"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, April 7, 2010

Usijidanganye!

Sex ni issue inayosumbua sana wanaume na wanawake katika ndoa.

Mwanamke katika ndoa huhitaji intimacy & affection ili ajihusishe na tendo la ndoa wakati mwanaume anahitaji tendo la ndoa na hana mpango na masuala la intimacy & affections tu.

Wapo wanawake ambao piga ua wamejipangia kwamba bila kuwa karibu na mimi kimapenzi sahau kuhusu sex kwani ni kama kuutumia mwili wangu.

Ukweli unaouma ni kwamba wanaume wengi wanaotoka nje ya ndoa (affair, cheat, chepuka, tembea nk) hufanya hivyo kwa sababu wananyimwa katika ndoa zao.

Mwanaume anayetoka nje mara zote ndiye anayebeba lawama na dhambi.

Yeye ndiye victim wa tatizo zima hata kama mke wake alihusika katika kutengeneza mazingira ya mwanaume kuchepuka.

Mwanamke huhitaji love ili kujisikia vizuri emotionally na mwanaume naye huhitaji respect kwa mke kutii hitaji lake la mwili (sex) ili kujisikia yupo mke anamtii.

Wapo wanaume ambao kwa kunyimwa hitaji lao la msingi la tendo la ndoa ndani ya ndoa zao huwa hawaoni shida au tatizo kupoteza familia, biashara, uongozi, hadhi (reputation), uhusiano na Mungu wake au kuaminiwa na jamii kwa kwenda kutimiziwa na mwanamke mwingine nje ya ndoa.

Unaweza kusoma hapa pia

Inaweza kuwa bado hujanielewa naongea kitu gani hata hivyo umeshaona wanaume wanatoka na kuacha wake zao wazuri na kwenda kutembea na wanawake ovyo ambao kila mtu hushangaa na ni wanaume wazito kwenye jamii.

Ukweli ni kwamba hitaji la tendo la ndoa kwa mwanaume ni kubwa kuliko unavyofikiria.

Inawezekana wewe ni mwanamke ambae mume wako ni mtumishi wa Mungu au mume wako ana cheo au wadhifa au anapenda sana familia na kwa kuwa siku za karibuni umeoana hakutumizii hitaji lako la kupendwa basi na wewe umeamua kumnyima tendo la ndoa hadi abadilike ndipo na wewe umpe mwili wako kwani una amini kwa namna alivyo hawezi kutoka!

Usijidanganye!

Hujasikia watumishi wa Mungu ambao wameanguka?

Hata kama huna mood kinakushinda nini kutumia dakika tano tu kumpa hitaji lake na awe happy na wewe all the time?

Katika kushauriana na wanawake wengi ambao waume zao hutoka nje wengi huruka na kukiri kwamba wanaume zao ni tamaa na shetani ndo amewatuma kufanya vitu kama hivyo hata hivyo mwanamke mmoja alikiri kwamba ni kweli ajisikia vibaya sana kwamba alihusika katika kusababisha mume wake kutoka nje kwani yeye alikuwa anajihusisha sana na watoto wake na kazi na hakupenda kabisa kumpe sex mume wake kwa muda mrefu.

Mume mmoja alilalamika kwamba:

Ni kweli simlaumu mke wangu kwa mimi kutoka nje ila hawezi kutoka msafi katika hili kwani alinifanya kujiona mimi ni failure wa kila kitu nyumbani mwetu na sikuruhusiwa hata kumgusa miezi na miezi.

Kama angenitii na kunipa hitaji langu la sex basi nisingetoka kwani mwanamke niliyetembea naye alinifanya nikisikia vizuri muda wote na kila alivyozidi kuniambia mimi ni mwanaume mzuri nilizidi kuwa karibu na huyo mwanamke na sikuwa na lengo la sex ila kutokana na respect aliyonipa ilifika mahali nikaamua kutembea naye hata kama sura na umbo lake linafanana na chimpanzee”.

Soma barua ya mwanaume mwingine hapa

Mwanaume anahitaji sexual release kama mwanamke anavyohitaji emotional release.

Bila tendo la ndoa mwanaume hujiona hujamtii au kumpa respect na moja kwa moja huanza kuwa na tabia zisizo za upendo kwa mwanamke.

Wanawake wengi huwa na ndoto za kuhakikisha baada ya kuolewa mahitaji yao ya emotions yanatimizwa na waume zao hata hivyo wao wenyewe hujisahau kuwapa waume zao mahitaji yao ya tendo la ndoa na automatically inakuwa ngumu kwa mwanamke mwenyewe kutimiziwa mahitaji yake ya emotions.

Namna mwanaume aliumbwa (anatomy & design) ni tofauti na mwanamke ndiyo sababu mwanaume anapenda tendo la ndoa na linampa satisfactions ambazo humfanya kukumchangamkia na kuchakarika kuhakikisha na yeye anamtimizia aliyemtimizia.

Wewe mwanamke unapenda tendo la ndoa pale mwanaume anapokuwa karibu kimapenzi na wewe (affection & intimacy) hata hivyo kwa mwanaume ni reverse gear, tendo la ndoa ndilo humfanya mwanaume kuwa karibu na mwanamke.

KUMBUKA

Shetani siku zote hufanya kila analoweza kuhakikisha wachumba wanajiingiza katika sex kabla ya ndoa na pia hufanya kila kitu analoweza kuhakikisha anawazuia wanandoa kuwa na sex katika ndoa yao.

Jiangalie usiwe mmoja wao!

Kwa maelezo zaidi soma hapa

6 comments:

Anonymous said...

Kaka Lazarus, tunashukuru kwa kutuelimisha umuhimu wa sisi wanawake kutokuwa wanyimi wa sex kwa waume zetu ila wakati mwingine ni kweli wanaume wanaitumia vibaya ile sentensi ya kuwa wao ni vichwa au ndio watafutaji wakuu ktk familia. Unakuta mwanamke unafanya kila kitu mume anaangalia tuu na kweli unakuwa umechoka sana pamoja na kwamba unapewa kila kitu unachohitaji lakini uchovu wa mwili unahitaji mume ambaye anaona na anajua kwamba kumsaidia mke ni kuongeza uwezekano wa kupata sex, kwani hata mke akiona anapendwa na anasaidiwa nadhani tofauti na mabadiliko yatakuwepo.

Mungu akubariki kaka.

Anonymous said...

Kaka Lazarus, tunashukuru kwa kutuelimisha umuhimu wa sisi wanawake kutokuwa wanyimi wa sex kwa waume zetu ila wakati mwingine ni kweli wanaume wanaitumia vibaya ile sentensi ya kuwa wao ni vichwa au ndio watafutaji wakuu ktk familia. Unakuta mwanamke unafanya kila kitu mume anaangalia tuu na kweli unakuwa umechoka sana pamoja na kwamba unapewa kila kitu unachohitaji lakini uchovu wa mwili unahitaji mume ambaye anaona na anajua kwamba kumsaidia mke ni kuongeza uwezekano wa kupata sex, kwani hata mke akiona anapendwa na anasaidiwa nadhani tofauti na mabadiliko yatakuwepo.

Mungu akubariki kaka.

Anonymous said...

Hapa kaka nashindwa kukuamini maana wapo wanawake wengi tu tena sana wanaolalalmiakia waume zao ndo wanawabania ndoa, na tena unakuta mama anajitahidi kuvuta vuta lakini mzee wapi anamsukumia kule huu ni ukweli, ongea na wanawake, wapo wengi sana wenye shida hii.

Lazarus Mbilinyi said...

Kimsingi siri kubwa ya ndoa inapatikana Efeso 5:33 Hata hivyo, kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake mwenyewe, naye mke lazima amheshimu mumewe.

Hii ina maana hitaji la msingi la mwanamke ni Upendo, kupendwa (mume kuwa karibu kwa maongezi, kusaidiana kazi, zawadi, kukumbatiwa, busu nk) na ndipo hufunguka kuwa tayari kwa tendo la ndoa.
Hitaji la msingi la mwanaume ni heshima, kuheshimiwa (respect) na hili halifundishwi wala kuongelewa na washauri au watu wanaofundisha mambo ya ndoa. Mwanamke anayemheshimu mume wake kwa namna anavyoongea (unaongea hadi anajiskia si failure katika maisha, unaongea na yeye kujisikia ni hero) basi atakupenda.

Ni kweli wanaume wengi hukaa tu huku mwanamke anahangaika na kazi za nyumbani wakati wote walikuwa kazini mchana kutwa, inawezekana hakusaidii kazi kwa sababu huna humheshimu na unaona hakupendi.

Ni kweli pia wapo wanaume (wajinga) wanaotumia lungu la kuwa kichwa cha nyumba na kushindwa kumpa mke upendo anaostahili na matokeo yake mwanamke anakuwa mtumwa na hawezi hata kushiriki tendo la ndoa.
Jambo la msingi ni kuhakikisha kama mke unajitahidi kuhakikisha unampa mume heshima au unamheshimu na mume asijione ni failure au hana lolote na chunga sana maneno unayoongea kwa mume wako.
Wanawake wa kanisani wanajua sana kuwapenda waume zao tatizo moja wapo ambao bado suala la kumheshimu mume limewapita pembeni.

Mungu atusaidie kila mmoja kufahamu nafasi yake kwa mume kumpenda mke na mke kumheshimu mume.

Lazarus Mbilinyi said...

Kuhusu wanaume ambao hawana hamu ya tendo la ndoa ni kweli wapo na wanawapa wakati mgumu sana wake zao na kwa mtazamo wa mwanamke suala haliwi tendo la ndoa tu bali anaweza kuwaza na kufika mbali zaidi kama vile labda hanipendi au labda nina kasoro au sina mvuto au amepata mwanamke mwingine nje.

Kuna moja ya tatu ya wanaume duniani wana kiwango kidogo cha homoni zinazohusika na kuongea hamu ya sex na pia kuna moja ya tatu ya wanawake duniani wana kiwango kikubwa cha homoni kama wanaume.

Jambo la msingi ni kwa mke na mume kukaa pamoja na kujadili tatizo na ikiwezekana kuwaona washauri ili kila mmoja aridhike na ndoa kwani kuna uhusiano mkubwa sana kati ya tendo la ndoa na kuridhika kwa ndoa kwa ujumla.

Upendo daima

Anonymous said...

ACHENI UNYIMI NA NYIE WANAWAKE, KWANI HIYO NI CHUNVI TUSEME INAISHA?. BURUDISHENI WAUME ZENU NAO WATAWABURUDISHA.