"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, April 19, 2010

Wanawapata Wapi?

Wanajadili lina watamaliza Project ili Boss akabidhiwe!

Je, mwanaume anayetoka kwenye nje (cheating, affair, astray) humpata wapi mwanamke ambaye anatembea naye (sex) na hata kuhatarisha ndoa yako?

Tafiti nyingi zinaonesha kwamba mfumo wa maisha umebadilika sana, sasa wanaume kwa wanaume wote wanashiriki katika kazi ambayo hapo miaka ya 47 ni wanaume tu au wanawake tu waliruhusiwa kufanya, modern society imetengeneza mazingira mapya ambapo wanawake na wanaume sasa wanashinda au tumia muda mrefu na watu wengine wa jinsi tofauti kuliko mke au mume.

Wanaume wengi wanaotoka nje ya ndoa zao mara nyingi hukutana na mwanamke mwingine sehemu zifuatazo

1. KAZINI/OFISINI

Kama tulivyoona huko nyuma kwamba cheating zote hazianzi kwa kuwa wahusika walikuwa na lengo la kufanya sex bali ni urafiki wa kawaida au kukosa hisia muhimu katika ndoa zao na kwenda kujisikia vizuri kwa hao wa nje.

Kazini ndipo Mahali ambapo inawezekana mume wako anaweza kumpata mwanamke wa ku-cheat.

Kama mwanamke unatakiwa kuwa makini na wanawake ambao anashinda nao kazini kwake na wakati mwingine kabla ya affair unaweza kumsikia akimtajataja mwanamke fulani huko ofisini kwao, uwe makini na hilo jina ulitunze kwenye hard disk yako.

Pia chunguza ratiba zake za kuchelewa kurudi nyumbani kutokana na project au conference anazohudhuria na je alikuwa na huyo mwanamke.

Uwe mzuri katika kuzungumza naye kuhusiana na kazi yake, office politics zao na hata mizaha waliyonayo huko ofisini.

Wapo wanawake ni waoga hata huogopa kwenda ofisini kwa waume zao; kazi kwelikweli!

2. KWENYE SHUGHULI ANAZOZIPENDA

Kama mume wako anaipenda activity fulani (hobbies, interests) na kutumia muda mwingi na wewe huna mpango nayo/nazo basi inabidi ufikiria upya.

Je, anaondoka nyumbani na kwenda kuangalia au kuchezea soka, jogging, golf, gym, kwaya, kazi za kujitolea nk?

Je, akikutana na mwanamke ambaye anapenda kila na yeye anapenda unadhani kitatokea kitu gani?

Wanaume wengi ambao walishafanya cheating, wanakiri kwamba kuwaacha peke yao wakikata mbuga katika ulimwengu wa interest na hobbies (passion) zao bila mke kuwepo ni risk kubwa sana kwani akimpata mwanamke ambaye anapenda kufanya kile na yeye anapenda uwezekano wa Kuzaliwa uhusiano mpya ni mkubwa sana.

Kuwa mwenyewe anaweza kujikuta Anafanya connection na mwanamke mwingine na hiyo inaweza kuwa hatua moja kuelekea kwenye affair.


Swali la kujiuliza wewe mwanamke ni hili:

Kuna shida gani kwa wewe kujifunza kile anapenda na hatimaye kwenda pamoja na kufurahia kile mume wako anafurahi kufanya?

Kuna shida gani kama mkienda wote kwenye ile shughuli anaipenda?

Usipokuwa naye ili umsaidie kutoa energy basi atampata mwingine wa kumsaidia kutoa hiyo energy.

Pia si busara kumwambia asiende eti kwa sababu wewe huenda, muhimu ni wewe kuwa active kwa kuwa naye katika hobbies zake kiasi cha kuweka uhusiano mzuri na kujenga urafiki.

3. WANAWAKE WANAOMZUNGUKA

Hii inaweza kuwa ni wale ambao mnafahamiana kwenye backyard yenu, majirani, kanisani, chama, shughuli za kujitolea na hata mtaa na eneo mnaloishi linaweza kuwa ni sehemu muhimu kwa mume wako kumpata mwanamke.

4. INTERNET

Wengi wanasema internet ni tatizo kubwa sana kwa wanaume kupata wanawake wambao hufanya cheating nao hata hivyo tafiti nyingi zinaonesha ni kweli anaweza kumpata mwanamke wa kuongea naye na uwezekano wa cheating (sex) si sawa na ule wa kazini au kwenye interest zake au majirani.

2 comments:

Anonymous said...

kaka mbilinyi Bwana asifiwe sana.unasema mwanamke awe anatembelea ofisini kwa mme wake sometime,na kujifunza kile anapenda.swali langu ni hili je kama ni mfanyabiashara na mara kwa mara anasafiri one week au two weeks utafanyeje na nyumbani una famili watoto huwezi kufuatana naye hapo mwanamke afanye nini?2 na kwa wanawake wanaotoka nje nao huwa inakuwaje na tatizo ni nini?Ubarikiwe na Bwana Ek.

Lazarus Mbilinyi said...

Hello EK,

Asante sana kwa swali zuri.
Kama ni mfanyabiashara na kila mara anasafiri naamini jambo la msingi kwanza ni wewe kuwa kitu kimoja na yeye katika biashara yaani uipende hiyo biashara na kujifunza na kufahamu vitu vya msingi ili umsaidie kutimiza malengo yake katika hiyo biashara, then siku nyingina na wewe unaweza kusafiri pamoja naye (sometimes not all the time)
Pia si hekima wala busara kumwambia asisafiri eti kwa sababu haendi na wewe. Jambo la maana ni wewe kuwa na ufahamu kuhusu malengo ya hiyo biashana na umsaidie kufanikisha hayo malengo ndipo atajisikia kweli unampa respect na kwamba mpo pamoja na badala ya kuwa na yule mwanamke atajiona wewe tayari umejaza nafasi kwani unapenda kile anapenda.

Ubarikiwe