"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, May 4, 2010

Je, Ni Vibaya?

Huu afadhari; lakini siyo huo unaouweka kifuani!

Je, kuna ubaya wowote kuwa karibu na mchumba wako (kulala kitanda kimoja bila sex huku tupo uchi) kabla ya ndoa?


Kwa kuwa swali linako linazungumzia uchumba na si ndoa na umeongezea kipengele cha kulala kitanda kimoja tena uchi, kwanza kabla ya kufika mbali kile kitendo cha kulala pamoja kitanda kimoja kinaleta picha ya ukaribu wa kimapenzi.

Swali kubwa linalonishangaza ni kwa nini mfike hadi hatua ya kulala pamoja tena uchi wakati hamhitaji kufanya sex?

Tukio gani limewafanya kuamua kutafuta sehemu ambayo mtakuwa wewe ni mchumba wako, chumba ambacho mtakuwa wawili tu, mkubaliane kulala kitandani kila mmoja aanze kutoa nguo kuanzia layer ya nje hadi chupi, kinachozangaza zaidi mlale pamoja uchi; kama si kumtafuta shetani maneno ni kitu gani!

Utawezaje kuweka makaa ya moto kifuani na usiungue?

Kumbuka aina yoyote ya ukaribu unaohusisha hisia za mapenzi ni mali ya ndoa kati ya mke na mume na si uchumba.

Ikitokea mwanaume na mwanamke ambao hawajaoana wakaenda kulala kitanda kimoja huku wapo uchi bila kufanya mapenzi bado ni dhambi.

Point ya msingi ni kile kitendo cha kuwa uchi, kuangalia uchi, kugusa na kuchezeana mwili nk.

Vitu hivi vyote vinatakiwa kutunzwa (reserved) kwa ajili ya marriage bed kati ya mke na mume.

Mungu anaagiza kwa kijana wa kiume na wa kike kuwa safi (morally pure) hadi ndoa.

Kuna maandiko mengi tu yanayozungumzia kwa upana, marefu na kina kuhusiana na mipaka ya kuweka kwa wachumba kabla ya ndoa.

1 Wakorintho 6:18, Efeso 5:3, Wakolosai 3:5, 1 Wathesolanike 4:2,

Ukaribu wowote unaohusiana na kuchezeana mwili (touching, caressing, cuddling, kisses etc) na mwingine au wote kuwa uchi hata bila sex ni kuvuka mipaka na ni DHAMBI.

No comments: