"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, April 16, 2010

Umenifanya Mpya???


Je utaridhika kama mchumba wako;
Ni mkorofi kwa wahudumu wa hoteli (waiters),
Kila siku ni kugombana na boss na anamwambia boss ndiye mwenye matatizo,
Mkorofi kwa watoto (mean)
Anapoendesha gari ni mkorofi kwa madereva wengine (anawaka)
Hana uhusiano mzuri na familia yake,
Aliwahi kupewa talaka?
Aliwahi kuwa mwingi wa habari,
Anawadanganya rafiki zake na wewe upo akiogopa kuleta mgogoro au kuumia moyoni,
Anasifika kwa kukalia (controlling) watu,
Kumbuka:
“History repeats itself”
Na ukisikia binti au kaka anakwambia maneno yafuatayo be very careful na ikiwezekana tumia akili kuliko moyo.
“Sijawahi kujisikia kwenye mapenzi (love) kama tulivyo mimi na wewe, sijawahi kupata mtu anayenifanya nijisikia vizuri kama wewe unavyonifanya nijisikia na hakuna mtu amewahi kunielewa kama unavyonielewa wewe”
Mtu anayeongea hivi kama aliwahi kupendwa na kuwa kwenye mahusiano inabidi uwe makini sana na haya maneno it may be misleading.
Hii ina maana anakwambia kwamba
Sitafanya kama nilivyofanya huko nyuma, nilikuwa ovyo na sikuwa nampenda kikwelikweli huyo wa kwanza
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
Wazo kwamba upendo wa kweli (true love) huweza kumbadilisha mtu kutokana na patterns zake za zamani kimuujiza si kweli mara zote hasa kama feelings zimetangulia zaidi ya akili.
Baada ya mwaka mmoja historia hujirudia na unaweza kuwa sawa na wale amekwambia hawajaweza kufanya ajisikia anapendwa.
Ndipo yatakupata ya kukupata!
Ni hatari sana kwako kukubali kwamba amekupenda kiasi cha kuweza kubadilika asili yake kama kweli huko nyuma alipendwa, si muda mrefu unaweza kukutana na full script ya maisha yake ya nyuma ndipo utakutana uso kwa uso na mbwa mwitu ambaye ulidhani ni kondoo.
Ili kumfahamu mtu vizuri ni muhimu kutafuta habari kamili kuhusu yeye kwa kuruhusu MUDA ufanye kazi yake.
Mwangalie tabia yake na maisha yake kwa mtazamo wa mtu mwingine na si wewe.
Kama kuna complaints kutokana na mahusiano yake ya zamani basi fanyia kazi.
Sikiliza ndugu zake na familia yake na marafiki zake kuhusiana na kila hadithi unaambiwa kuhusu yeye, nzuri na mbaya.
“An apple doesn’t fall far from the tree”

No comments: