"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, April 6, 2010

Ni muhimu Pia

MAMBO MUHIMU KUJADILIA KABLA YA KUOANA

AKILI (intelligence)

Ingawa kuna intelligence za aina tofauti kama vile kusoma (learning), ufahamu (common sense), ufundi nk.

Je, upo tayari kuoana na mwanaume mwenye PhD ambaye akienda store au Mall hawezi kujua maziwa yanapatikana sehemu gani ila ukimpa Computer anaichambua kama karanga.

Au upo tayari kuoana na darasa la saba ambaye ukimpa injini ya gari yenye matatizo anaitengeneza na kujua tatizo kama vile ndiye aliyegundua injini za magari.

Kama unahitaji spouse ambaye ni smart kuliko wewe Please don’t go for less tafuta mtu anaye-fit specification zako.

KIROHO

Kama maisha ya kiroho kwako ni muhimu sana basi kuoana na mtu ambaye anatofautiana dini na wewe lazima mbele ya safari utalipa gharama kubwa sana No matter what, you are going to pay the price!

Kama hajaweza kuokokan au kubadili dini kabla ya kukuoa nini kitamfanya aokoke au abadili dini wakati tayari anajua wewe ni mke wake?

VITU

Je ana value vitu kuliko watu?

Je, wewe una ndoto ya nyumba (jengo) aina gani au namna gani?

Je, unapenda kuwa na watoto wasome wapi? International schools au shule za kawaida.

Kuna wanandoa wapya (mwezi mmoja tangu waoane) kwa bahati mbaya wakati wanatuandalia chakula mke alivunja glass ile vita iliyotokea sitasahau bahati mbaya mwanamke alihamia kwa mwanaume ambaye kila kitu amenunua yeye mwanaume hadi kijiko cha chai.

WATOTO

Hatuoani ili kuwa na watoto bali watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu na hakuna binadamu mwenye uwezo wa kukiri mia kwa mia kwamba akioa au kuolewa atakuwa na uwezo wa kupata watoto, hata hivyo kuzungumzia issues zinazohusu watoto ni muhimu sana kabla ya kuoana.

Unataka watoto wangapi, isije wewe ukawa anataka watoto 2 mwenzako anataka watoto 8.

Lini mzae watoto, kwani mtoto anapozaliwa hubadilisha kila kitu na ndoa nyingi zimevunjika kwa sababu ya kuzaliwa mtoto/watoto bila maandalizi.

Je, nini mtazamo wako na mtazamo wa mwenzako kuhusu kulea watoto ni jambo la msingi sana kujadili.

ARI YA KUFANYA MAMBO MAKUBWA AU TOFAUTI (ambition)

Je, unapenda au kuwaza kuoana na mtu mwenye malengo ya kuwa mbunge au upo tayari kuolewa na mwanaume mwenye uwezo wa kuwa na duka la kung’arisha viatu.

Kila uchaguzi una faida na hasara yake.

Wabunge wengi au watu wenye vyeo vya aina hiyo wengi (si wote) hawana muda na familia pia wasafisha viatu hawawezi kuwa wageni rasmi katika sherehe zozote.

Na kama inner drive ya maisha inatofautiana sana kati ya wanandoa basi jiandae kwa frustrations na conflicts.

UNYUMBUFU (flexibility)

Hata uchague mchumba mzuri namna gani au kiasi gani hata hivyo baada ya kuoana kuna tofauti zitajitokeza zinaweza kuwa ndogo ndogo kubwa.

Inaweza kuwa mke akawa anapenda intimacy na mume anapenda privacy, mke anaweza kuwa anawahi kulala na mume anapenda kuchelewa kulala, mke anapenda kula milo 2 kwa siku na mume anapenda milo 3 ya uhakika kwa siku, inawezekana mke hapendi kuongea na mume anapenda kuongea kama MC au mtangazaji wa kutuo cha Radio za FM

Bila kuwa na uwezo wa kubadilika na kuendana na hali mpya (flexible and adaptive) ndoa inaweza kuingia kwenye mitalo ya maji machafu.

“When there are differences in marriage it takes two people who are willing to compromise and adjust.

MAPENZI

Soma hapa

PESA

Soma hapa

=================================

1 comment:

Anonymous said...

HII TAMU KWELIKWELI