"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, April 6, 2010

Miezi 3 tu!

Three months rule:

Uwe kijana au mzee linapokuja suala la mapenzi ni suala lisilo kwepeka hata hivyo kuwa mwangalifu ndicho kitu cha msingi kuliko kitu chochote na ili kumfahamu mtu unahitaji kitu kinaitwa MUDA.

Miezi mitatu ni magic number ya kumfahamu mtu research na study nyingi zinakiri.

Unahitaji kusubiri hadi mwezi wa tatu kwa mtu kuanza kuonesha namna au jinsi alivyo kihalisi (deep seated patterns) sahihi za mtu unayetaka kuwa na mahusiano naye huanza kuonekana.

Hii ina maana kwamba upya wake au ule umaalumu wake kwako huanza kuchakaa na unaanza kumuona mtu wa kawaida.

Vichekesho vyake utaanza kuvizoea, tabia zake alizokuwa anaficha zitaanza kuonekana wazi.

Hii ina maana kwamba kuoana na mtu ndani ya miezi 3 ni risk kubwa mno labda Mungu awe ameongea na wewe uso kwa uso kama Musa.

No comments: