"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, April 22, 2010

Ndivyo Walivyo!

Wanaume hawapo interested in losing battle.

Wapo trained kushindwa na wasipo shinda kama timu basi angalau yeye binafsi awe na sifa inayoonesha alikuwa tofauti.

Wanaume wanapotazama sport yoyote let say Soka, mood hubadilika kutokana na matokeo.

Kama mume wako ni shabiki ya timu fulani (iwe Yanga, Simba, Arsenal, Man U, Liverpool nk) siku timu yake kufungwa unajua na siku ikishinda unajua na kuna tofauti kubwa katika mood.

Hata hivyo hiyo attitude ya ku-win ina uhusiano mkubwa sana na ndoa yake.

Mke anayemfanya mwanaume kujiona failure na loser nyumbani kwake humpa wakati mgumu sana mume wake kwani huharibu kabisa utu wake (ego) kiasi ambacho ni hatari sana kwa mahusiano yao ya ndoa.

Mwanaume akishajisemea moyoni sentensi ifuatayo “I feel I can’t win no matter what I do” basi mwanamke inabidi ajipange upya.

Kinachotokea kwa huyu mwanaume ni kujiweka kwenye kibox chake na kuwa mbali na mwanamke kihisia na mke hujisikia mume yupo unloving na ndipo mgogoro huanza.

Mwanamke anayempokea mume kwa uso wa huzuni na hasira na maneno mengi ya kusemana na kulalamika (kefyakefya) bila kumpa hata dakika kadhaa apumzike au kama kila siku akirudi nyumbani jioni anakutana na kasheshe kutoka kwa mke, mwanaume hujiona ni loser na failure na atafanya kila analoweza kukwepa kurudi mapema nyumbani.

“When a man can’t win at home, he will start looking to win somewhere else”

Pia wapo wanawake huwatuhumu mno waume zao (too much suspicious) kiasi cha kusababisha mume kujisikia haheshimiwi na matokeo yake mwanaume huamua kufanya kweli kwa kufanya kile mke anamtuhumu.

“Why go lengths to avoid cheating if my wife is going to think I am cheating?”

Kama haheshimiwi nyumbani basi ataanza kutafuta ne game ambayo itamfanya kujiona anaheshimiwa.

Jambo linaloleta matumaini ni kwamba:

Mume anapojisikia ana win nyumbani kwake atajitahidi kufanya kila anachoweza kum-please mke wake hapo nyumbani.

Hii ina maana mke anayempa mume wake respect, appreciation na loving gesture basi atamwezesha mume kufanya kazi kwa kujituma na atakuwa sensitive kutimiza mahitaji ya mke wake kimwili na kiroho.

No comments: