"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, May 9, 2010

Jina baada ya kuolewa!

Je, nibadilishe jina baada ya kuolewa?

Utangulizi.

Hivi karibuni kumekuwa na kujiuliza kwingi kwa akina dada ambao wanatarajiwa kuolewa kama anaweza kubadilisha jina la ukoo na kulichukua lile la mume wake.

Wengi wamejikuta wakifanya huku hawajafahamu maana au kwa nini wanachukua hatua kama hiyo hata hivyo ni vizuri kufanya jambo ambalo una uhakika na ufahamu wa kutosha kuliko kufuata tu traditions na taratibu ambazo ni kama kufuata mkumbo.

Pia kuna maswali kwamba je, kubadilisha jina baada ya kuolewa ni suala la kibiblia au ni mapokeo tu na zaidi kwa nini wanaobadili majina ni wanawake na si wanaume.

Je, kubadili jina nyakati za leo kuna manufaa yoyote kimaadili na kiimani?

Wanaharakati wa mambo ya wanawake (feminist) wanasema haina haja kubadili jina maana mwanamke anapoteza identity yake na kila kukicha wanawake wanaoolewa kwa hiari yao huamua kubadilisha majina yako na kuendelea kufurahia maisha ya ndoa na waume zao wapya.

Enzi za Biblia:

Kihistoria nyakati nyingi za nyuma hata enzi za Biblia watu walitambulika jina moja tu bila jina la ukoo.

Wengi walijulikana kwa makabila, tamaduni, mji anaotoka, kazi anayofanya au cheo alicho nacho katika jamii.

Mfano Mfalme Daudi, Yesu wa Nazareth, Mary Magdalena nk

Majina yalikuwa katika mfano wa business card kwani majina yalieleza wanatoka wapi na wanafanya nini, tofauti na majina yetu leo ambayo ni kukutambulisha wewe tu kuwa tofauti na mwingine na hayaelezi unafanya kazi gani, unatoka wapi nk.

Pia nyakati za Biblia Mungu alihusika kubadilisha majina kutokana kupewa makusudi na wajibu mpya.

Kama vile;

Abram kwenda Abrahamu,

Sarai kwenda Sara

Sauli kwenda Paulo

Kwa nini anayebadilisha jina ni mwanamke na si mwanaume?

Traditions ambazo ni biblical zinaonesha kwamba kwanza Adamu aliumbwa ndipo Eva (Hawa) na Eva alitoka katika ubavu wa Adamu.

Adamu na Eva baada ya kuunganishwa wamekuwa mume na mke yaani mwili mmoja (one couple).

Mungu amewaunganisha mwanaume mmoja na mwanamke mmoja kufanya kitu kimoja na mke ndiye amemfuata mume (kipande cha ubavu kilichotolewa ili kumuumba Eva) kuwa kitu kimoja kupitia agano la ndoa.

Mbele za Mungu wanandoa wawili mke na mume huwa ni kiumbe kipya kimoja kinachoitwa ndoa moja (couple), hii ina maana kwamba ingawa mwanaume mmoja ambaye hajaoa huonekana ni mtu mzima kiroho bado huwa nusu na huhitaji kuunganishwa na nusu nyingine ya mwanamke kufanya kitu kimoja yaani ndoa.

Mwananaume huwa hajakamilika hadi anapooa na mwanamke huwa hajakamilika hadi aolewe.

Mwanamke kumchukua jina la mume ni kuipa heshima ndoa na kudhihirisha kuwa kitu kimoja kipya kimezaliwa.

Mke anapoolewa hudhihirisha kwa ulimwengu kuwa amepata identity mpya na anatambua uimbaji wa kimungu kupitia ndoa (acknowledge God’s new creation).

Baada ya kuolewa anaingia kwenye agano jipya kati ya mke na mume na Mungu.

“she becomes part of something greater than herself, the union created and blessed by God”.

Isipokuwa:

Jamii nyingi za kilatini nchi kama Italy, France, Belgium, Netherlands (ambao wengi ni Christian); mwanamke hutambulika tu in public kwamba amebadilisha jina lakini kwenye documents zote za kisheria (legal contract) jina la ukoo la mama huwa jina la katikati katika majina matatu ya watoto hii ni kuhakikisha historia za familia zao (genealogy) zinadumishwa.

6 comments:

Anonymous said...

Binafsi naamini kubadilisha jina au kutobadilisha jina ni personal choice ya mke na mume (wanandoa wapya) pia wanaweza kujadili namna wanaweza kuwapa majina watoto wao.
Hakuna uhusiano kati ya kubadilisha jina na mwanamke kuwa mtii kwa mume, nasema hivyo kwa sababu jina unalolibadilisha halikufanyi uwe namna ulivyo, upo namna ulivyo kwa sababu ya choices unazofanya katika maisha yako.

Anonymous said...

Katika tamaduni nyingi (hadi sasa) wanawake hawawezi kumiliki mali baada ya kufa mume.
Mama na watoto huendeleza jina na kuendelea kumiliki mali na fedha alizoacha baba kama ikitokea tatizo la kifo au kupotea moja kwa moja. Mama huwa kundi moja na watoto chini ya jina la baba wa watoto.
Ingawa kwa leo hata ukiishi na mke kwa miezi kadhaa na kutumia anuani moja basi mali zitagawanywa nusu kwa nusu, mke atajichukulia nusu yake na kuamua kukaa na watoto au kuanza mbele (sehemu ambazo sheria ina meno)

Pia baadhi ya jamii ndoa ni usalama wa mwanamke kutokana na vitisho vya mwili wake, usalama kutoka kwa wanaume wengine, wanyama na kila ina ya mother nature; hivyo kuchukua jina la mume kwake ni fahari na kuonesha yeye ni “belong to” mume wake na hupokea heshima na ulinzi/usalama katika jamii husika.

Anonymous said...

Nilizaliwa katika familia ambayo baba alikuwa hopeless na sipendi kabisa kusikia jina lake hivyo baada ya kuolewa tu nilibadilisha jina na kumchukua jina la mume wangu na kuendelea na maisha na kuangalia future, najisikia fahari kuitwa Mrs .....

Anonymous said...

Feminism ni chaguo na haina haja kuwakataza wanawake wengine ambao wanapenda sana kubeba majina ya waume zao hivyo naamini kila mwanamke ana uhuru wa kufanya kile anakipenda.

Anonymous said...

Natarajia kuolewa miezi sita ijayo na nina hamu sana kubadilisha jina na kutumia jina la ukoo la mume wangu, napenda iwe hivyo, that is my choice!

Anonymous said...

sisi wanawake tunapenda kutumia jina ka ukoo la upande wa mume, hata ,mie nilianza kujiita kabla na napenda sana sijui kwanini nadhani ni asili yetu wanawake