"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, May 31, 2010

Nitamwelezaje?

SWALI:

Kaka Mbilinyi kwa miaka 10 nimekuwa najizuia kuwa wazi kimapenzi kwa mume wangu kwa kuwa wakati mtoto nilikumbana na kudhalilishwa kimapenzi kitu ambacho hunifanya nisijiweke katika mazingira ya kuumizwa tena.

Sikupenda kuongelea sex wala kufanya mapenzi na mume wangu isipokuwa tu pale nilipojilazimisha kwa kuwa nilitamani kuwa na watoto (Mungu ametujalia kupata watoto wawili).

Baada ya kusoma makala mbalimbali kwenye blog yako nimejikuta naumia sana kwa namna nimekuwa namnyima mume wangu haki yake kwangu na naumia zaidi kwa kuwa amenipenda miaka yote acha historia ngumu ya maisha yangu.

Je, nawezaje sasa kuanza upya kushiriki tendo la ndoa bila kukumbuka za yale niliyopitia wakati mtoto na je, naweza vipi kumueleza mume wangu ambaye amekuwa anaonesha upendo mkubwa kwangu na nimekuwa namnyima haki yake kwa muda mrefu?

Dada Jane

JIBU:

Dada Jane kwanza hongera sana kwa ujasiri wa kutaka kurekebisha mambo sasa, kutokana na uzoefu wa mambo hatari uliyopitia na kustahimili ni kweli wewe ni mama jasiri kuanza kuyazungumzia tena ili kupata majibu ya kudumu na kuondoa mzizi wa jambo lenyewe.

Ndiyo maana mume wako anakupenda sana naamini ni kwa sababu wewe ni mwanamke mwenye moyo au mtazamo mzuri wa maisha hasa kutoridhika na zaidi kuhakikisha unaoleta tofauti.

Utaanzeje kumueleza mume wako?

Utaanza kwa kumuomba kama ana muda kwani unahitaji kuongea naye tena unaweza kumwambia mwende sehemu, sehemu ambayo kumetulia au mnaweza kwenda nje ya mazingira ya kawaida hasa siku za weekend (retreat) na itakuwa busara sana kumwambia mapema kabisa kabla ya kuondoka kwenda huko kwamba unataka mkaongee ili asije kukasirika kwa kudhani mnaenda kuenjoy kumbe unaenda kumweleza mambo mazito, kwa njia hii itamsaidia yeye kujisikia vizuri baada ya kuelezwa.

Mwambie unampenda sana na kwamba unajisikia hujamtendea haki kwa muda mrefu na sasa unatarajia kufanya mabadiliko, ndipo Mwangalie usoni, mshike mkono na mwambie

Mpenzi wangu, my honey naomba msaada wako”

Mwambie kila kitu, na tangu mwanzo mwambie kabisa kwamba maelezo yako yanaweza kuwa marefu kwa kuwa ni muhimu sana wewe kuongelea kila kitu na details zote kwa wakati mmoja ili akuelewe, na maliza maelezo yako kwa kuwambia, hii ndiyo sababu nimekuwa sipo wazi kwa sex kwa miaka yote kwani nilikuwa naogopa au nilikuwa na hofu ya kuumizwa tena, nilikuwa naogopa kupoteza kuaminiwa, nilikukosea”.

Je, unaweza kukusamehe?

Huo muda ambao mmeutumia pamoja, namna ulivyokuwa mkweli na wazi itamfanya huyo mwanaume kukubali kama ni kweli mumeo anakupenda na ana ubongo unaofanya kazi vizuri.

Namna ulivyomnyenyekevu na namna utakavyoongea kitu halisi kilichotokea katika maisha yako kama mwanamke mwenye hisia (sijasema ulie sana bali naamini utakapokuwa unamueleza naamini hutakwepa kutoa machozi na naamini mtakuwa na wakati mzuri kama wanandoa kuwa na connection ya kihisia kwa namna ya tofauti sana na mtaijenga ndoa kwa namna mpya kabisa.

Ni maombi yangu kwamba atakusamehe na mtaweza kuanza ukurasa mpya kimapenzi katika ndoa yenu.

Kukabiliana na Abuse

Namna ya kukabiliana na maisha ya abuse ya huko nyuma:

MOJA

Fahamu kwamba hata iweje kilichotokea katika maisha yako hapo zamani na kusababisha wewe kudhalilishwa huyu uliyeoana naye hana uhusiano nacho na wala hahusiki kabisa. Mara nyingi watu hulipa dhambi za matendo ya nyuma ya wazazi wao au ndugu zao hasa wanawake; kama wewe ni mwanamke ambaye ulikuwa abused Kumbuka kwamba huyo ambaye umeoana naye si baba yako au ndugu yako ambaye alikudhalilisha kimapenzi au kwa maneno.

Huyo ni mume wako, mwanaume anayekupenda wewe

MBILI

Kila unalojiambia mwenyewe ni muhimu sana (extremely important) katika kujikubali mwenyewe. Watu ambao huwa abused mara nyingi huificha ndani hiyo siri ya kuwa abused na kuendelea kuji-abuse wenyewe. Hukataa kuruhusu vitu ambavyo vingefanya wafurahie (enjoy) kwa kuwa wanajiona hawastahili na hawana thamani ya kupokea upendo na kufurahia.

Hivyo basi dumu katika kujisemea mwenyewe kila siku kwamba “Napendwa, Mungu ananipenda, mume wangu ananipenda, mchumba wangu ananipenda, watoto wangu wananipenda, ninastahili kupendwa na kupenda, mume wangu ananipenda na kunijali kama nilivyo, ananiheshimu kwa jinsi nilivyo, Bwana nisaidie kupenda kama unavyonipenda mimi” unaweza pia kusema haya maneno mbele ya kioo huku unatazama kwa macho yako ili kupata picha yako mwenyewe.

TATU

Fahamu kwamba upo katika safari. Mambo yaliyokupata ambayo yalitakiwa yasikupate ambayo wewe hukusababisha yataendelea kujirudia katika akili zako na mawazo yako katika nyakati tofauti. Kile kilitokea wakati mtoto kimesababisha kuwa na hofu na mashaka fulani katika maisha yako sasa. Namna unavyoitikia kihisia katika matukio tofauti tofauti leo ni matokeo ya abuse uliyopata wakati ukiwa mtoto.

Je, hii ina maana maisha kwako hayana maana?

HAPANA, hapana kubwa.

Unahitaji kufahamu kwamba kutakuwa na mabaki ya hizo hisia katika maisha na mtazamo wako mpya ni muhimu sana katika kukabiliana na hizo hisia zilizobaki.

NNE

Chagua kusema hapana kwa negativity. Kawaida usitunze kumbukumbu za mambo mabaya tu katika maisha yako. Kama kuna daftari umeandika mambo mabaya yaliyotokea katika maisha yako ni bora ukalitupa na kuandika daftari jipya ambalo utaandika mambo mazuri yaliyotokea katika maisha yako ili kuponywa haraka katika abuse yako.

Mawazo mabaya yanapojifunua kwako yafunike kwa mawazo ya vitu vizuri (positive), andaa orodha ya mambo mazuri ambayo umefanya katika maisha yako na yatunze na kuweka sehemu ambayo kila siku utayaona na kuyasoma. Kile unaona na kutunza katika akili zako ndicho kitakachotoka nje.

Ni Mpito, uwe makini!

Namna ya ku-handle maisha yanapokuwa tofauti na ulivyotegemea.

Kwa nini maisha ya ndoa ya watu ambao wapo katika umri wa makamo (midlife) huwa na crisis nyingi na wakati mwingine kuishi kwa kuachana au talaka?

Je, inawezekana ni kwa sababu ni wakati ambao familia huwa katika wakati wa mpito (transition) kwa maana kwamba familia ilizoea kuwa na baba, mama na watoto na sasa watoto wote wapo shule (vyuo) mama ana kazi yake au kubaki nyumbani mwenyewe na baba kwanza ndiyo anahaha kuongezewa cheo kazini au kupanda ngazi katika taaluma yake vitu kama kusoma Masters au PhD nk.

Suala hili (mabadiliko ya maisha kifamilia) huonekana ni dogo sana hata hivyo huweza kubadilisha dynamics za familia kwa namna ya ajabu sana.

Wapo wanawake ambao maisha yao asilimia kubwa tangu kuolewa huwa ni kuwa karibu na watoto, watoto huwa kila kitu kwao na wakati mwingine huenda mbali zaidi kwa kuwaweka waume zao pembeni na watoto hupewa first priority.

Matokeo yake mume huamua kujichimbia katika taaluma zake na kazi zake ambazo zinampa identity zaidi.

Pia huamua kuwa na maisha yake ambayo huko anaweza kutimiziwa mahitaji yake ya kihisia pia, kitu ambacho huwa hatari zaidi kwa ndoa yake.

Sasa watoto hawapo, wamebaki mke na mume wanatazamana, kibaya zaidi kila mmoja anamshangaa mwenzake kwani huvutii kama zamani, mume anamuona mke amekuwa jimama fulani maana kajazia huwezi amini kama ndiye yule ki-portable cha miaka 18 iliyopita. (Anyway mwanaume smart atakupongeza bila kujali una figure gani kwani kitendo cha kumzalia watoto ni sifa njema, hasa kama anafahamu nini hutokea huko kwenye chumba cha labour)

Mke naye anamuona mume ni mbabu fulani kwani ndo anagundua mzee kitambi kimeshuka ghafla na kuonekana amechuja hana jipya.

Wanajikuta hakuna tena kuvutiana kimwili.

Sasa nyasi kwenye nyumba ya jirani (yule mwanamke au yule mwanaume) huanza kuonekana za kijana zaidi ndipo utasikia sasa mwanaume anamtelekeza mke wake (miaka 20 kwenye ndoa) na kwenda kuoa kabinti kenye miaka karibu sawa na binti yake.

Inawezekana mke alikuwa ana mawazo kwamba siku moja yeye na mume wake watastaafu wakiwa ni watu kwenye legacy kubwa katika jamii hata hivyo ndoto zinayeyuka hivi hivi huku anaona kwa macho mawili yasiyo na upofu wowote.

Kwa kuwa kila mtu sasa ana ratiba yake inakuwa ngumu sana kwa wawili hawa kuwa na connection emotionally.

"THE GRASS IS ALWAYS GREENER ON THE OTHER SIDE OF THE FENCE"

AN AMERICAN PROVERB OF DISCONTENT

Hanisisimui Wala Kunivutia Tena!

Picha kwa hisani ya life in big London!

SWALI

Lazima niwe mkweli, mke wangu kwa sasa hanisisimui kimapenzi hata kidogo nikilinganisha na zamani.

Nimejitahidi lakini naona feelings zangu zipo mbali sana yaani hanivutii.

Je, hii ni kawaida kutoka hasa ndoa inavyozidi kuongeza umri?

Je, kuna kitu naweza kufanya?

MAJIBU:

Ni kweli kuna kitu unaweza kufanya na hali ikarudi na ukaanza kusherehekea raha ya mapenzi na mke wako. Unajua wanaume wengi huwa na mawazo (stupid) wakati wanaoa kama vile hujisemea “Nimempata mrembo wa nguvu, nitakuwa sasa napata sex siku zote, muda wowote ninaotaka, njia yoyote ninavyotaka, kwa kiasi ninachotaka maisha yangu yote yaliyobaki duniani na baada ya kuona ile kufika honeymoon tu unaanza kuogelea kwenye maraha.

Kutokana na swali lako namna umeuliza inaonesha kwamba wewe ni mbinafsi, selfish, maana umejiongelea wewe tu, si unajua kwamba ndoa ni kutoa na kupokea. Lengo la msingi la mke wako si kukutimizia wewe raha ya mapenzi tu bali kuwa msaidizi (helpmate & soul mate) kila eneo la maisha yako.

Hivyo na wewe pia unatakiwa kufanya kama mke wako kwa maana kwamba unatakiwa kumfikiria yeye kwanza na si wewe tu.

Je, unafahamu mke anahitaji kitu gani kutoka kwako?

Anahitaji wewe kuwa tender, mwanaume unayemsikiliza, unayempenda, unayemjali, mwanaume anaweza ku-share feelings na yeye na mwanaume umpofanya mambo muhimu kama hayo unaweza kuuona moyo mzuri wa mke wako na utamuona anazidi kuwa attractive kwako.

Nakupa hamasa wiki hii kuhakikisha unaandaa orodha ya vitu ambavyo unaona ni vya thamani sana kwa mke wako, utakapogundua thamani yake, emotions zako zitaanza kubadilika.

Inawezekana hutakuwa na feelings za zamani hata hivyo utapata feelings mpya na nzuri zaidi.

Sunday, May 30, 2010

Jana; Inavyoisumbua Leo!

Jema baada ya kufikisha miaka 7 ndipo aligundua kwamba baba yake ndiye anahusika na kumdhalilisha kimapenzi. Jema aliendelea kuwa abused hadi akiwa na miaka 13 ndipo siku moja yeye pamoja na mdogo wake wakaamua kutoroka nyumbani kutoka na mchezo huo mbaya wa baba yao.

Dada Naja alikuwa ndiyo yupo mwaka wa mwisho kumaliza chuo hata hivyo siku moja alipopata mwaliko na kijana wa kiume, kijana mstaarabu ambaye Naja aliamini wangakuwa na wakati mzuri kujuana na hata kuwa wachumba hata hivyo baada ya kunywa soda moja hakukumbuka tena kilichoendelea (pass out) hadi alipozinduka baada ya masaa mengi kujikuta yupo katikati ya msitu porini nusu uchi, alikuwa amebakwa na kuachwa porini peke yake nje ya mji.

Miaka yote hadi anakuwa mkubwa Catherine alishuhudia baba yake wa kambo na mlevi siku zote akimtumia mama yake kimapenzi (sex). Walipofika umri wa miaka 14 na 15 huyu baba wa kambo aliwalazimisha Catherine na mdogo wake kuwangalia yeye baba wa kambo akifanya sex na mama yao eti kuwafundisha namna hiki kitendo kinafanywa ili na wao wakiolewa wafahamu namna ya kuwaridhisha waume zao.

Ikitokea hawa watu hapo juu wakawa wameolewa basi kuna uwezekano mkubwa kwamba kuna aina ya struggle ambayo itaendelea katika ndoa zao linapokuja suala la sex.

Wataalamu wanatuambia kwamba kuna asilimia hadi 40 ya wanawake wameshafanyiwa abuse katika jamii zetu, asilimia ya wanaume ni ndogo kwa kuwa wanaume ni wagumu kukubali kwamba wamekuwa abused. Pia wanawake ni target nzuri kwa wanaume kuwafanyia sexual abuse.

Tukumbuke watoto huzaliwa na natural trust kwa wazazi wao au walezi wao, huweza kujirusha kwa wazazi au walezi hata kama ni zaidi ya mita 4 kwa sababu wanawaamini wazazi/walezi wao na watawashika au kuwakamata na kuwadaka vizuri na kuwa safe.

Pia kuna watoto ambao hulelewa na akina baba mdogo au baba mkubwa, kaka, dada, mjomba, shangazi, binamu na kujikuta wameumizwa kwa kufanyiwa vitendo vya ajabu (sexual abuse).

Wengine hulelewa na vituo vya kulea watoto tena na watu ambao sisi kama jamii tumewapa uhakika kwamba watoto hawa watakuwa ni salama kwa kuwa hawa watu ni watu wa Mungu hata hivyo mambo yamekuwa kinyume na matarajio yetu.

Watoto kama hawa hawafahamu upendo ni kitu gani kwani hawajapata nafasi ya kufahamu upendo ni kitu gani na nani hasa anaweza kukupenda bila kukuumiza.

Wanachoona ni ubabe, kukaliwa, kudhalilishwa na kuwa abused kwa jina la upendo.

Baada ya huyu mwanamke aliyedhalilishwa kimapenzi kumpata mwanaume ambaye amempenda, mwenye hamu ya mapenzi in natural way unajua nini kitatokea?

Wewe kama mwanamke ambaye ulikuwa abused utakumbana na wakati mgumu kwa sababu kwanza hujiona kama unastahili au huioni thamani yako kwamba unastahili kupendwa.

Matokeo yake unaweza kuanza kukwepa sex kwa kuwa picha ya zamani inaanza kujirudia wakati wa tendo la ndoa wakati huohuo mume wako anakuwa hajui lolote ni giza nene.

Kama ni mwanaume ambaye uliwahi kuwa abused unaweza kuwa the best father and husband in the world, unaweza kuwa unatabasamu, ukafanya mambo makubwa. Unaweza kuwakumbatia watu na kuwakaribisha warmly, hata hivyo ndani kabisa ya moyo wako, umejifunza kwamba ukiruhusu mtu awe karibu na wewe anaweza kukuumiza, hivyo unaamua kupaka uso wako rangi ya tabasamu na unajikuta unaishi katika pande mbili za dunia.

Abuse ni kitu kibaya sana na kigumu sana kuondokana nacho kwa sababu huweka alama ndani yako. Unaweza kuwasamehe wote waliokufanyia hivyo vitendo hata hivyo mabaki ya hivi vitendo huendelea kukuwinda mara kwa mara.

Kama hii ni moja ya habari ambayo unayo katika maisha basi ni kweli hii ni safari ambayo inahitaji msaada zaidi ya kawaida, pamoja na ushauri wa kitaalamu unahitaji msaada wa kiroho wa mtu ambaye anafahamu namna ya kushughulikia tatizo la abuse.

Je, kuna makovu yatabaki, jibu ni ndiyo, je kuna gharama ya kulipa jibu ni ndiyo na kama nitakwambia vinginevyo nitakuwa nakudanganya.

Hii haina maana hutajifunza kufurahia sex na mume wako au mke wako kwani Mungu aliiweka sex ni kitu cha kufurahia wewe ni yule unayempenda na ambaye mmeamua kuishi pamoja hadi kifo.

“What happened to you in the past has everything to do with how much you enjoy sex now”.

Saturday, May 29, 2010

If you want to get a man's attention, touch him.
If you want to get a woman's attention, whisper.

Friday, May 28, 2010

Ni Uamuzi wako!

Ni kawaida jua linapowaka na mionzi kutua juu ya siagi huweza kuifanya kuyeyuka na wakati huohuo mionzi ya jua ikipenya kwenye udongo wa mfinyanzi huufanya kuwa mgumu zaidi.

Joto la jua ndilo linaelekeza au kudhihirisha tabia za ndani za siagi na udongo wa mfinyanzi.

Tunapokuja kwenye suala la ndoa, maisha yetu hufanana sana na namna siagi na udongo wa mfinyanzi umeonesha tabia zake kutokana na mionzi ya jua.

Inawezekana partner wako anasumbua muda mwingi (irritant), hii hutokea, partner wako anakuhangaisha, anakufanya ujione kila kitu ni kichungu, anaudhi sana na unajisikia kutaka kumjibu kwa jeuri au kama inawezekana uandae power point presentation umwelekeza namna ambayo amekuwa boring kwako.

Hata hivyo mwanandoa mwenye busara huamua kufanya choice, kumjibu na kutenda kwa hekima ya kimungu au kumjibu jeuri na kutenda kwa kumkomoa (which is sinful way)

Ni rahisi mno kumlaumu mke wako au mume wako, pia mke wako au mume wako naye ana kila sababu za kukulaumu wewe.

Hata hivyo wewe ukiamua kutia njia ya kulaumiana (blame route) utaishia kuwa victim na kuharibu siku yako.

Unapoona mke wako au mume wako amewasha moto ambayo joto lake limeanza kupanda Kumbuka jambo moja na kujiambia mwenyewe kwamba:

Kwa kuwa mimi ni mtu mzima (mature person) mwenye uhuru wa ndani wa kuamua na kutoa maamuzi, nafahamu wazi kwamba uamuzi wangu ni wajibu wangu

Kuishi na kuwa na mtazamo wa aina hii si kawaida inahitaji hekima na busara na kujifunza kwani ni wanandoa wangapi huharibu siku kwa jambo dogo tu.

Kuijua hii siri ni rahisi kupenda na kujali mwenzi wako.

“Unaweza kuumizwa ila ni uamuzi wako kuamua kulaumu”

Mke wako au mume wako anaweza kukuudhi, kukusumbua, kukupigia kelele, kukuumiza na kukuhuzunisha hata hivyo unao uamuzi wa kuchagua kupita njia ya dawa ya moto ni moto au kumsamehe na kuendelea kufurahi na kumwangalia Mungu.

“Hakuna mtu anayeweza kukufanya usiwe na furaha hadi uamue mwenyewe”

Si Ukubwa wala Udogo!

Ukiangalia masuala ya “body image” namna watu na jamii kwa ujumla wanavyojihusisha hushangaza na kufurahisha sana.

Hata kama watu sasa wanafanya mazoezi ya mwili kuliko wakati mwingine bado pamoja na kufanya mazoezi na (program) mbalimbali suala la kujiamini na sura zetu limekuwa gumu.

Kwa mfano asilimia 35 ya wanaume na wanawake hawapendi namna walivyo katika mwonekano wao (appearance), kwa maana kwamba wanajichukia, wanajiona wangekuwa vinginevyo na si kama walivyo, wanatamani baadhi ya vitu vingebadilishwa.

Katika hili kundi asilimia 45 ya wanawake ambao hawana furaha kabisa namna walivyo na asilimia 30 ya wanaume ambayo hawaridhiki wapo tayari kufanya surgery ili wawe tofauti (Cash, Winstead & Janda, 1986).

Kama unajiona au unajihisi au unadhania hupo attractive unaweza kujibadilisha au kujikubali.

Ukijikubali una haki ya kufurahia ulivyo kwani hakuna mwingine kama wewe duniani isipokuwa wewe na tunakufahamu wewe kwa sababu ya namna ulivyo.

Pia kuna vitu ambavyo unaweza kuvibadilisha kama vile wembamba, unene, nywele nk na kuna vingine huwezi kuvibadilisha kamwe kama vile sura, urefu, matiti, makalio, uume nk inawezekana kufanyiwa surgery kunaweza kuleta mabadiliko hata hivyo uwe tayari “to pay the price”.

Kwa mfano matiti yanaweza kuongezwa size au kupunguzwa size hata hivyo pamoja na gharama kubwa pia matiti hupoteza uwezo wa kusisimka (sensation)

Kuna wanaoamini kwamba “bigger is better” na wao mtazamo wao upo kwenye matiti makubwa na wanaume wenye maumbile makubwa.

Hata hivyo tafiti zinaonesha kwamba matiti makubwa si sensitive kama matiti madogo na kuna sexologists ambao wanadai kwamba matiti madogo husisimka zaidi kwa kuguswa na huwapa ridhiko zaidi kuliko matiti makubwa.

Hata hivyo kwa kuwa wanaume wapo brainwashed na conditioned kwamba matiti makubwa ndiyo yenyewe hii imesababisha wanawake wengi kutoridhika na size za matiti yao na kuamua kufanyiwa surgery.

Ukweli ni kwamba ukubwa au udogo wa matiti hauna uhusiano (has nothing to do) na uzoefu na feelings za mapenzi.

It's what you do with what you've got that counts”.

Baadhi ya wanawake huwa na hofu kuhusiana na size ya uume wa mwanaume kuwa mdogo.

Inajulikana wazi kwamba udogo au ukubwa wa uume ni an unnecessary concern.

Kwa maelezo zaidi soma hapa.

Watu ambao ni sophisticated wanafahamu kwamba namna unafahamu sanaa ya mapenzi, ile asili ya kufahamu kupenda na kupendwa ni muhimu kuliko size za viungo.

Wanawake wapo brainwashed kwamba mwanaume mwenye maumbile makubwa ni fantastic, mtazamo kama huo lazima uhamishwe kuelekea kumpa mwanaume ufahamu wa kujua kupenda, kujali na kuwa mwororo

Pia kwa kujifunza zaidi soma hapa

Thursday, May 27, 2010

Unachotaka ni Mwili tu

Ulikuwa unanisubiri mlangoni kwa hamu kubwa, leo mmmm!

Mume amesafiri kwa wiki nzima kwa ajili ya business.

Akiwa huko safarini anamkumbuka sana mke wake na anaamua kufupisha muda wa safari ili arudi nyumbani Ubungo Dar es Salaam na kuwa na muda na mke wake na watoto.

Na kuwahi kurudi kwake anapenda iwe surprise kwa mke wake hivyo kutua tu uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere anaamua kuwahi nyumbani kwani kichwani tayari anawaza namna atakuwa na muda mzuri na mke wake (romantic sexual evening).

Ile anafika nyumbani anakutana uso kwa uso na mke wake ambaye kwa mshangao anamuuliza

Unatafuta nini sasa hivi hata umewahi kurudi mapema hivi tena bila hata taarifa? Ok, kwa kuwa umewahi kufika kawachukue watoto shule, na pia tuna kikao cha Walimu na wazazi so inabidi muda ukifika uende, pia mwanao John inabidi uongee naye kwani Walimu wamepiga simu kwamba anasumbua wenzake na pia unaporudi kuwachukua watoto shule pitia dry cleaner nichukulie nguo zangu, tena nilitaka kusahau dada yangu atakuja hivyo nitatoka naye kwenda dinner so wewe utabaki na watoto

Imekuwa too much kwa mwanaume ambaye ameahirisha safari yake na kuwahi nyumbani kumpa mke surprise na romantic sexual evening, sasa ni watoto, vikao, kupitia mizigo na mke na dada yake.

Wote mume na mke wapo kwenye kikao cha wazazi na Walimu na mume anaonekana amekasirika na kuvunjika moyo kwa namna jioni yake ilivyoharibiwa na makujumu ya mke wake.

Wanaporudi nyumbani kwenye gari mke na mume wote wapo kimya, kila mmoja anawaza yake. Mke amekasirika kwa nini mume pamoja na kusafiri kwa wiki zima mume hamuulizi wiki nzima Ilikuwaje na mambo gani alikutana naye. Mume naye amekasirika kwa sababu anaona mke wake hajampa respect na yupo unreasonable kumpa makujumu yote hayo na kumthamini dada yake na watoto kuliko yeye mume.

Baada ya dinner ambayo haikuwa nzuri sana kwani kila mmoja alikuwa na donge moyoni, mke na mume Wanaingia chumbani kulala.

Mume anajitahidi kuyamaliza kwa kutumia mtindo ule ule wa wanaume wengi kwa kumgusa (rub) mke wake mgongoni kitu ambacho ni njia nzuri ya kuanzisha ile kitu.

Mke anaguna na kumwambia “Hapana, nimechoka” kwa hasira anageuka mgongo kwa mgongo na kulala huku akiugulia na ameumizwa bila kusema kitu.

Mke naye akifahamu fika kwamba mume wake amekasirika anamwambia

Huwezi hata kufikiria yaani Unachotaka kwangu ni sex tu, you are insensitive!”

Mume kwa mshangao anamwambia mke wake

Siamini kama unaweza kusema hivyo, nimesafiri wiki nzima, narudi nyumbani hata kunipokea huwezi, salaamu hakuna, unachokijua ni watoto na dada yako, ninapojitahidi kuwa karibu na wewe unaniambia umechoka na mimi ni insensitive”.

Sasa mke naye amekasirika na kuumia anamjibu,

Hukuniuliza namna gani nimeshinda na watoto kwa wiki nzima na nimekutana na mambo gani, muda tu ambao unakuwa interested na mimi ni wakati unapotaka sex

Mume naye anamjibu mke,

Ndiyo nimesafiri wiki nzima hata hivyo unakumbuka wakati ule tumetoka kuoana, nikisafiri ulikuwa hata unaniambia niahirishe kukaa huko nikuwahi kwani ulikuwa na hamu na mimi, ulinisalimia mlangoni kwa furaha na upendo huku ukitabasamu na tunapeana busu, leo ninaporudi unaniangalia usoni na kusema Kwa nini upo nyumbani mapema hivi, asante sana na nashukuru kwani sikufahamu upo hivi

Kama wewe ni mtaalamu wa mambo ya ndoa, Je tatizo lipo wapi?

Wednesday, May 26, 2010

Kuwasiliana Chumbani

MAWASILIANO KATIKA TENDO LA NDOA

MOJA

Uwe mkweli, wazi, unayeongea moja kwa moja bila kuzunguka, usijifanye (pretending), uwe wewe halisi, kama hufahamu mke wako au mume wako anawaza nini, anahitaji kitu gani, au anajisikiaje (inawezekana hujui) muulize, usifanye kwa kudhania.

MBILI

Achana na imani potofu (nonsense) kwamba mwanaume anafahamu yote au anatakiwa awe anafahamu kila kitu kuhusu kufanya mapenzi (sex).

Hakuna mwanaume anayefahamu mwanamke anavyojisikia (feel), au ni kitu gani anahitaji ili kufika kileleni, kila mwanamke ni tofauti, ni muhimu sana kuwasiliana ninyi wawili.

Usiache kujadili ili kuondoa tatizo.

Kila mmoja lazima awasirishe kwa mwenzake namna au ni kitu gani kinamfanya ajisikie vizuri wakati wa sex

TATU

Sahau imani potofu kwamba mwanaume siku zote ndiye anatakiwa kuanza (initiate), au mwanaume anawajibika kuhakikisha sex inakuwa tamu, au Kumwachia mume afanye kila analoweza kukufanya wewe mwanamke ujisikie vizuri huku wewe umelala kama gogo huna habari unasikilizia tu.

Hayo ni mawazo potofu ambayo ni outdated.

Asilimia 80 ya wanandoa wanaoridhishwa kimapenzi ni pale ambapo mke na mume wote hujihusisha na kusaidiana kupeana raha ya mapenzi.

“Wonderful sex experience is when both partners are active”

NNE

Jitahidi sana kuachana na mawazo negative kuhusu mke wako au mume wako, ni muhimu sana kuwa makini kumlaumu mwenzako kutokana na matatizo yako.

Eti ooh ningefika kileleni kama angekuwa anajua mapenzi!

Au ooh kama ananipenda angechukua muda mrefu zaidi, angeninong’oneza maneno matamu, ange-massage mgongo wangu, angenichezea kisimi au uume wangu!

Hizi negative thinking ni vitu vinavyoficha udhaifu wa mhusika mwenyewe.

TANO

Hakuna kitu kinachoweza kuharibu mapenzi (sex) kama tabia ya kulaumiana.

SITA

Mara nyingi ni vizuri kuonesha namna ya kufanya kitu fulani kuliko kuelezea kwa maneno.

Kama mwanaume anachukua mkono wa mwanaume na kuupeleka kadi kwenye kisimi na kumuonesha namna ya kufanya huleta mawasiliano mazuri kuliko kubwabwaja maneno.

SABA

Usitegemee maisha ya mapenzi (sex) kuwa juu siku zote.

Namna wanandoa wanashiriki tendo la ndoa hutofautiana kila baada ya muda fulani. Hakuna kitu kinaitwa perfect, ingawa ni kweli una haki ya kufurahia maisha mazuri ya sex.

Ni muhimu kuongelea “new things” na msisahau kucheka pamoja pia.

Mume Akupende!

Haijalishi ni kazi gani mume anafanya anastahili kupewa appreciation!

Wanaume wakikutana wenyewe kwa wenyewe kama hawafahamiani swali la kwanza kuulizana ni “unafanya kazi gani?”
Sababu ya msingi ni kwamba wanaume wengi suala la kazi ni kitambulisho (identity)
Ndivyo walivyoumbwa na Mungu na hiki ni kitu wanachozaliwa nacho kujikuta ni mtu wa kwenda kuwinda, kulima, kufanya kazi kwa ajili ya familia yake.
Kufanya kazi ni jambo la msingi kwake.
Akipata ugonjwa anaweza kupigana na kuhimili kila aina ya msongo wa mawazo au mgandamizo wa damu hata hivyo linapokuja suala la kazi kwake huwa maumivu ni makubwa kiasi cha kuwa na stress au depression.
Mwanaume anaweza kusimama imara hata katika ugonjwa unaoleta mauti kama cancer lakini si suala la kupoteza kazi au business.
Mwanaume mmoja baada ya kufanya deal la uhakika kwa kutengeneza Mamilioni ya pesa, kwa furaha akaenda nyumbani kwa mke wake kumwambia hizo habari njema na mke wake akamjibu kwa mkato “sawa nimekusikia” then akaendelea na kazi zake pale nyumbani.
Mume alikatishwa tamaa na kuvunjwa moyo kiasi cha kutoa maamuzi kwamba kuanzia hapo hatamshirikisha mke wake jambo lolote au maamuzi yoyote kwani hakutegemea kama mke wake angejibu kwa mkato vile na kuonekana alichofanya hakina maana.
Wanawake wengi hawafahamu umuhimu ambao wanaume wameuweka katika kazi zao na kwamba ukimshukuru kwa kazi anayofanya basi anaweza kukuonesha upendo wa ajabu.
Fikiria wewe ni mwanamke sasa umegundua kwamba ni mjamzito na unaenda kumweleza mume wako naye anakujibu “sawa” then anaendelea kuangalia TV utajisikiaje?
Basi ndivyo mume wako hujisikia pale Unapokuwa hutambua kazi yake hata kama wewe unafanya kazi na kupata fedha kubwa zaidi.
Mwanamke anaweza kuamua au kuchagua kufanya kazi au kuwa nyumbani na kulea watoto, hata hivyo mwanaume anaweza kuchagua kufanya kazi au kwenda jela.
Ni kweli mwanaume mwema huolewa kwa sababu ya UPENDO na si FEDHA, hata hivyo mwanamke huyu mwema huwa na hekima na maarifa ya kufahamu sifa ya ndani ya huyu mwanaume kama anaweza kujenga kiota na kuhudumia vifaranga kwa chakula, mavazi na malazi maisha yao yote.
Je umewahi kumshukuru Mume wako kwa kazi anayofanya?
Kwa mwanamke ambaye anataka kuonesha respect kwa mume wake anaweza kujaribu kuandika hata message au note na kuiweka hata kwenye Lunch box yake na kumwambia “ mpenzi mume wangu nashukuru sana kwa namna unajituma kufanya hiyo kazi kwa ajili ya familia” au vyovyote unavyotaka wewe.
Pia unaweza kumshukuru kwa uhuru aliokupa wewe mwanamke kufanya kazi au kukaa nyumbani na yeye kufanya kazi.
Wapo wanawake ambao huwaza mara kwa mara kwamba wangewashukuru waume zao kwa kufanya kazi, hata hivyo kuwaza peke yake si lolote unachotakiwa kufanya ni kumshukuru au kumwambia.
Je, utajisikiaje mume ambaye anasema kwamba huwa anafikiri mara kwa mara kukwambia anakupenda na hajawahi kukwambia anakupenda!
Ukweli mahusiano ni two way street, mume anatakiwa kukwambia “ANAKUPENDA” na wewe unatakiwa siku moja kumwambia mumeo “Asante sana nashukuru kwa kazi unayofanya ambayo inatupa fedha na maisha
Nakuahidi atafanya mambo ya ajabu sana kuhusiana na kukupenda wewe kwa sababu ataamini wewe ni mwanamke ambaye unaamini katika yeye.
Mume wako anajiona unamshukuru kwa kazi anayofanya pale tu
Pale unapomwambia kwa maneno au maandishi kwamba kile anafanya kina maana kwako na familia.
Unaelezea imani yako katika taaluma yake.
Unasikiliza stories mbalimbali kuhusu kazi zake na taaluma yake, inaweza kuwa ni magari, ualimu, Computer, forestry, nk.
Kumsaidie kukamilisha ndoto zake kama wakati ule wa kuchumbiana.
Hulalamika kuhusiana na kazi zake