"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, April 8, 2010

Niheshimu Nikupende!

Kulia ni Upendo na kushoto ni Heshima!

Katika ndoa si upendo tu bali kuheshimiana.
Mke huhitaji upendo na mume huhitaji heshima.
Niheshimu nami nitakupenda!
Sex kwa mwanaume na love kwa mwanamke ni two way street.
Mwanaume anapoihudumia roho yako (emotional release) ili akubaliwe na mwili wako wewe mwanamke (sexual release) maana yake wewe mwanamke unahitajika kumhudumia mwili wake ili na yeye akupe upendo wake.
Kuheshimiwa au heshima ni hitaji la msingi (primary need) kwa mwanaume kama ilivyo kupendwa au upendo ulivyo hitaji la msingi la mwanamke.
Hii haina maana kwamba mwanaume hahitaji upendo au mwanamke hahitaji kuheshimiwa bali ukimheshimu mwanaume hujiona unampenda na ukimpenda mwanamke hujiona unamheshimu.
Katika utafiti mmoja ambapo wanaume 100 waliulizwa swali kama wangelazimishwa kuchagua moja kati ya mambo mawili (negatives) kuishi nayo au kudumu nayo.
(A) Kuwa mwenye na bila kupendwa duniani
(B) Kuonekana hufai na kutoheshimiwa na kila mtu duniani.
Asilimia 70 walichagua A kwa maana kwamba afadhari mwanaume usipendwe na uwe mpweke kuliko kuonekana hufai na kutoheshimiwa na mtu yeyote duniani.
Hii ina maana roho ya mwanaume inajiona afadhari kutopendwa kuliko kutokuwa respected.
Mwanamke hujisikii vizuri kihisia kutokana na maongezi mazuri na mume wake na kwa kutimiziwa hitaji lake la kuwa karibu na mume wake kwa maongezi hujisikii anapendwa.
Mume akigoma kuongea na mke wake hii ina maana kwamba mke hupata signal kwamba hapendwi na mume wake na pia mume hamjali.
Na mume naye akinyimwa sex na mke wake hupata signal kwamba mke hamjali na hamheshimu katika kumtimizia mahitaji yake.
Ni kama mume analalamika kwamba mke wake hupo unfair kumwambia
Niangalia kwa macho tu na sex hapana
Mke huonesha respect pale anapomtimizia mume wake hitaji la sex na mume huonesha upendo pale anapomtimizia mke wake hitaji ya emotions zake.
Kuna mambo mawili ambayo mke anahitaji kufahamu kuhusu mume wake linapokuja suala la sex.
KWANZA
Linapokuja suala la sex kuna tofauti kubwa kati ya mke na mume.
Mwanaume ni visually oriented, hamu ya mapenzi hupenda kwa kuona.
Akimuona mwanamke mrembo sura ya umbo anakuwa stimulated.
Mwanamke hasisimki kimapenzi kwa kuona kama mwanaume.
PILI
Anahitaji tendo la ndoa (sexual release) kama wewe unavyohitaji upendo (emotional release)
Bila sex anajiona mke hamheshimu na anaanza kuonesha tabia zisizo za kiupendo.
++++++++++++++++++++
Kama ni mwanaume umefika Mahali mke analia kwa sababu ya kukosa upendo unahitaji kujitazama upya na kama ni mwanamke imefika Mahali unamsema mumeo hadi anajiona si lolote au hana tofauti na watoto basi jitazame namna unavyomkose heshima.
Kumbuka maandiko yananena wazi kwamba
Hata hivyo, kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda NAFSI yake mwenyewe, naye mke LAZIMA amheshimu mumewe.
Efeso 5:33

1 comment:

Anonymous said...

Kaka upo sahihi,
Mwanamke anapokufanya ujione wewe na watoto mpo sawa ni kukukosea heshima na kukusemasema (kefyakefya) bila utaratibu kama vile mwanaume hamnazo au ku-critisize kila kitu hata mbele za watu wanaume hujiona ni failures na inabidi uwe mbali na mke kwani ni fedheha na huumiza sana na matokeo yake tunakuwa mbali kihisia (emotional) na mke na matokeo yake mke atajiona hapendwi na mimi mume najiona siheshimiwi na sifai na sina maana. Ni kweli wanawake wanatakiwa kutupa heshima wanaume na sisi tutawapenda kwa kwenda mbele!