"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, April 6, 2010

Wivu Mwingine!

Alipofungua drawer akaikuta barua................

Wivu huua upendo katika mahusiano.

Kuna usemi wa kingereza kwamba;

The more possessive you’re the more love you demand and the less love you receive.

The more freedom you give, the less love you demand and the more love you receive.

Wivu ni mkatili kama kuzimu (Wimbo ulio bora 8:6)

MFANO WA KWELI

Ryan ni mwanaume ambaye alikuwa na wivu mkubwa kwa mke wake Amanda.

Kila kitu ambacho Amanda alifanya Ryan alikuwa suspicious.

Amanda anapoongea na simu mume wake Ryan huacha kile alikuwa anafanya na kuelekeza masikio kusikia mkewe anaongea na nani na anaongea nini na baada ya kumaliza simu huulizwa na kama ni mwanaume basi vita kuu ya tatu ya dunia huanza.

Akienda mahali kama si kufuatwa kwa nyuma basi akirudi lazima afanyiwe drill kujieleza alienda kwa nani, na nani na kwa nini.

Siku moja Amanda hakuwepo nyumbani na huyu mwanaume mwenye wivu wa kupindukia akafanya pekua pekua chumbani kwao na mke wake na akaikuta barua ya mapenzi kwenye droo ya kabati aliyoandikiwa Amanda, Ryan bila kuangalia tarehe wala nani aliiandika alipata wivu ghafla, hasira zikampanda kama kifaru, akawa anawaka kwani alihisi mke wake kapata bwana wa nje.

Amanda alivyofika nyumbani tu alimdaka kwa mangumi na mateke na kumpiga kwa hasira na kumjeruhi vibaya hadi akapoteza fahamu, majirani wakapiga simu polisi na Ryan akakamatwa na baadae mahakamani na mwisho akaenda Jela miaka 5.

Katika kupeleleza polisi waligundua kwamba ile barua iliandikwa na yeye mwenyewe Ryan miaka 15 iliyopita wakati yeye mwenyewe Ryan alikuwa anamchumbia Amanda mke wake na Amanda alikuwa ameitunza ile barua kama kumbukumbu ya mapenzi yao.

Tatizo ni kwamba Amanda hakupewa muda wa kujitetea au kuelezea ile barua ya nani.

The grass is greener on the other side of the fence only when you have bothered building fences.

Do you think fences make good neighbours?

No comments: