"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, April 13, 2010

Shingo Yangu!

SWALI

Kaka Mbilinyi,

Kwanza nashukuru sana kwa hii blog kwani nimejifunza mambo mengi sana kuhusiana na masuala ya mahusiano.

Mimi ni mwanamke mwenye miaka 29 na ni mwaka wangu ya 3 kwenye ndoa hata hivyo nilitaka kuuliza swali lifuatalo kama unaweza kunisaidia.

Mume Wangu anatabia ya kunikaba au kunikwida shingo wakati tukifanya mapenzi (sex) sijajua tabia kama hii ina maana gani.

Nimevumilia kwa muda mrefu hata hivyo imefika Mahali sijisikii kuwa comfortable na hii tabia yake.

Je, ni kitu cha kawaida kwa mwanaume kukukwida shingo wakati wa tendo la ndoa bila kuleta madhala yoyote?

JIBU:

Asante sana kwa swali zuri na pia kupita hapa ili kujifunza tips mbalimbali za maisha ya mahusiano.

Swali lako la msingi linasema

Je, ni kitu cha kawaida kwa mwanaume kukukwida shingo wakati wa tendo la ndoa?

Ukweli ni kwamba linapokuja suala la mapenzi (sex) Binadamu (mke na mume) huonesha tabia nyingi ambazo hushangaza sana (binadamu ni kiumbe wa ajabu sana).


Wapo ambao wakati wa sex hufanya vitendo au kuonesha tabia zifuatazo;

kama vile kufinyana, kuumana kwa meno, kupiga kelele na wengine yowe as if kuna msiba (hadi majirani wanawajua), kupeana matusi ya nguoni, kupigana makofi (kuzabana vibao), kufungana kamba au pingu na kuchapana viboko, wapo wanaume akilifuma kufuli la mke wake hulifakamia na kulinusa kwa dakika kadha na kujisikia raha, wapo ambao hukomalia kunusa kwapa, wengine ni kupeana ahadi kama kununuliana magari au kujengeana ghorofa Mbezi beach (wakiamka asubuhi wanajikuta wapo nyumba ya kupanga manzese jijini Dar es Salaam), sijawasikia hao wa kukwidana shingo na viungo mbalimbali vya mwilini (hii naona inahatarisha maisha zaidi)

Tabia zote hizi wao wanasema ni “to have fun” na kusherehekea mapenzi, hata hivyo inawezekana kwako zisikubalike na kwao zikakubalika.

Usiige!

Napenda ufahamu kwamba kuvumilia tabia au kitu ambacho hukipendi siyo jambo zuri katika uhusiano wa mapenzi kati ya mke na mume, uwe wazi na mweleze ukweli wa vile unajisikia.

Ni muhimu Sana kuweka mipaka kwa vitu ambavyo huvifurahii katika tendo la ndoa na pia muulize mume wako naye ni vitu gani anavipenda na vitu gani havipendi.

Otherwise, nilitakiwa kumuuliza huyo mume wako huwa anasukumwa na kitu gani hadi anakukwida wakati sensitive kama huo au ndo kuzidiwa na mahaba!

Naamini umeridhika!

No comments: