"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, April 5, 2010

Unamaratajio kiasi gani?

Wana matarajio makubwa kwa ndoa!

Uamuzi wa maana kuliko uamuzi wowote duniani ambao mtu anatakiwa kuufanya ni ule wa kumkubali Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako.

Huu uamuzi hudhihirisha ubora wa maisha yako hapa duniani na mbinguni.

Uamuzi wa pili na wa maana sana ni ule wa kuchagua yule utaoana naye hapa duniani na uamuzi huu unachangia sana furaha yao au huzuni yako katika maisha ya hapa duniani.

Inawezekana upo katika mchakato wa kutafuta nani uoane naye, au inawezekana umeridhika na yule umeoana naye na mnaishi maisha safi ya ndoa (hongera sana) au inawezekana unatamani kama ungempata mwingine kwani yule umeoana naye anakupa wakati mgumu au inawezekana upo mwenyewe baada ya kuumizwa kwenye mahusiano na sasa unaona mahusiano hayana maana yoyote kwako.

Ukiwauliza wengi waliooana sababu zilizopelekea kuoana wanaweza kukwambia walioana kwa sababu;

Walipendana tu na kila mmoja alivutiwa na mwenzake (kimwili),

Kwa sababu rafiki zao walikuwa wameolewa au kuoa,

Walihitaji ulinzi wa kuwa na mtu,

Kwa sababu kila mtu anaoa na kuolewa,

Kwa sababu wazazi waliwaambia ni wakati wa kuoa

Au waliona kuoana ndilo jambo sahihi.

Nk.

Hata hivyo Baadhi ya sababu hapo juu si za msingi sana katika kuoana.

Hebu tuangalia matarajio ya mwanamke kuhusiana na mwanaume katika ndoa kwa kufuata umri.

MIAKA 18 – 29

Mwanamke huangalia mwanaume mwenye sifa za uzuri, moto wa mapenzi na sifa nyingi ambazo ni illusions.

MIAKA 30 – 39

Mara nyingi wanawake wenye huu umri wakiwa kwenye ndoa hupatwa na mshangao wa mwanaume waliyenaye namna asivyofanana na matarajio walikuwa nayo wakati wa kuoana.

MIAKA 40 – 49

Wanawake wa umri huu hujikuta kile walikuwa wanakihofia wakati wa umri wa miaka 30 kimeshapita.

MIAKA 50 – 59

Wanawake wa umri huu hujiuzuru (resign) Kuamini kwamba waume zao wanaweza kubadilika.

MIAKA 60+

Wanawake wa umri huu wanafahamu kwamba kazi ya kuwabadilisha waume zao si yao na kufanya hivyo ni kupoteza muda na wamejifunza namna ya kuyafanya maisha yawe ya furaha na kwamba furaha huanza na wao kwanza na si kutegemea mume kumpa furaha ya maisha.

“The older the woman, the less she expects from her marriage"

No comments: