahadi ya kuishi pamoja katika raha na shida, afya na ugonjwa hadi kifo kitakapo watenganisha.

Amemchagua kuwa malkia wake na kwamba anampenda, na kumlinda na kumpa mahitaji yake yote.

Baada ya miezi sita na yeye analia machozi na kujuta

“Inakuwaje jambo hili linatokea, nilidhani nimemfahamu vizuri hivi ni mwanamke gani nimeoa?”

Kama hujaoa au kuolewa unatakiwa kuwa makini hili jambo lisitokee.

Je, kwa nini baada ya kuoana watu hukutana na frustrations nyingi?

Sababu kubwa ni:-

Higher expectations and low preparations.

Hata kama una nusu akili likija suala la kuona hakuna anayekuzuia kwani ni haki yako, ila jambo kubwa ni namna utakavyoweza kuishi kwenye ndoa yako.

Nchi nyingi duniani zinaweza kukunyima leseni ya kuendesha gari ila likija suala la leseni ya kuoa (marriage certificate) unapata kirahisi tu.

Unatakiwa kujua namna ya kuendesha gari kabla ya kuliendesha.

Unatakiwa kujua elimu ya udaktari kabla ya kuanza kutibu wagonjwa.

Unatakiwa kwenda chuo cha ualimu na kumaliza mafunzo ndipo uwe mwalimu.

Je, una ufahamu na elimu ya kutosha kuhusu ndoa?

Kuwa na matarajio makubwa sana kwa ndoa yako pia husababisha kuwa unhappy kwenye ndoa.

No comments: