"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, April 13, 2010

Ukizima Moja, Zote zinazima!


Mwanaume na mwanamke wapo tofauti zaidi kuliko kufanana na hivyo ndivyo walivyo, kukataa haiwezi kubadilisha ukweli.
Mwanamke na mwanaume husikia na kuona vitu kwa utofauti mkubwa acha suala la chumbani.
Sasa fikiria mume na mke ni electric circuit, na circuit ya kwanza ina taa (bulb) 3,000 na mfumo wake ni kwamba ukizima bulb moja unasababisha bulb zote 2,999 kuzima.
Na circuit ya pili ina bulb 3,000 pia na ipo designed kwa namna ambayo ukizima bulb moja, zingine zinaendelea kuwaka, ukizima bulb 2,000 bado zilizobaki 1,000 zitaendelea kuwaka.
Mwanamke ni sawa na electric circuit ya kwanza kwa maana kwamba kukiwa na conflict eneo moja la ndoa au maisha mwanamke hufunga system nzima ya mwili wake (bulb moja ikizima zote zinazima) kwani feelings za mwanamke zimeunganishwa (integrated system) na kuingiliana mwili, roho na nafsi, hii ina maana akiumia roho na mwili unaumia na nafsi inakuwa imeumia.
Hii ina maana mume akifanya jambo moja linalomkera mke; mke atajisikia hapendwi na mume hamjali (bulb zote zitazima) hadi matengenezo ya mwanaume kuwa wazi na karibu ndipo anaweza kurudi kwenye hali ya kawaida na si kuwambia let’s forget it eti ndo umemalizana naye.
Kumbuka somo la spaghetti
If she is in a battle with him in one area, she is at war with him in all areas
Kila mwanaume na afahamu kwamba:
Kama mke anajisikia kuna tatizo katika eneo moja la maisha (kuumizwa, upweke, kukataliwa, kuchoka, mawazo, kukosa upendo, kutoheshimiwa, hasira nk) hukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.
“When her spirit is crushed, her body is not available”
Wanaume huweza operate kama vile hawana feelings au tatizo, hata wanawake hulalamika kuhusu hili.
Kwani yeye ikizima bulb moja bado zinazobaki hupendelea kuwaka, hata ukizima zingine nyingi bado bulb zilizosalia hupendelea kuwaka.
Hii ina maana mwanaume ni mfano wa box kiasi kwamba hawezi kuhusanisha tatizo moja na lingine kwake mwili ni kitu kingine, roho ni kitu kingine na nafasi ni kitu kingine.
Ndiyo maana mwanaume anaweza kuwa katika mgogoro katika eneo moja la maisha na asiathirike chochote.
Ndiyo maana kukiwa na mgogoro kati ya mke na mume bado mume anaweza kuhitaji tendo la ndoa bila tatizo na akajisikia vizuri tu kushiriki.
Tutaendelea........

2 comments:

Anonymous said...

Hi!
Ni ukweli mtupu umenena kaka, halafu umenifumbua masikio kwa nini unajua sisi wengine tumeolewa na wanaume ambao ni wajuaji kila kitu anajua hata tukiwa mbele za watu.

Sasa fikiria ndio ndani weeeee ndio mjuaji zaidi ya wa nje,nimegundua nikigombana na King mimi hata kumsalimu tabu tena nimemnunia hapo toka asbh lakini tukiingia 6*6 anaanza mhhhh!

kumbe ndivyo walivyo nimegundua na jinsi ya kuhendo hiyo hali very thx!Mama P!

Lazarus Mbilinyi said...

Mama P,

Asante kwa ujumbe wako na zaidi kwamba umeelewa wanaume tulivyo simple, migogogoro ya hapa na pale katika ndoa wakati mwingine haituumizi sana kama ninyi wanawake.
Wakati mwingine tukipishana kidogo (conflict) asubuhi tunapoondoka; wewe mwanamke utawaza siku nzima zaidi ya mara 20 huko kazini na kuchambuachambua na kujiuliza hivi ilikuwaje hadi mume wangu akafanya hivi na vile na siku nzima kwako inakuwa balaa, mawazo matupu na unajiandaa ili mkirudi jioni ikiwezekana mmalizane.
Hata hivyo mume wako ni kinyume chake kwani yeye akienda kazini ule mgogoro wa asubuhi anauachana hukohuko nyumbani na akienda kazini yeye anafikiria kazi na hakumbuki hata kidogo na akirudi nyumbani jioni anakushangaa bado unakumbuka kitu cha asubuhi na anakwambia "lets forget it" kirahisi tu wakati wewe bulb zote zimezima na usichangae usiku huohuo anakupapasa mgongoni kuashiria anataka...... wakati wewe bado bulb zote zimezima na mwili bado haupo available hadi mgogoro ujadiliwe na kumalizwa kwa ukaribu na uwazi.
Badala yake wewe utaanza kubehave bila heshima (without respect) bila kujua na utaona yeye amekuonesha unloving behaviour wakati na yeye atajiona huna respect na matokeo yake atakuona huna heshima kwa kutotambua mahitaji yake.
Inaweza kuwa vuta nikuvute wiki nzima kama wote hamna Mungu ndani yenu kwani inahitaji mwanandoa mmoja aliyekomaa kukubali kwamba nimekukosea mwenzange samahani na nisamehe kwa upendo na heshima.

Upendo na Heshima daima!