"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, May 3, 2010

Ameniumiza Mno!

Kaka Mbilinyi,

Kwanza nashukuru sana kwa masomo mbalimbali yanayohusu mahusiano kweli tunajifunza.

Mimi ni mwanamke ambaye nipo kwenye ndoa mwaka wa 3 sasa hivi karibuni mume wangu amenifanyia kitu ambacho kimenifanya nijione nachanganyikiwa na sijajua kama ni dalili kwamba kuna matatizo kichwani mwake.

Kuna siku wakati wa tendo la ndoa mume wangu alinipiga kwa nguvu sehemu siri (niliumia sana clitoris), niliumia sana (maumivu) na ilibidi pale pale kila kitu kisimame.

Je, umewahi kusikia mwanaume akimfanyia huo mchezo mke wake? Inanichanganya sana, nisaidie!

AMM

Dada AMM Pole na yaliyokupata!

Ukweli sijawahi kusikia mwanaume anapiga sehemu za siri kwa mke wake au mpenzi wake na sijajua hiyo tabia ameipata wapi au ni mdudu gani alimwingia kichwani mwake wakati tete kama huo ambao naamini wewe ulijiweka tayari tayari kujipatia raha kwa huyo umpendaye.

Hata baada ya kusema hivyo bado nakiri kwamba binadamu ni viumbe wa ajabu sana linapokuja suala la mapenzi (sex) kwa maneno mengine kuna wanaume na wanawake ambao hufurahia kufanya vitendo ambavyo mimi na wewe hatuwezi kuvumilia na tungeviepuka kwa gharama zozote.

Ninachokuhakikishia ni kwamba haina haja kuchanganyikiwa, jambo la msingi ni kwamba hiyo tabia huwezi kuivumilia na ulifanya vizuri kusimamisha zoezi zima na naamini ulimweleza wazi kwa mapana, marefu na kina huku ukionesha upendo na heshima (respect) kwamba kitendo alichokufanyia hakiwezi kuvumilika na kilikuumiza sana na aache na kama hujafanya (jadili pamoja) basi kama mke na mume mnatakiwa kukaa na kujadili tena kwa upendo na uwazi.

No comments: