"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, April 15, 2010

Ni Kelele tu!

SWALI:

Nina swali linalonitatiza, Mimi ni mwanamke ambaye nimezaa mtoto miezi 6 iliyopita kinachotokea ni kwamba kila tukiwa kwenye tendo la ndoa na mume wangu uke hutoa sauti ambayo inayokera sana.

Na wakati mwingine mume wangu akiwa ndani yangu najisikia kama anasukuma hewa ndani na najisikia maumivu kwa mbali.

Je, kwa nini hii hutokea?

Je, kuna njia ya kuondoa tatizo hili?

JIBU:

Asante sana kwa swali zuri na Samahani kwa kuchelewa kukujibu swali lako hasa kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uweza wa binadamu yeyote chini ya uso wa dunia.

Ni kweli kutokana na maelezo yako mkiwa kwenye tendo la ndoa hewa hupenya ndani ya uke wako na kutoa sauti ambayo inakukera (kama mtu anayetoa gas)

Uke ni kiungo cha ajabu (elastic tube) ambacho huweza kutanuka size ambayo huwezesha mtoto anayezaliwa kupita kuja kwenye uso wa dunia.

Kuzaliwa mtoto huweza kubadili size na shape kwa muda (temporarily) ya uke na pia process nzima ya kuzaa (labour & delivery) huweza kuathiri nerves (damage) na kulegeza misuli na kufanya uke kupwaya (loose) au uke huwa mpana zaidi.

Namna uke unavyobadilika (size/shape na weakness) hutegemea vitu vingi mojawapo ni kama muda kiasi gani mwanamke alitumia kwa ajili ya labour (uchungu na kusukuma mtoto), size ya mtoto, idadi ya watoto, uimara wa misuli yake ya uke na genetics.

Inawezekana sasa size na shape ya uke wako haipo sawa (ni kubwa) ukilinganisha wakati kabla hujazaa hivyo basi size mpya inawezesha hewa kupenya na kuingia na hatimaye hunasa ndani (trapped) wakati wa tendo la ndoa.

Hivyo sauti inayotoka ni hewa inayojaribu kutoroka ndani ya uke.

NB:

Mwanamke anapokuwa amesisimka uke hupanuka na urefu wake huongezeka pia kitendo kinacho create vacuum kwenye uke.

Wakati wa sex hewa husukumwa ndani na kunasa huko na wanavyoendelea na tendo la ndoa hutokea msukumo na mgandamizo ambao husababisha kelele za ajabu.

Si kelele za mdomoni wala kitanda bali kelele za uke kama vile tyre la baiskeli linavyopiga kelele wakati mwingine linavyojazwa upepo kimaridadi kabisa.

Hivyo wakati mwingine ni jambo la kawaida haina haja kubabaika badala yake celebrate!

JE, HILI TATIZO LINAWEZA KUDUMU?

Jibu ni ndiyo au hapana.

Ni ndiyo kama hutachukua hatua yoyote yaani utaridhika na hali iliyopo.

Ni hapana; Kama utachukua hatua ili kurudisha umbo lako la uke kwenye original state (size, shape, strength) au kukaribia na ilivyokuwa mwanzo na hii hutokea haraka pale tu utakapoipa misuli ya uke (PC Muscle) mazoezi na zoezi muhimu ni zoezi la kegel.

Misuli ikikaza hutaweza kusikia hiyo milio ya ajabu kwani kutakuwa hakuna njia ya hewa kupita ili kuingia ndani.

Kwa maelezo zaidi ya misuli ya PC (kegel) bonyeza hapa na kuhusu zoezi la misuli ya PC (kegel) bonyeza hapa.

Kama unajisikia maumivu basi hapo kuna tatizo na inawezekana ni kutokana na kushuka kwa uterus na cervix kutokana na hekaheka za kusukuma mtoto wakati wa kuzaa na kinachofanyika ni kwamba mume wako hugonga hilo eneo wakati wa tendo la ndoa.

Unachoweza kufanya ni kutumia love making position ambazo wewe utajisikia comfortable.

Ukiona hakuna mabadiliko katika maumivu inabidi umuone daktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi isije kuwa unaumwa Recto- Vaginal fistula tatizo ambalo husababishwa na kuharibika kwa tissue kati ya rectum na vagina na matokeo yake badala ya gas kupita huko inatakiwa kupita hubadili njia na kupita kwenye uke.

No comments: