"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, April 10, 2010

Ni Zawadi!

Tendo la ndoa ni zawadi (God-given) Binadamu tumepewa katika ndoa.

Hii ina maana kwamba shetani hawezi kutoa chochote zaidi ya kuharibu maana.

Tendo la ndoa ni ubunifu wa Mungu mwenyewe kwa ajili ya mke na mume kuwa mwili mmoja.

Wimbo ulio bora 4: 1-16

Mungu aliumba tendo la ndoa (sex) ili kuwaunganisha mke na mume kiroho na kimwili.

Kutoka kwa mmoja Adamu wakaumbwa wawili (Adam na Eva) na hawa wawili hawakamiliki hadi wawe mmoja tena kupitia tendo la ndoa katika ndoa.

Mwanzo 2:23-24

Mungu aliumba tendo la ndoa lenye mipaka kamili.

Mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa ni uhalibifu na kuna matokeo mabaya kiroho na kimwili.

Mathayo 19:5 -6

Katika tendo la ndoa, wanandoa huweza kunufaika na kuwa kitu kimoja (Mwanzo 2:24), kufarijiana (Mwanzo 24:67), kuijaza dunia (Mwanzo 1:28) pia kwa kujilinda na majaribu ya dunia (1Wakorintho 7:2, 5)

No comments: