"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, May 30, 2010

Jana; Inavyoisumbua Leo!

Jema baada ya kufikisha miaka 7 ndipo aligundua kwamba baba yake ndiye anahusika na kumdhalilisha kimapenzi. Jema aliendelea kuwa abused hadi akiwa na miaka 13 ndipo siku moja yeye pamoja na mdogo wake wakaamua kutoroka nyumbani kutoka na mchezo huo mbaya wa baba yao.

Dada Naja alikuwa ndiyo yupo mwaka wa mwisho kumaliza chuo hata hivyo siku moja alipopata mwaliko na kijana wa kiume, kijana mstaarabu ambaye Naja aliamini wangakuwa na wakati mzuri kujuana na hata kuwa wachumba hata hivyo baada ya kunywa soda moja hakukumbuka tena kilichoendelea (pass out) hadi alipozinduka baada ya masaa mengi kujikuta yupo katikati ya msitu porini nusu uchi, alikuwa amebakwa na kuachwa porini peke yake nje ya mji.

Miaka yote hadi anakuwa mkubwa Catherine alishuhudia baba yake wa kambo na mlevi siku zote akimtumia mama yake kimapenzi (sex). Walipofika umri wa miaka 14 na 15 huyu baba wa kambo aliwalazimisha Catherine na mdogo wake kuwangalia yeye baba wa kambo akifanya sex na mama yao eti kuwafundisha namna hiki kitendo kinafanywa ili na wao wakiolewa wafahamu namna ya kuwaridhisha waume zao.

Ikitokea hawa watu hapo juu wakawa wameolewa basi kuna uwezekano mkubwa kwamba kuna aina ya struggle ambayo itaendelea katika ndoa zao linapokuja suala la sex.

Wataalamu wanatuambia kwamba kuna asilimia hadi 40 ya wanawake wameshafanyiwa abuse katika jamii zetu, asilimia ya wanaume ni ndogo kwa kuwa wanaume ni wagumu kukubali kwamba wamekuwa abused. Pia wanawake ni target nzuri kwa wanaume kuwafanyia sexual abuse.

Tukumbuke watoto huzaliwa na natural trust kwa wazazi wao au walezi wao, huweza kujirusha kwa wazazi au walezi hata kama ni zaidi ya mita 4 kwa sababu wanawaamini wazazi/walezi wao na watawashika au kuwakamata na kuwadaka vizuri na kuwa safe.

Pia kuna watoto ambao hulelewa na akina baba mdogo au baba mkubwa, kaka, dada, mjomba, shangazi, binamu na kujikuta wameumizwa kwa kufanyiwa vitendo vya ajabu (sexual abuse).

Wengine hulelewa na vituo vya kulea watoto tena na watu ambao sisi kama jamii tumewapa uhakika kwamba watoto hawa watakuwa ni salama kwa kuwa hawa watu ni watu wa Mungu hata hivyo mambo yamekuwa kinyume na matarajio yetu.

Watoto kama hawa hawafahamu upendo ni kitu gani kwani hawajapata nafasi ya kufahamu upendo ni kitu gani na nani hasa anaweza kukupenda bila kukuumiza.

Wanachoona ni ubabe, kukaliwa, kudhalilishwa na kuwa abused kwa jina la upendo.

Baada ya huyu mwanamke aliyedhalilishwa kimapenzi kumpata mwanaume ambaye amempenda, mwenye hamu ya mapenzi in natural way unajua nini kitatokea?

Wewe kama mwanamke ambaye ulikuwa abused utakumbana na wakati mgumu kwa sababu kwanza hujiona kama unastahili au huioni thamani yako kwamba unastahili kupendwa.

Matokeo yake unaweza kuanza kukwepa sex kwa kuwa picha ya zamani inaanza kujirudia wakati wa tendo la ndoa wakati huohuo mume wako anakuwa hajui lolote ni giza nene.

Kama ni mwanaume ambaye uliwahi kuwa abused unaweza kuwa the best father and husband in the world, unaweza kuwa unatabasamu, ukafanya mambo makubwa. Unaweza kuwakumbatia watu na kuwakaribisha warmly, hata hivyo ndani kabisa ya moyo wako, umejifunza kwamba ukiruhusu mtu awe karibu na wewe anaweza kukuumiza, hivyo unaamua kupaka uso wako rangi ya tabasamu na unajikuta unaishi katika pande mbili za dunia.

Abuse ni kitu kibaya sana na kigumu sana kuondokana nacho kwa sababu huweka alama ndani yako. Unaweza kuwasamehe wote waliokufanyia hivyo vitendo hata hivyo mabaki ya hivi vitendo huendelea kukuwinda mara kwa mara.

Kama hii ni moja ya habari ambayo unayo katika maisha basi ni kweli hii ni safari ambayo inahitaji msaada zaidi ya kawaida, pamoja na ushauri wa kitaalamu unahitaji msaada wa kiroho wa mtu ambaye anafahamu namna ya kushughulikia tatizo la abuse.

Je, kuna makovu yatabaki, jibu ni ndiyo, je kuna gharama ya kulipa jibu ni ndiyo na kama nitakwambia vinginevyo nitakuwa nakudanganya.

Hii haina maana hutajifunza kufurahia sex na mume wako au mke wako kwani Mungu aliiweka sex ni kitu cha kufurahia wewe ni yule unayempenda na ambaye mmeamua kuishi pamoja hadi kifo.

“What happened to you in the past has everything to do with how much you enjoy sex now”.

No comments: