"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, May 7, 2010

Hawezi!

Hakuna mwanaume anaweza kutimiza mahitaji YOTE ya kihisia kwa mwanamke” Hii ina maana mume wako hawezi kukutimizia mahitaji yako yote ya kihisia (emotional needs)

Mara nyingi mwanaume anapokuwa amesusa kuwa karibu na mke wake; mke huanza kuwa demanding ili kutimiziwa mahitaji yake.

Na mume anapoona hawezi kutimiza mahitaji ya mke wake hujiona ni failure na loser na njia sahihi kwake ni kwenda pangoni.

Mwanamke hisia zake ni mfano wa barabara kubwa (8 lanes) au grand canyon tofauti na mwanaume ambaye hisia zake (emotions) ni mfano wa kajinjia ka kwenda msituni.

Hii ina maana hata kama tutawapanga wanaume wote katika mtaa unaoishi hawataweza kutimiza mahitaji yako emotionally.

Unahitaji kumwangalia Mungu peke yake ambaye anaweza kukutimizia mahitaji yako yote kihisia na si mwanaume katika planet earth!

Sana sana mume wako atajitahidi sana hata hivyo usikate tamaa pale unapoona hajatimiza kwa kadri unavyotaka wewe.

No comments: