"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, April 29, 2010

Usimwachie yeye tu

Kwa kuwa mume huwa na hitaji kubwa la sex katika ndoa mara nyingi (siyo mara zote), hii husababisha sex kuwa suala la kimwili (physical) kuliko mke unavyohitaji.

Wanawake hukiri kwamba wanapozungumzia sex ni pamoja na kukumbatiwa (hugs &cuddling), busu na kushikana shikana kunakupelekea kuwa na maandalizi ya kutosha (foreplay) kuliko waume zao wanavyofanya yaani kukimbilia down there na kumaliza kazi.

Jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba wanandoa wengi wakiwa chumbani wanaume ndiyo huachiwa usukani wa kuendesha suala zima la mahaba na matokeo yake wake zao huishia kutoridhishwa.

Kumbuka sex inapokuwa kwa ajili yake (mwanaume) basi huishia kuwa ni “routine” na mwisho huwa ni “boring

Kumwachia mwanaume (mume) kila kitu chumbani ni sababu mojawapo ya mwanamke (mke) kutoridhika kwani yeye si mwanamke ajue nini unahitaji kwa wakati huo na zaidi device zake zinafanya kazi tofauti na mwanamke.

Hivyo kama wewe ni mwanamke ambaye umemwachia mume wako jukumu la kuongoza yote mnayofanya mkiwa chumbani na unajiona ni kweli haridhiki au huridhishwi inavyotakiwa basi anza sasa na wewe kuhakikisha unasaidiana naye kuweka mambo sawa.

‘Men read newspapers, not minds

Bottom line ni kwamba mwanamke yeyote anayekuwa mbunifu na anayependa kuimarisha masuala la sex; mume humpokea kwa mikono miwili kwani sex ni hitaji lake muhimu katika kukufanya awe karibu na mke wake.

Hivyo tumia hiyo opportunity!

4 comments:

Anonymous said...

Mmm kaka Mbilinyi hii ni ngumu kidogo, nilikuwa na shida ya kutoridhishwa kimapenzi, nikaomba ushauri kwa watu wenye busara ila matokeo yake ni kwamba mume wangu aliniambia mimi nimeanza tabia za uhuni sasa nimebaki kumwachia yeye gwaride zima.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Pole sana,
Ingawa hujafafanua approach uliyotumia kuingiza topic mpya ya wewe kuhusika katika suala zima la kuwa wazi katika kusherehekea faragha na mume wako,
Si unajua wote wanaume na wanawake kila gender ilitoka sayari tofauti hivyo kuna tofauti kubwa sana namna na kuwakilisha ujumbe na namna mwingine anavyoupokea. Bila kujua hiyo siri basi unaweza kuishia kuambiwa umeanza uhuni (tena hiyo afadhari wengine huzabwa makofi kabisa)
Namna ya kuufikisha ujumbe kwa mwanaume ni tofauti sana na unavyoongea na mwanamke mwenzako, naamini ukiimarisha namna ya kufikisha ujumbe anaweza kubadilika na ukawa na uwezo mkubwa wa kupendekeza gwaride liweje.

Ningefurahi sana kufahamu namna uliufikisha ujumbe wako!

Upendo daima!

Anonymous said...

habari ya kazi kaka mbilinyi,kupitia blog hii nimejifunza mambo mengi sana ila nimeupenda huu ujumbe ,mwanaume husoma magazeti hasomi mawazo ya mkewe
hii imenifanya nifikirie mbali sana maana sisi wanawake huwa tunaamini mwanaume ataelewa tu nini mimi nawaza
keep it up br

Lazarus Mbilinyi said...

Ni kweli,
Hata kama tunajitahidi sana kusoma mawazo yenu bado tafsiri tunayopata ni nyingine.
Na ninyi huwa mnatuchanganya zaidi pale mnapodhani sisi wanaume tutafahamu kile kimo kwenye mawazo hatuna hiyo talent sisi tunasoma magazeti, ukitaka kitu sema tu kwani ukidhania nitakuelewa kwa kukusoma kimawazo sahau kabisa.
Pia sisi si watu wa emotions ndiyo maana hata kama unaona mume wako anaonesha leo hayupo sawa na ukamuuliza "vipi kuna tatizo gani?" atakwambia "hakuna tatizo" utaendelea kumsuta hadi anakasirika kwani kuna wakati hatujijui! nhahahaha

Upendo daima