"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, April 14, 2010

Sikiliza tu!

Wengine kazi kuwasikiliza!

Ili Mke awe available kwa mume kimwili na kiroho inampasa mume awe sifa zifuatazo:

Ukaribu (intimate), uwazi katika mambo yake, anayeeleweka, mtu wa amani, anayempa uhakika mke kwamba ni yeye peke yake ndiye anapendwa na mume wake na pia kumpa uhakika kwamba yeye ni mwanamke mwenye sifa anazozipenda kimwili (beauty) na kiroho.

Je, unawezaje kuwa mume ambaye mke anakuelewa (understanding)?

Ili mke akuelewe mume unahitaji kutumia secret weapon ya sikio lako.

Kumsikiliza tu mke huweza kuonesha kwake kwamba umemuelewa kuliko hata kabla hajamaliza kuongea wewe unamkatiza na kusema ulikuwa unajua anataka kusema kitu gani.

“We have two ears and one mouth so that we can listen twice as much as we speak”.

Tofauti kubwa ya mwanamke na mwanaume ni kwamba mwanaume kawaida yupo wired kusikilizwa na si kusikiliza, na mara nyingi mwanaume hupenda kutatua tatizo au matatizo au kutoa jibu kwa ajili ya tatizo lolote, hivyo anapoongea na mke wake kwa kutomfahamu anakuwa na haraka ya kutaka kutoa majibu badala ya kusikiliza tu.

Narudia tena;

Si mara zote mwanamke anapouliza swali au kukwambia kitu anahitaji majibu, mara nyingi anakuwa katika harakati ya kujihusanisha (connection) na wewe na anachahitaji ni sikio lako tu na si namna ya kupata majibu.

Unachotakiwa kufanya ni kumsikiliza na kushiriki katika kuzungumzia hiyo shida yake na kuliona kama tatizo lenu wote.

“The first duty of love is to listen”.

Mwanamke huhitaji mtu wa kumsikiliza tu na sikio lako wewe mume ndilo analihitaji na si uwezo wako wa kutatua tatizo.

Ukimsikiliza, atajisikia vizuri tofauti na ukirukia kukatiza kile anaongea au kuanza kupendekeza solutions kwa kile anakwambia.

“Don’t solve your wife’s problems but just listen, you will show empathy and understanding”

Wanaume kujitahidi kutoa solutions za kile mke anaongea au hata kukatiza kile anaongea kwa mume kujifanya anajua mke alitoka kuongea kitu gani ni moja ya matatizo sugu ya kwenye ndoa.

Hata kama wewe ni mwanaume maarufu kutatua matatizo ya wanaume wenzako bado ukiwa na mke wako unatakiwa kumsikiliza tu na sikio lako hadi aridhike.

“Listening is a magnetic and strange thing, a creative force.

The men who listen to us are the ones we move towards them.

When we are listened to, it creates us, makes us unfold and expand.”

By women.

No comments: