"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, May 31, 2010

Hanisisimui Wala Kunivutia Tena!

Picha kwa hisani ya life in big London!

SWALI

Lazima niwe mkweli, mke wangu kwa sasa hanisisimui kimapenzi hata kidogo nikilinganisha na zamani.

Nimejitahidi lakini naona feelings zangu zipo mbali sana yaani hanivutii.

Je, hii ni kawaida kutoka hasa ndoa inavyozidi kuongeza umri?

Je, kuna kitu naweza kufanya?

MAJIBU:

Ni kweli kuna kitu unaweza kufanya na hali ikarudi na ukaanza kusherehekea raha ya mapenzi na mke wako. Unajua wanaume wengi huwa na mawazo (stupid) wakati wanaoa kama vile hujisemea “Nimempata mrembo wa nguvu, nitakuwa sasa napata sex siku zote, muda wowote ninaotaka, njia yoyote ninavyotaka, kwa kiasi ninachotaka maisha yangu yote yaliyobaki duniani na baada ya kuona ile kufika honeymoon tu unaanza kuogelea kwenye maraha.

Kutokana na swali lako namna umeuliza inaonesha kwamba wewe ni mbinafsi, selfish, maana umejiongelea wewe tu, si unajua kwamba ndoa ni kutoa na kupokea. Lengo la msingi la mke wako si kukutimizia wewe raha ya mapenzi tu bali kuwa msaidizi (helpmate & soul mate) kila eneo la maisha yako.

Hivyo na wewe pia unatakiwa kufanya kama mke wako kwa maana kwamba unatakiwa kumfikiria yeye kwanza na si wewe tu.

Je, unafahamu mke anahitaji kitu gani kutoka kwako?

Anahitaji wewe kuwa tender, mwanaume unayemsikiliza, unayempenda, unayemjali, mwanaume anaweza ku-share feelings na yeye na mwanaume umpofanya mambo muhimu kama hayo unaweza kuuona moyo mzuri wa mke wako na utamuona anazidi kuwa attractive kwako.

Nakupa hamasa wiki hii kuhakikisha unaandaa orodha ya vitu ambavyo unaona ni vya thamani sana kwa mke wako, utakapogundua thamani yake, emotions zako zitaanza kubadilika.

Inawezekana hutakuwa na feelings za zamani hata hivyo utapata feelings mpya na nzuri zaidi.

1 comment:

Anonymous said...

"Mh! hapana si kawaida, kaa chini fikiria mara mbili nijuavyo mimi ndoa ni ndoa tu na mke/mume ni yule yule jana leo na hata milele! but angalia mwenendo wako mzima watu unaokutana nao mara kwa mara then acha kumfananisha mwanamke yoyote na mkeo coz hakuna mzuri kama mkeo so anzia hapo kwanza kama una mapenzi ya dhati na huyo mkeo, ni hayo tu!"