"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, May 19, 2010

Anakimbilia Chini, nifanyeje?

SWALI:

Mimi na mume wangu tulikuwa na maisha mazuri sana linapokuja suala la tendo la ndoa hata hivyo hapa karibuni amekuwa na kawaida ya kwenda moja moja kwenye intercourse bila maandalizi ya kutosha au kusisimuana na kuniandaa kiakili na kimawazo kabla ya kuingia chumbani tofauti na zamani na hii inanifanya nijione labda simvutii.

Napenda aniambie maneno matamu na mapya, napenda kukumbatiwa, busu, kushikana shikana na kuchezeana; vitu kama hivi hunifanya nijione nipo close na yeye na tayari kumpa mwili.

Je, nifanyeje?

JIBU:

Asante kwa swali zuri ambalo limelenga kuonesha ukweli kwamba wanaume tupo tofauti na wanawake linapokuja suala la sex na kwamba bila kuwa makini mume anaweza kuharibu mambo.

Asilimia kubwa ya wanaume baada ya kuoa huchukua miezi 6 hadi 12 na wakati mwingine mapema zaidi kuanza kile tunaita “short-cut sex’” kwa maana kwamba wao hukimbilia moja kwa moja kwenye tendo lenyewe na kuruka suala zima la maandalizi.

Hii haina uhusiano na suala la mke kupendeza na kuvutia au la bali ni mazoea (easy and comfortable), wanaume hufika Mahali na kujiuliza kwa nini kuzunguka alphabeti zote kuanzia A – Z bila ya kwenda moja kwa moja down there!

Ukweli unabaki pale pale kwamba kuruka kipengele cha maandalizi ya tendo la ndoA huathiri sana mwanamke kwani wao huhitaji kati ya dakika 20 hadi 25 kwa ajili ya kumsisimua kiakili na kimwili na hii hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke na pia hata mwanamke mmoja bado anakuwa tofauti kutokana na siku katika mzunguko wake, na pia mwanamke huyo huyo hutofautiana namna ya kusisimuliwa kila baada ya miaka kadhaa, ndiyo maana ni muhimu sana kwa mwanaume kuongeza ujuzi kila miaka inavyozidi kwenda.

+++++++++++++++++++++

Jambo la msingi ni wewe kuongea naye wazi kwamba apunguze mwendo na mwambie kwa upendo na hekima ya hali ya juu kwani suala la sex ni moja ya maeneo tete sana kwenye ndoa.

Au mkiwa wote kwenye mood na mmeanza kwa kubusiana; ukishaona anapeleka mkono kule chini mshike na kuupeleka pale unapenda uende kwanza bila kuongea chochote.

Na ukiona ameondoa pale umeupeleka na wewe hajaridhika; urudishe tena pale pale na mwambie vile unajisikia raha na msisimko Mahali anakuchezea au kukugusa na unaweza kuongea maneno ya kimahaba zaidi ili umwingize mjini.

Kama ukiona bado hakuelewi hapo inahitaji kukaa pamoja (hasa mkiwa relaxed), mwambie ni kweli mpo busy sana hata hivyo ingependeza zaidi kama mtakuwa na muda zaidi katika kuandaana kimapenzi kwanza kwa wewe kumpa respect namna anavyokufurahisha kimapenzi.

JE WANAWAKE WANA MTAZAMO GANI KUHUSU TENDO LA NDOA?

Inajulikana wazi kwamba wanaume wengi ni ignorant namna akili na moyo wa mwanamke unavyofanya kazi hasa linapokuja suala la sex.

Kama ukiwauliza wanawake 100 kujua wanasemaje au mtazamo gani kuhusiana na suala la tendo la ndoa asilimia zaidi ya 90 watakwambia wanachokipenda kwenye tendo la ndoa ni:

Just hold me close and be tender, forget about the act

Wanawake wengine wanasemaje?

Ninachokipenda sana kuhusiana na tendo la ndoa ni kile kitendo cha kupeana maneno matamu ya kimahaba na mabusu na kushikana shikana kunakoleta msisimko wa kimapenzi, kinachofuata ni usumbufu tu na kumalizana nguvu!

Nina uhakika sex ilikuwa designed kuwapa raha wanaume.

Naomi

Ninapenda sana kuwa na watoto 3 na baada ya kupata hao watoto 3 kwa kweli nitafurahi sana kama kila mmoja mimi na mume wangu kila mtu awe na chumba chake. Sex haina maana yoyote kwangu.

Josyline

Ninachokipenda sana kwenye suala la tendo la ndoa ni kile kitendo cha “cuddling and caressing” kushikana shikana/ngozi kwa ngozi/mwili kwa mwili bila kuhusisha sex organ, na maneno matamu ya kimahaba yanayoendana na anavyoonesha kunijali.

Bila hivyo huwa nahisi mume wangu ananibaka!

Jane

Kusema kwamba maneno matamu ya kimahaba na kushikana shikana ndiyo inatosha kwangu ni sawa na kuridhika na harufu ya pilau bila kuila.

Raha ni kulila pilau lenyewe.

Helena

Bila maneno matamu na kukumbatiwa, kubusiana na kushikana shikana kimahaba nahisi kama wanyama vile. Kwa miaka 10 sikupenda kabisa sex kwani mume wangu aliyefariki ni mtu wa short-cut na niliyenaye sasa ananifanya nijione nipo “in heaven’

Joan

Napenda sana maneno matamu na “cuddling/caressing and just holding” kwani mume wangu nikianza kuongea tu ananiambia nyamaza unaharibu mambo!

Happiness

HITIMISHO

Tendo la ndoa huwa kitu kinachoridhisha pale wawili wanaopendana (mke na mume) wanapokuwa wamepotelea ndani ya moto wa mapenzi unaoweza kupoteza fahamu zao na kuzama katika mahaba.

Pale tendo la ndoa Linapokuwa kama gari linalobeba upendo wao; hivyo ndivyo ilikuwa tangu mwanzo.

1 comment:

Anonymous said...

HAHAHAHAH KKA HII KALI NI WKELI KABIAS HAYA MAMABO YAPO BE BLESSED.